Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

MABADILIKO.


Mabadiliko ya email ya kuwasiliana na blog hii. kutoka fromcoast@hotmail.com kwenda rea_mwinyi@yahoo.co.uk


ahsante endelea kutembelea blog hii..
[ Read More ]

FLAVIANNA MATATA ON GLASS MAGAZINE!


Young and beautiful, humble but fierce it's Flavy on Glass Magazine looking sexy as usually...
[ Read More ]

FACEBOOK WILL END ON MARCH 15th!


PALO ALTO, CA –Mark Zuckerberg announced that Facebook will be shut down in March.
 Managing the site has become too stressful.
Facebook has gotten out of control,” said Zuckerberg in a press conference
 outside his Palo Alto office, “and the stress of managing this company has
 ruined my life. I need to put an end to all the madness.”
Zuckerberg went on to explain that starting March 15th, users will no 
longer be able to access their Facebook accounts.
“After March 15th the whole website shuts down,” said Avrat Humarthi,
 Vice President of Technical Affairs at Facebook. “So if you ever want to see 
your pictures again, I recommend you take them off the internet. You won’t be 
able to get them back once Facebook goes out of business.”
Zuckerberg said that the decision to shut down Facebook was difficult, 
but that he does not think people will be upset.
“I personally don’t think it’s a big deal,” he said in a private phone interview.
 “And to be honest, I think it’s for the better. Without Facebook, people will 
have to go outside and make real friends. That’s always a good thing.”
Some Facebook users were furious upon hearing the shocking news.
“What am I going to do without Facebook?” said Denise Bradshaw,
 a high school student from Indiana. “My life revolves around it.
 I’m on Facebook at least 10 hours a day. Now what am I going to do 
with all that free time?”
However, parents across the country have been experiencing a long
 anticipated sense of relief.
“I’m glad the Facebook nightmare is over,” said Jon Guttari, 
a single parent from Detroit. “Now my teenager’s face won’t be glued to a
 computer screen all day. Maybe I can even have a conversation with her.”
Those in the financial circuit are criticizing Zuckerberg for walking away 
from a multibillion dollar franchise. Facebook is currently ranked as one of the
 wealthiest businesses in the world, with economists estimating its value 
at around 7.9 billion.
But Zuckerberg remains unruffled by these accusations. He says he will 
stand by his decision to give Facebook the axe.
“I don’t care about the money,” said Zuckerberg. “I just want my old life back.”
The Facebook Corporation suggests that users remove all of their personal 
information from the website before March 15th. After that date, all photos, 
notes, links, and videos will be permanently erased.


[ Read More ]

MICHUANO YA MAPINDUZI CUP - BASKET BALL

MCHEZAJI wa timu ya Usolo Hafidh Mgeni akiwapita walizi wa timu ya Stone Town katika michezo ya fainali ya Kombe la Mapinduzi
 MCHEZAJI wa Timu ya Usolo Abubakari Buba akijaribu kumpita mchezaji wa yimu ya Stone Town Juma Mbai katika mashindanoiya Kombe la Mapinduzi yanayafanyika uwanja wa Basketi Maisara timu ya Stone Town imeibuka na Ushindi.
  WACHEZAJI wa Stone Town wakimsikiliza Mgeni Rasmin Mbunge wa Jimbo la  Kikwajuni Hamad Masauni akitowa nasaha zake kwa wachezaji wa mchezo huo
 WACHEZAJI wa timu ya Usolo wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mwenye suti Hamadi Masauni akizinduwa mashindano ya Kombe la Mapinduzi kutimiza miaka 47, uliofanyika kiwanja cha Maisara. 




<> MCHEZAJI wa timu ya Usolo Abubakari Buba mwenye mpira akimpita mchezaji wa timu ya Stone Town katika mchezo wa kuadhimisha miaka 47 ya Mapinduzi ya Zanzibar uliofanyika Uwanja wa Maisara.
<>
 
WACHEZAJI wa Timu ya Stone Town wakifahamishana jinsi ya kuwamiliki wapizani wao Timu ya Usolo katika mchezo wa maadhimisho ya miaka 47 ya Mapinduzi mchezo uliofanyika uwanja wa Basket Ball Maisara timu ya Stone Town imetoka na ushindi.
[ Read More ]

MAALIM SEIF AIOMBA KOREA KUWAJENGEA UWEZO VIJANA.

