Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

TAARIFA KUTOKA BENKI KUU YA TANZANIA KUHUSU TOLEO LA NOTI MPYA

-
Rehema Mwinyi.

Gavana Mkuu wa Benki Kuu ya Tanzania Prof.Benno Ndulu akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam Kuhusu noti mpya zinazotumika nchini kuwa zina ubora na viwango vya kimataifa na kuwataka wananchi kuwa makini katika kufwatilia na kuzitambua alama muhimu za noti halali ikiwemo ile ya kutoa rangi pindi inaposugulia kwenye karatasi nyeupe.Kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Kibenki (BOT) Bw Emmanuel Boaz
Toleo jipya la Noti za Tanzania,Marekani  na Rwanda ambazo zina ubora na kiwango cha kimataifa zikionyeshwa mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Jana.Picha na Aron Msigwa-MAELEZO
---

BENKI KUU YA TANZANIA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
 

KUHUSU TOLEO LA NOTI MPYA
 


1. Mwezi Januari 2011 Benki Kuu ya Tanzania ilitoa toleo jipya la notiza Shilingi 500, 1000, 2000, 5,000 na 10,000. Baada ya kipindi chatakriban mwezi mmoja sasa, pamejitokeza dukuduku na maswali mbalimbali
kutoka kwa wananchi. Kwa kuwa ni maswali ambayo yakijibiwa yatasaidiakuelimisha jamii katika ufahamu wa noti hizi tumeona ni vyematukayajibu kupitia kwenu.

2. Maswali yaliyopokelewa au kuandikwa katika vyombo vya habariyameonekana kutaka kutoa uelewa zaidi katika maeneo yafuatayo:

2.1 Noti mpya zikisuguliwa kwenye karatasi nyeupe zinaacha rangi nakwamba zikilowa zinatoa rangi. Je hali hii haitokani na uduni wa notihizi mpya?

Hali ya kuacha rangi noti zinaposuguliwa kwenye karatasi nyeupe ni yakawaida kwa noti zote zilizochapishwa kwa teknolojia maaluminayojulikana kwa kitaalamu kama “Intaglio Printing”. Aina hii yauchapishaji (Intaglio Printing) inazifanya noti kuwa na hali yamparuzo zinapopapaswa. Teknolojia hiyo imetumika ili kuimarisha kingoza noti kwa lengo la kupunguza uwezekano wa kuchanika na kuchakaaharaka. Miparuzo hii huacha rangi noti inaposuguliwa kwa nguvu kwenyekaratasi nyeupe kitendo ambacho kinathibitisha kuwa noti hiyo nihalali. Hali hii pia ni moja alama ya usalama (security feature)inayothibitisha kuwa noti siyo ya bandia.

Aidha, noti halali hazichuji zikilowekwa kwenye maji kama inavyodaiwakwa kuwa wino uliotumika hauyeyuki katika maji. Vilevile noti hizizimetengenezwa kwa teknolojia ya kuwekewa kinga dhidi ya uchafu
inayojulikana kitaalamu kama “Anti Soiling Treatment” ili kupunguzauwezekano wa kunasa uchafu inapokuwa katika mzunguko.Teknolojia hizi mbili zinalenga kuongeza uhai wa noti katika mzunguko.

2.2 Je noti za zamani bado ni halali na zinaendelea kutumika?

Noti za zamani bado ni noti halali na zitaendelea kuwa katika mzungukopamoja na zile mpya mpaka zitakapotoweka kwenye mzunguko kwa sababu zauchakavu wake. Kwa hiyo wananchi wanashauriwa kuendelea kutumia notiza toleo la zamani bila wasiwasi wowote.

2.3 Kwa kuwa noti mpya ni ndogo kuliko za zamani kwa umbo je thamani ya noti hizo siyo pungufu kulizo zile za toleo lililotangulia?

Thamani ya noti ni ile iliyoonyeshwa kwa tarakimu zilizoandikwa kwenye noti yenyewe bila kujali ukubwa wake. Kwa hiyo thamani ya noti za zamani na za sasa haitofautiani.

