BAADHI ya watumiaji wa simu za viganjani zenye televisheni ni miongoni mwa watu watakaoathirika na uzimaji wa mitambo ya utangazaji wa televisheni ya mfumo wa analojia.
Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, wakati Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasialiano nchini (TCRA), akitoa taarifa kuhusu uzimaji wa mitambo hiyo ya analoji kwenda dijitali, kwa mkoa wa Dar es Salaam, Injinia Endrew Kisaka alisema hali hiyo inatokana na simu hizo kuunganishwa na mfumo huo.
Alisema simu hizo zitakosa huduma hiyo ya matangazo hadi pale kampuni hizo za simu kwa shirikiana na malaka hiyo kuzindua mfumo utakaokwenda sambamba na dijitali hivi karibuni.
Injinia Kisaka, alisema uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika haraka ili kuepusha usumbufu unaoweza kujitokeza kwa watumiaji wa simu hizo.
Akifafanua zaidi kuhusu changamoto kuhusu ving’amuzi, alisema endapo utatokea usumbufu wananchi wasisite kurudi sehemu waliko nunua king’muzi hicho kwa maelezo zaidi.
“Unajua kuna baadhi ya maeneo kama vile yenye majengo marefu na mabonde ambapo maeneo hayo hukosekana ‘signal’ sasa mkiona hivyo rudini kwa wauzaji wenu wawape ushauri wa kitaalamu utakaosaidia kupata matangazo hayo kwa ubora”alisema Kisaka.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka hiyo, Prof. John Nkoma alisema serikali imejitahidi kuondoa kodi katika kuingiza ving’amuzi ambapo imesaidia kupunguza bei na kuwa sh 39,000 ambayo anaamini kila Mtanzania atamudu kukipata.
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imekuwa ikitoa elimu kwaumma kwa kiwango chakuridhisha,hivyo uhamaji hautakuwa na usumbufu kwa watumiaji wa huduma za utangazaji.
Pamoja na hayo, alieleza mabadiliko hayo hayatahusu
utangazaji kwa satelaiti, waya (cable) na redio.
NA FULLSHANGWEBLOG.COM DAR ES SALAAM