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, ameiomba serikali ya watu wa Korea Kusini, kuangalia uwezekano wa kuisaidia Zanzibar katika sekta za Elimu na Kilimo ili kuwajengea uwezo wa kiuchumi vijana.

Maalim Seif, alitoa ombi hilo huko Ofisini kwake Migombani alipokuwa na mazungumzo na Balozi wa Korea Kusini nchini, Kim Young Hoon, ambapo pamoja na mambo mengine walizungungumzia haja ya kukuza ushirikiano kati ya nchi mbili hizo.

Makamu huyo alisema Zanzibar ni miongoni mwa nchi zinazoendelea, inakabiliwa na changamoto nyingi za kimaendeleo, ikiwemo kuwajengea uwezo wa kielimu vijana wake ili waweze kujiajiri pamoja na kuimarisha sekta ya kilimo.

Alisema Serikali ya Zanzibar imeunda Wizara maalum ya Kazi, Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika, kwa lengo la kuwajengea mazingira bora vijana ili waweze kujiajiri kwa kufanya kazi za amali.

Aidha alisema msukumo zaidi unahitajika ili kuinua kiwango cha elimu, kuanzia ngazi za msingi hususan katika fani za kiufundi, hivyo alimuomba Balozi huyo kutoa fursa zaidi za masomo katika nyanja hiyo.

Maalim Seif alifahamisha vijana wa Zanzibar, wanakabiliwa na changamoto kubwa ya ushindani wa ajira katika soko la pamoja na Afrika Mashariki, ambapo vijana wa ukanda huo watakuwa na fursa ya kufanyakazi kutoka nchi yoyote mwanachama.

Aidha Maalim seif alimweleza Balozi huyo kuwa visiwa vya Zanzibar vinahodhi eneo dogo la ardhi, ambapo upatikanaji wa mazao umekuwa sio wa uhakika kwa vie unazingatia zaidi mvua, huku kukiwa na mabadiliko ya hali ya hewa kila mara.

Alimwomba Balozi huyo kuangalia uwezekano wa nchi yake kusaidia uimarishaji wa miundo mbinu ya kilimo cha umwagiliaji pamoja na pembejeo ikiwemo ‘Power tiller’, sambamba na kutoa fursa zaidi za mafunzo kwa wataalamu wazalendo ili hatimae waweze kueneza taaluma hiyo kwa wakulima.

Katika hatua nyingine Malim Seif alimuomba Balozi huyo kuangalia uwezekano wa Shirika la Ndege la nchi yake kufanya safari za moja kwa moja hadi Zanzibar, ikiwa ni njia moja wapo ya kukuza utalii.

Alisema Serikali ya Zanzibar inaendelea na jitihada za kuimarisha miundo mbinu ya mawasiliano ikiwemo uimarishaji wa kiwanja chake cha Ndege kwa lengo la kukuza sekta hiyo muhimu inayochangia asilimia kubwa ya pato la taifa.

Nae Balozi Kim, alimuhakikishia Makamu wa Kwanza wa Rais, kuwa Korea itaendeleza ushirikiano wake wa muda mrefu na Zanzibar kwa kuongeza fursa za masomo kwa Wazanzibari ili kuwajengea uwezo vijana pamoja na kutuma Wataalamu wa kujitolea kushirikiana na wazalendo katika miradi mbali mbali.

Alisema vijana wa Zanzibar wanaweza kufaidika zaidi kutokana na fursa za mafunzo kwa kutafuta taarifa sahihi kupitia mtandao wao wa  Koika.

Aidha aliiomba serikali kuangalia kwa karibu zaidi usalama wa wataalamu wake wa kujitolea pale wanapokuwa nchini katika shughuli za kazi katika maeneo ya vijijini.
[ Read More ]

MGAMBO!!!!???? HII NI HAKI KWELI???






Ukamataji 'wamachinga' katika baadhi ya maeneo Tanzania... aibu tupu
(Source: Mpoki Bukuku blog)

[ Read More ]

Mti Waangukia Magari Dar Leo



Mti unaoonesha umekula chumvi nyingi mchana huu umeangukia magari mawili yaliyopaki mtaa wa Jamhuri jijini Dar na kusababisha uharibifu mkubwa wa gari moja
wananchi wakipita karibu na ajali hiyo
Kioo cha mbele kimepata madhara, gari lingine limesevu kiasi
[ Read More ]

VYUO VYA AMALI MSINGI KUWAWEZESHA VIJANA- SAMIA

WAZIRI wa Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano, Samia Suluhu Hassan, amesema ujenzi wa vituo vya mafunzo ya amali nchini unalenga kuwasaidia na kuwajengea uwezo vijana.

Alisema vyuo hivyo ni msingi wa kuwawezesha vijana ili waweze kujiari na kuajiriwa jambo ambalo litawasaidia kuepukana na ugumu wa maisha.

Alisema hayo jana, wenye ufunguzi kituo cha Elimu ya Amali huko Chukwani, Wilaya ya Magharibi Unguja, ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya Mapinduzi Zanzibar yanayotimiza miaka 47.

Alisema kujenga kwa kituo hicho ni chachu ya maendeleo na kupunguza umasikini kwa wananchi, ambapo inakwenda sambamba na sera za Serikali ya kuwawezesha vijana kupia vituo hivyo kwa ajili ya kujiajiri wenyewe na kuajiriwa.

Alieleza kituo chiho kitatoa mafunzo ya kompyuta, lugha ya kiingereza na ufundi wa magari kwa kuanzia, ambapo alitoa wito kutangazwa zaidi ili vijana waweze kujiunga na kufaidika na matunda hayo.

Waziri Samia alizishukuru taasisi zilizotoa msaada wa ujenzi wa kituo hicho ikiwemo Ujerumani ambayo ilishirikiana na ‘Pamoja Zanzibar’, ambapo jumla ya Euro milioni 4.7 zilitumika katika kituo hicho ikiwemo vifaa vya kisasa vilivyofungwa.

Hata hivyo, aliwakumbusha wananchi wanakila sababu ya kusherekea Mapinduzi Matukufu 1964, ambayo ndio yaliyowakomboa wananchi na matunda yake yanaonekana.

Mapema Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Ramadhan Shaaban aliwapongeza wahisani hao kupitia Jumuiya ya Pamoja Zanzibar na mashirikiano makubwa baina ya Chuo cha Ufundi na Taasisi ya Sayansi na Teknolojia katika kufanikisha ujenzi huo, ambao unatokana na sera ya elimu ya kuwajengea uwezo vijana.

Nae Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Dk. Guido Herz aliishukuru Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kukubali kujengwa kwa kituo hicho ambacho kitasukuma mbele maendeleo ya kiuchumi na kupambana na umasikini

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa taasisi ya Sayansi na Teknolojia, ambao ndio walezi wa kituo hicho, Haji Abdulhamid alieleza Marehemu Mzee Abeid Amani Karume alianzisha Chuo cha Ufundi Mbweni kwa ajili ya kukuza maendeleo kupitia sayansi na teknolojia.

Alisema uwepo wa chuo hicho ni kuziendeleza fikra za kiongozi huyo aliyeasisi Mapinduzi ya Zanzibar miaka 47 iliyopita.
[ Read More ]

WAFANYAKAZI SKULI YA HIGH VIEW WAACHISHWA KAZI, WAKOSESHWA HAKI ZAO

JUMLA ya wafanyakazi wanne walioajiriwa kwa mkataba usio rasmi katika skuli ya HIGH VIEW, wameachishwa kazi na kukoseshwa haki zao zote ikiwemo mishahara ya miezi miwili.

