Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

Sheikh Mkuu Wa Misri Dr Muhammad Sayyed Tantawyi Afariki Dunia


Sheikh Mkuu wa Tanzania Sheikh I ssa Shaabani Simba (shoto) akiwa katika picha ya pamoja na Sheikh Mkuu wa Misri (Sheikhul-Azhar v-GRAND SHEIKH OF AL-AZHAR - Pr,) Dr Muhammad Sayyed Tantawyi katika Ofisi zake za Masheikhatul-Azhar zilizopo mji wa Darassa mwezi jana.
Habari zinasema Dr. Tantawyi amefariki dunia huko Misri.
Sheikh Mkuu wa Tanzania alikuwa nchini Misri kuhudhuria Mkutano Mkuu wa 22 (The 22nd General Conference. Under the Title The Objectives of Shariah(Islamic Law)And Issues of the Contemporary Age.



Marehemu amefariki leo saa 12:00 asubuhi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mjini Riadh Nchini Saudi Arabia akijiaanda kwa safari ya kurudi Nchini Misri.
Sheikh alikuwa Nchini Saudia Arabia Kuhudhulia Hafla ya ugawaji wa tunzo ya Mfalme Faisal iliyokuwa ikigaiwa kwa baadhi ya viongozi kutoka Nchi mbalimbali akiwemo Waziri Mkuu wa Uturuki.

Sababu za kifo chake ni Presha(Mshtuko wa Moyo) uliomtokea Ghafla akiwa kwenye ngazi ya Ndege,Taarifa zinasema hali hiyo imetokana na Uchovu aliopata kutokana na Shughuli hiyo ya jana.      


source:michuzi                                               




[ Read More ]

MAALIM SEIF YU HAI NA ANAENDELEA VIZURI

Uvumi ulioenea nchini ya kwamba Maalim Seif emefariki dunia unaonekana hauna ukweli wowote baada ya kuthibitika kwamba Maalim anaendela vizuri katika Hospitali ya Hindu Mandal.
Uvumi huo uliokua ukisambazwa leo hii kwa njia ya simu (SMS)unaeleza kua Maalim Seif amefariki dunia leo katika Hospitali ya Hindu Mandal ambapo alikua amelazwa tokea jana baada ya kuanguka jana Uwanja wa Ndege Jijini Dar-es-salaam alipokua akisubiri ndege kuelekea nchini Oman.
Maalim alikua anasumbuliwa na tatizo la Presha pamoja sukari, lakini kwa sasa anaendelea vizuri na anatarajia kuruhsiwa kwenda nyumbani hii leo.
InshaaAllah Mungu ampe afya njema......Amiin
[ Read More ]

UMEME ZANZIBAR KUREJEA JUMANNE IJAYO

Huduma ya umeme visiwani Zanzibar inatarajiwa kurudi Jumanne ijayo baada ya kukamilika kazi za utengenezaji wa kituo cha kupokea umeme kilichopo Fumba, Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja.

Kaimu Meneja wa Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO), Hassan Ali Mbarouk, aliwaambia waandishi wa habari waliotembelea katika kituo chenye kufanyiwa matengenezo cha Fumba kwamba ikiwa kazi ya kurejesha huduma hiyo itafanyika kama ilivyopangwa basi huduma hiyo itarejea siku hiyo.

Alisema kazi hiyo iliyobakia ni kuunganisha waya za umeme kutoka nchi kavu na baharini na kazi hiyo ya kuunganishwa kwa waya kutoka katika vituo vya Fumba hadi Ras Kiromoni Tanzania Bara itachukua muda wa siku tatu.

Akitaja hatua zitakazochukuliwa za kurejesha huduma hiyo, Kaimu Meneja huyo alisema hadi Jumapili ijayo kazi ya matengenezo itakuwa imemalizika na matarajio Machi 8 kutafanyika vipimo vya majaribio na Machi 9 ndiyo huduma hiyo inatarajiwa kuwashwa.

Aliwaeleza waandishi wa habari kuwa kuchelewa kwa huduma hiyo kumesababishwa na mafuta yaliyokuwemo ndani ya waya zinazoleta umeme kutokuwa safi na kulazimika kusafishwa kwa muda wa siku tatu.

Wakazi wa visiwa hivyo wamekosa huduma ya umeme tangu Desemba mwaka jana, baada ya kutokea hitilafu katika kituo cha kupokea umeme huo kutoka Ras Kiromoni hadi Funmba mjini Unguja.
[ Read More ]

300 dead in massive quake in Chile, search on for survivors.


SANTIAGO: Rescue teams hunted for survivors on Sunday after one of the largest earthquakes on record killed at least 300 people in Chile and sent giant waves roaring across the Pacific Ocean.

