Wanawake wawili wafanyabiashara wa nchini wametiwa mikononi mwa walinzi wa raia na mali zao mjini Morogoro wakidaiwa kukwapua kitita cha fedha kiasi cha Shilingi milioni 4.4 za kitanzania.
Taarifa za kipolisi kutoka Moropgoro zinapasha kuwa wanawake hao walikwiba fedha hizo mali ya Jackson Edson mkazi wa mjini Morogoro alipo fika kuweka fedha benki ya CRDB , Morogoro.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Adolfina Chialo , aalitanabaisha hayo na kuwataja watuhumiwa hao kuwa ni Iren Kharim na Jane Ndunilo kutoka jiji laNairobi, Kenya.
Chialo alitoa taarifa hizo kuwa tukio lilitendeka siku ya Aprili 4 mishale ya saa 4 asubuhi CRDB tawi la Morogoro katika mitaa ya Masika na Ngoto.
Wanawake hao majasiri wanadaiwa kufanya wizi huo kwa njia ya aina yake ambayo watu wote tunaoingia benki yatupasa kuwa makini nayo ya kuombwa msaada wa kufanyiwa kitu au kuelekezwa.
“Watuhumiwa hao waliomba msaada kutoka kwa mfanyabiashara huyo wa kuwajazia fomu lakini na wakati wakipatiwa msaada huo walivuta bahasha yenye fedha hizo iliyokuwa mezani na kuondoka,”alisema Kamanda wa Polisi.
kamanda wa Polisi anasema ni Polisi jamii tu ndio iliyo okoa bulungutu hilo la fedha baada ya watu waliopo ndani ya Benki kuwataiti wakisaidiana na askari wa benki.
Baade watuhumiwa walipelekwa katika kituo cha Polisi cha kati kilichopo mjini hapa kwa mahojiano zaidi na pindi uchunguzi wa Kipolisi utakapo kamilika watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani kujibu mashtaka yao.
Categories: