VIJANA wanaomaliza vyuo vikuu vya Zanzibar wataanza kunufaika na utaratibu wa kupatiwa mafunzo maalumu ya biashara pamoja ufundi yatakayowawezesha kufungua miradi kujiajiri na kuwaajiri vijana wengine na kukuza hali zao za maisha.
Utaratibu huo unatarajiwa kutekelezwa kufuatia mazungumzo yaliyofanyika kati ya ujumbe wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar unaoongozwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad na Idara ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (IT&C) ya Andhara Pradesh yaliyofanyika Hoteli ya Grand Kakatiya mjini Hyderabad.
Mbali na hatua hiyo Serikali ya Andhra Pradesh imemwomba Balozi wa Tanzania nchini India, John Kijazi kuandaa utaratibu utakaowezesha Zanzibar kunufaika na makubaliano yaliyofikiwa katika ziara ya Makamu wa Kwanza wa Rais kukuza mashirikiano katika nyanja za kiuchumi, biashara, kilimo na elimu kwa faida ya nchi mbili hizo.
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa Serikali ya Andhra Pradesh, Pannola Lakshmaiah alisema utaratibu huo unapaswa kuandaliwa mikakati ya ya utekelezaji mapema ili Serikali mbili hizo hasa Zanzibar iweze kunufaika mapema na kuchangia harakati zake za kuinua hali yake ya kiuchumi.
Alisema Jimbo la Andhra Pradesh limepata heshima kubwa duniani kote kwa Teknolojia ya Mawasiliano na Habari (IT), ambapo pia katika eneo hilo kunapatikana mji maalum wa Teknolojia ya Mawasiliano (Hyderabad Technology City) unaotoa mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa eneo hilo na India kwa ujumla.
“Jambo muhimu tutiliane saini makubaliano ya mashirikiano leo hii jioni (jana) na kitakachofuata Balozi aandae utaratibu wa utekelezaji kwa vile hakuna muda wa kusubiri, teknolojia ya habari na mawasiliano hivi sasa ni ajira ni uchumi ni kila kitu”, alisema Waziri wa IT& C.
Katika mazungumzo hayo, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Ramadhan Abdallah Shaaban alisema bado Zanzibar iko nyuma katika elimu ya IT&C, licha ya juhudi kubwa zinazoendelea kuchukulia kuinua elimu hiyo, ukiwamo mpango mahsusi ulioanzishwa na Serikali ya Zanzibar uitwao E -government.
Waziri Shaaban alisema kuna haja Serikali ya Andhra Pradesh ambapo inafanana kiutawala na Zanzibar ndani ya Jamhuri ya Muungano kushirikiana kuandaa utaratibu wa masomo kwa vijana wa Zanzibar.
Alisema kazi hiyo inaweza kufanikishwa chini ya utaratibu wa kupeleka wataalamu Zanzibar kutoa mafunzo hayo au vijana wa Zanzibar kwenda India kujifunza na baadaye kurudi nyumbani kutumia ujuzi huo kwa maslahi yao na nchi.
Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko, Nassor Ahmed Mazrui alisema Zanzibar kuna vijana wengi wanaomaliza vyuo vikuu na kukaa muda mrefu bila ya kupata ajira na utaratibu huo utawasaidia kupunguza tatizo la uhaba wa ajira na kuwapa mafunzo ya kazi maalumu za amali zitakazosaidia kuimarisha maendeleo.
Waziri Mazrui alisema maeneo mengine ambayo Zanzibar inaweza kunufaika katika mashirikiano na Andhra Pradesh ni usindikaji wa bidhaa kama vile za matunda, viungo pamoja na mazao ya baharini.
Waziri Mazrui alisema Zanzibar imejaaliwa kuna rasilimali za viungo kama vile karafuu zao ambao linasafirishwa kwa wingi kwenda India na kama kutakuwa na utaratibu wa kufanyiwa ‘branding’ na baadaye kusafirishwa litaweza kupata soko kubwa zaidi ya sasa katika soko la dunia.
Yaap hapo mambo yatakuwa ni mazuri kwa vijana kwani elimu wanayo na ujuzi wanawo. Kazi ni kwenu tuu vijana.Nawatakia mafanikio mema muwe kama vijana wa http://www.jigambe.com, hebu tembelea then utajua nini wamekifanya mara baada ya kumaliza chuo.