In an address to the nation on Saturday, President Michelle Bachelet said two million Chileans had been affected but, after touring the worst-hit areas by plane, she found it hard to spell out the magnitude of the disaster.

In Pics: Massive quake in Chile

"The power of nature has again struck our country," Bachelet said, declaring six of Chile's 15 regions "catastrophe zones" in the aftermath of the 8.8-magnitude quake.

Highways in the South American nation of 16 million were sliced to pieces, bridges imploded and buildings collapsed as the earthquake struck at pre-dawn hours Saturday some 325 kilometers (200 miles) southwest of the capital Santiago.

"This is a catastrophe of immense proportions, so it will be very difficult to give precise figures," Interior Minister Edmundo Perez Yoma said. Officials later said at least 300 people had been killed.

Waves well over two meters (seven feet) high crashed into the Chilean coast after the quake struck at 3:34 am (0634 GMT) and tore out into the Pacific, killing at least five people in the remote Robinson Crusoe islands.

In the Chilean port of Talcahuano, trawlers were sent shooting inland to the town square where they lay oddly marooned next to abandoned cars.

About 50 countries and territories along an arc stretching from New Zealand to Japan braced for giant waves, five years after the Indian Ocean tsunami disaster that killed more than 220,000 people.

More than 70,000 people fled vulnerable coastal areas of Japan Sunday as a tsunami slammed into the country's long Pacific coastline.

"Please do not approach the coast at any cost," Prime Minister Yukio Hatoyama said in nationally televised comments as Japan, one of the world's most quake-prone nations, went on its first major tsunami alert in 15 years.

The first tsunami wave, 30 centimetres (one foot) high, hit Nemuro on the northern island of Hokkaido in the early afternoon, the Meteorological Agency said.

The massive quake plunged much of Santiago into darkness, snapping power lines, severing communications. The international airport was closed after sustaining significant damage to the terminal.

Many Chileans were still in nightclubs partying at the start of the weekend when the quake struck before dawn, ripping up roads, bringing roofs crashing down and toppling power lines.

"It was the worst experience of my life," said 22-year-old Sebastian, standing outside his house in eastern Santiago.

"Friends who were at clubs said it was pandemonium," said Santiago resident Maren Andrea Jimenez, an American expert working for the United Nations. "It was scary! Plaster began falling from the ceiling."

President Barack Obama said the United States "stands ready to assist in the rescue and recovery efforts, and we have resources that are positioned to deploy should the Chilean government ask for our help."

"Early indications are that hundreds of lives have been lost in Chile and damage is severe. On behalf of the American people, Michelle and I send our deepest condolences to the Chilean people," he said at the White House.

The total value of economic damage caused by the quake is likely to range between 15 billion and 30 billion dollars, a US risk modeling firm predicted.

Despite officials saying up to 1.5 million homes could be affected, Chile's Foreign Minister Mariano Fernandez asked countries that had offered aid to hold off until local authorities could assess the emergency needs.

Chile does not want "aid from anywhere to be a distraction" from disaster relief, Fernandez said, adding: "Any aid that arrives without having been determined to be needed really helps very little."

The European Union said it would provide three million euros (four million dollars) in immediate assistance. Unlike Haiti, struck by a devastating earthquake last month, Chile is one of Latin America's wealthiest countries.

The US Geological Survey said it had recorded more than 51 aftershocks ranging from 4.9 to 6.9 since the quake.

Earthquake-prone Chile lies along the Pacific rim of fire and is regularly rocked by quakes, but damage is often limited as they mostly hit in remote desert regions.

It was the second major earthquake to hit the Western hemisphere in seven weeks after more than 200,000 people were killed in Haiti last month by a 7.0-magnitude quake.

The epicentre was just a few hundred miles north of the biggest earthquake on record, a 9.5-magnitude monster in May 1960 that killed between 2,200 and 5,700 people and triggered a huge tsunami that reached as far as eastern New Zealand.
[ Read More ]

Joti wa ze comedy alazwa moi....


[t.JPG]
Msanii maarufu wa kundi la vichekesho la Orijino Komedi,Lukac Mhavile a.k.a Joti (pichani) anahofiwa kuvunjika shingo,baada ya kupata ajali alipokuwa akirekodi kipindi pamoja na wenzake eneo la daraja la Salender,jijini Dar.




Joti aligongwa na lori aina ya Scania malai ya Ubalaozi wa Ubelgiji nchini,saa 5:30 jana asubuhi.Amelazwa Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) kwa matibabu,akiwa amefungwa kifaa maalum cha kuzuia shingo kukunja na kugeuka.


Akizungumzia tukio hilo,Kamanda wa Polisi mkoa wa Kinondoni,Sebastian Masinde,alisema ajali hiyo ilitokea wakati msanii huyo akiwa na wenzake wakiigiza tukio lililodaiwa kutokea eneo hilo la Mwanamke kuoata Manyoya baada ya kumpa ombaomba pesa.


Alisema walipokuwa wakiigiza wakiwemo pia wasanii wenzake Masanja na Mpoki,ombaomba waliokuwa karibu walichachamaa na kuwazuia wasiigize ambapo katika kufanya hivyo waliwavamia na Joti na wenzake wakalazimika kukimbia.


"walipokuwa wakikimbia ndipo alipogongwa na gari,wamekasirika kwa sababu sasa mwenye kila gari lake anayepita pale anafunga vioo,hivyo hawakupenda Komedi waigize tukio hilo na kuanza kuwafukuza.
kamanada Masinde alisema kuwa baada ya tukio hilo, Majeruhi walipelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako amelazwa MOI,na dereva wa Lori hilo anashikiliwa na polisi pamoja na gari lililosababisha ajali hiyo.
source michuzi.
[ Read More ]

PRESIDENT JK CONFERRED PHD IN INTERNATIONAL RELATION IN TURKEY!

President Jakaya Mrisho Kikwete prepares to deliver his acceptance speech shortly after he was conferred with Honorary Doctorate Degree in International Relations yesterday at Fatih University, in Instabul, Turkey Friday evening. Photo by Freddy Maro.


The Rector of Fatih University in Instabul, Turkey, Professor Shariff Ali confer upon President Jakaya Mrisho Kikwete a honorary Doctorate Degree (Honoris Causa) in International Relations during a colourful ceremony held at Fatih Univesity in Instabul Turkey Friday evening.Photo by Freddy Maro.
[ Read More ]

JK Ziarani Uturuki






Rais wa Uturuki Abdullah Gul na mkewe wakiwakaribisha ikulu ya jıjını Ankara JK Mama Salma leo asubuhi

JK na mwenyeji wake Raıs wa Uturuki Abdukkah Gul wakıkagua gwaride la heshima muda mfupi baada ya Rais Kıkwete kuwasili katika ikulu ya nchı hıyo iliyopo jijini Ankara leo asubuhi.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo 18 Feb, 10 anaanza ziara ya siku tatu nchini Uturuki kwa makaribisho rasmi ambapo Rais wa Uturuki Mheshimiwa Abdullah Gul atamkaribisha Rais Kikwete katika kasri ya nchi hiyo.

Mara baada ya makaribisho hayo, viongozi hao wawili watafanya mazungumzo rasmi ya kiserikali na kushuhudia utiaji saini kwa mikataba mitano kati ya nchi mbili hizi shughuli ambazo zitafanywa na mawaziri.


Mchana wa leo, (18.2.10) Rais na ujumbe wake utakutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Uturuki, Mheshimiwa Recep Tayyid Erdogan kabla ya kukutana na kufanya mazungumzo na spika wa Bunge la Uturuki Mheshimiwa Mehmet Ali Sahin.

Rais Kikwete pia atakutana na kufanya mazungumzo na Umoja wa Wafanyabiashara wa Uturuki na baadaye kukutana na mabalozi wa Nchi za Afrika waliopo Uturuki na baadaye jioni hii Rais Kiwete na ujumbe wake watahudhuria dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa kwa heshima yake na mwenyeji wake.



[ Read More ]

Ajiua baada ya kumchinja mkewe kwa wivu

MKAZI wa Kitefu wilayani Arumeru mkoani hapa, George Lukas (27), anatuhumiwa kumuua mkewe kwa kumchinja na kisu na kisha kuacha ujumbe mzito, kabla naye kujiua kwa sumu kutokana na wivu wa mapenzi.

Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Basilio Matei alisema tukio la kuuawa kwa mke huyo, Asumin Hussein (36), limetokea juzi saa 12 jioni katika Kitongoji cha Kitefu, Maroroni wilayani Arumeru.

Akielezea chanzo cha tukio hilo, Kamanda Matei alisema wanandoa hao wamekuwa na ugomvi wa mara kwa mara, huku mume akimtuhumu mkewe kuwa sio mwaminifu kwani amekuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamume mwingine, na kwamba amewahi kutoa ujauzito wake ili aolewe na mwanamume mwingine.

Alisema siku ya tukio, mwanamume huyo alifika nyumbani na kuanza kudai ujauzito wake kutokana na majibizano, kulitokea ugomvi wa kutoelewana, na kusababisha mume kuchukua kisu na kumchinja mkewe, na kusababisha kifo cha mwanamke huyo.

Baada ya tukio hilo, Kamanda alisema Lukas alichukua karatasi na kuandika ujumbe kabla ya kujiua kwa sumu, ambayo haikufahamika.