2.4 Kwa kuwa kumekuwa na matatizo ya upatikanaji wa noti mpya, je Benki Kuu ina mipango gani kuhakikisha noti mpya zinapatikana nchi nzima?

Benki Kuu huingiza noti mpya katika mzunguko kwa kupitia benki za biashara. Benki Kuu inaendelea kutoa noti hizo mpya kupitia benki hizo lakini kwa kuwa mtandao wa baadhi ya matawi ya benki hizo ni mpana
imechukua muda mrefu kwa baadhi ya maeneo kufikiwa na noti hizo. Hata hivyo kwa kuwa biashara nchini haina mipaka, noti hizo zitaendelea kusambaa nchini kote kupitia mzunguko wa kibiashara na kuongezeka siku
baada ya siku.

2.5 Je noti halali zinatofauti gani na noti bandia?

Ili kuhakiki uhalali wa noti tunawashauri wananchi kuzichunguza kwa makini noti kwa kutumia alama za usalama kama zilivyoainishwa kwenye matangazo na vipeperushi vilivyotolewa na Benki Kuu ama kuwasiliana na ofisi zetu kwa ufafanuzi zaidi pale mtu anapokuwa na mashaka na noti hizi.

2.6 Je Benki kuu ina mikakati gani ya kuelimisha jamii na hasa
vijijini kuhusu toleo jipya la noti?

Mtakumbuka baada ya uzinduzi wa noti mpya tarehe 17 Desemba 2010nilisema noti hizi zitaanza kuingizwa katika mzunguko Mwezi Januari 2011. Hii ililenga kutoa kipindi cha kutoa elimu kwa jamii kupitia
vyombo vya habari kuhusu toleo jipya kabla ya kuliingiza katika mzunguko. Aidha Benki Kuu ina mikakati endelevu ya kufikisha elimu ya “tambua noti zako” kwa wananchi wote kupitia matangazo, semina,
ushiriki katika mikusanyiko mikubwa kama Sabasaba na nanenane na kwenye masoko pamoja na minada mikubwa ya mifugo. Tovuti ya benki kuu Bank of Tanzania (BOT): Home Page : Benki Kuu ya Tanzania vilevile imetoa maelezo mazuri kuhusu kutambua alama muhimu katika noti.

2.7 Kwa kuwa Benki Kuu inabadilibadili fedha kila baada ya miaka mitano hadi saba. Je ni kwa nini isiwe na toleo la kudumu kama ilivyo kwa fedha ya Uingereza au ya Marekani?

Kubadili noti husababishwa na maendeleo ya teknolojia ya uchapaji wa noti katika kuongeza uhai wa noti katika mzunguko na kuweka alama bora zaidi za usalama ambazo ni ngumu kuzighushi. Aidha sio kweli kwamba Uingereza na Marekani hazijabadili noti zake. Kuna mabadiliko makubwa
na mengi tu yaliyopita na yanayotarajiwa kwa noti za nchi hizi.

2.8 Kwa nini Benki Kuu haikutoa noti kubwa zaidi ya 10,000 ilikurahisha malipo katika biashara?

Benki Kuu haikuona haja ya kutoa noti yenye thamani kubwa zaidi kwa sasa kwani malipo makubwa yanahimizwa kufanywa kupitia njia nyingine za kibenki. Noti ya Shilingi 10,000 bado inakidhi mahitaji ya malipo ya kawaida katika biashara kwa sasa.

Ni matumaini yetu kwamba ufafanuzi huu utaondoa wasiwasi uliokuwepo na kujenga imani kuhusu noti zetu mpya. Na Benki Kuu na matawi yake iko tayari kutoa ufafanuzi zaidi kuhusu noti zetu mpya pindiunapohitajika.

Asanteni sana

Prof Benno Ndulu
Gavana
Benki kuu ya Tanzania

3 Februari 2011

Leave a Reply