Polisi baada ya kupata taarifa, walifika eneo la tukio na kukuta karatasi yenye ujumbe uliosomeka kuwa “nimeamua kumuua mke wangu kwa sababu ametoa mimba yangu na ana uhusiano na mwanamume mwingine.’’

Katika tukio jingine, Lembrisi Taiko (25), mkazi wa Sanawari Moivo katika Manispaa ya Arusha, ameuawa kwa kukatwakatwa na panga na wananchi baada ya kujeruhi kwa panga.

Kamanda Matei alisema tukio hilo limetokea juzi saa 4:30 usiku baada ya Taiko kukutwa akimshambulia kwa panga, Saimoni Lizer (45) na kumjeruhi vibaya kwa sababu ambazo hazikufahamika.

Miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru kwa uchunguzi zaidi.
[ Read More ]

Mtoto aliyenusurika mauaji Musoma asimulia alivyookoka

MTOTO wa miaka minne aliyenusurika katika mauaji ya watu 17 wa familia tatu za ukoo mmoja katika eneo la Buhare, nje ya Manispaa ya Musoma, mkoani Mare, ameeleza namna alivyojiokoa dhidi ya wauaji kwa kuingia uvunguni.

Kituo cha Redio Clouds jana kilirusha sauti ya mtoto huyo (jina lake limehifadhiwa) akijieleza kwamba alifanikiwa kuingia uvunguni mwa kitanda mara baada ya wahalifu hao kuanza kuwakata kwa mapanga ndugu zake.

Mtoto huyo ambaye kwa mujibu wa mwandishi wa kituo hicho alionekana kisaikolojia kuathirika kutokana na tukio hilo, alisikika akisema hakuweza kuwatambua wavamizi kutokana na jinsi walivyojifunika makoti meusi.

Akielezea walivyoonekana, mtoto huyo ambaye kwa mujibu wa mahojiano redioni alikuwa amefuatana na watu wazima, akiwamo kiongozi wa ukoo, alidai kuwa aliwaona watu wanne waliokuwa na makoti meusi na viatu alivyovitaja kwamba vinafanana na vya kuchezea mpira.

Alisema aliwasikia wakiwataka wanafamilia hao kutoa fedha na kuwaambia wasipotoa, watawaua.

Mkuu wa Mkoa wa Mara, Enos Mfuru, wakati wa maziko ya miili ya watu waliouawa kwenye tukio hilo ambalo kati ya marehemu 17, kati yao, 11 ni watoto wenye umri wa kati ya miezi 11 na miaka 13 wakiwamo wazazi wake, aliahidi kwamba Serikali itamhudumia mtoto huyo.

Mfuru alisema mtoto huyo atasomeshwa na Serikali. Naye Mbunge wa Musoma Vijijini, Vedastus Mathayo (CCM), aliahidi kumsaidia.

Mfuru alisema Serikali itahakikisha inagharimia matibabu kwa majeruhi wa tukio hilo waliolazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Mara mjini Musoma. Maiti hao 17 walizikwa juzi katika tukio lililohudhuriwa na mamia ya watu.

Taarifa zinasema mauaji hayo yalifanyika kutokana na kinachosadikiwa kuwa ni kulipiza kisasi. Polisi katika taarifa yake ya juzi, ilisema watu watano walikuwa wamekamatwa wakihojiwa juu ya tukio hilo.

Miili 16 ilizikwa katika kijiji cha Mgaranjabo nje kidogo ya Musoma na aliyekuwa mwanafunzi wa sekondari ya Mkirira, Joseph Sofareti, alisafirishwa kwenda kijijini kwao Kome, Musoma Vijijini baada ya heshima za mwisho kutolewa.
[ Read More ]

Aanguka toka ghorofa ya tisa

FUNDI ujenzi aliyefahamika kwa jina moja la Ally, amekufa baada ya kuanguka kutoka ghorofa ya tisa wakasti akiwa katika shughuli za ujenzi katika ghorofa hiyo.

Fundi huyo alikuwa katika ya nyumba ya Shubas Patel iliyokuwa na ghorofa 12 na alianguka wakati akiwa kazini.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile, amesema ajali hiyo ilitokea jana, saa 10 jioni, Mtaa wa Sewa na Zanaki Ilala jijini Dar es Salaam.

Alisema fundi huyo, akiwa na wenzake wakiendelea na kazi kwenye ghorofa ya tisa, ghafla alidondoka hadi ghorofa ya tatu ambapo alinasa kwenye kizuizi cha mabati.

Alisema alipata majeraha kwenye paji la uso pamoja na kuvunjika mkono wake wa kushoto.

Hata hivyo wenzake walimkimbiza Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu na alikufa muda mfupi baada ya kufikishwa hospitalini hapo.


SOURCE;NIFAHAMISHE.COM
[ Read More ]