Wakizungumza na Zanzibar Leo wafanyakazi hao walisema uongozi wa skuli hiyo umechukua hatua ya kuwafukuza kazi kwa vile walikuwa wanadai haki zao kisheria.

Aidha walifahamisha kuwa mnamo Disemba 2 mwezi uliopita, waliandikia barua kwa uongozi wa skuli hiyo na kudai kupatiwa mishahara, posho la likizo na kupatiwa mikataba rasmi pamoja na kupatiwa vitambulisho vya ZSSF.

Walimu hao walisema wameajiriwa katika skuli hiyo kwa kipindi cha zaidi ya miaka miwili na tokea kipindi hicho wamekuwa wakikatwa fedha zao mfuko wa hifadhi ya jamii, lakini wanashangazawa kuona hadi kufikia hii leo hawajapatiwa vitambulisho vyao.

“Tumekwenda hadi ZSSF kudai mafao yetu tumeambiwa kuwa hakuna fedha zilizowasilishwa na skuli hiyo hivyo hawawezi kupata haki yoyote”, alisema mmoja wa walimu hao.

Hata hivyo waliongeza kwa kusema kuwa skuli hiyo imekuwa ikiwajiri walimu kwa mikataba isiyo rasmi kwani haipitii katika kamisheni ya kazi na inaishia kwa wakuu wenyewe.

Aidha walieleza kua uongozi wa skuli hiyo umekuwa ukiwanyanyasa wafanyakazi wake na kutowapa fursa ya kujitetea.

Hata hivyo juhudi za kumpata miliki wa Skuli hiyo ili kuweza kujibu madai hayo zimeshindikana kutoka na kuwepo kwa nje ya ofisi na walimu waliyokuwepo Skulini hapo walishindwa kujibu madai hayo
[ Read More ]

SHAMSI VUAI NAHODHA - KUTOKA UULEDI HADI UNAHODHA


Kutoka Uuledi hadi Unahodha

Katika viongozi waliobahatika kuteuliwa katika nyadhifa kubwa na huku wakiwa na umri mdogo ni Mheshimiwa Shamsi Vuai Nahodha. Katika mwaka 2000 akiwa na umri wa miaka 38 tu, alikabidhiwa moja ya vyeo vya juu kabisa katika nchi ya Zanzibar kwa kuteuliwa na Rais wa wakati huo Aman Abeid Karume kuwa Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Waziri Kiongozi kikatiba ndiye mwenye dhamana ya kusimamia na kuiendesha serikali kwani yeye huwajibika kwa Rais pekee katika utendaji. Mawaziri wote huripoti kwake kwa kupokea maelekezo na maagizo ya utendaji.

Alipochaguliwa, wengi walishangazwa na uteuzi wa Rais na ninaweza kudiriki kutamka hata mwenyewe alijishangaa lakini aliyapokea maamuzi ya Rais kwa mikono miwili na kuingia kazini akiripoti katika Ofisi ya Waziri Kiongozi hapo Vuga.

Waliobahatika kukikalia cheo hiki kabla yake walikuwa ni wanasiasa waliobobea au wakongwe waliokuwa na uzoefu katika siasa kama Mheshimiwa Ramadhan Haji Faki (Februari 1983 – Februari 1984), Maalim Seif Sharif Hamad (Februari 1984 – januari 1988), Dk Omar Ali Juma (Januari 1988 - Oktoba 1995) Dk Mohammed Gharib Bilaal (Oktoba 2005 – Novemba 2000). Hivyo wengi walikuwa na hamu ya kuona utendaji wa Waziri Kiongozi mpya, kijana mgeni kwenye ulingo wa siasa na hasa wakati alipoingia katika Serikali kulikuwa na vugu vugu la msuguano wa vyama viwili vyenye nguvu CCM na CUF.

Mheshimiwa Nahodha alizaliwa 20/11/1962 na kupata elimu yake katika Skuli ya Msingi Kiongoni huko Makunduchi na kuendelea Sekondari katika Skuli ya Benbella na kisha kufanikiwa kujiunga katika Taasisi ya Kiswahili na Lugha za Kigeni. Ana Shahada ya kwanza aliyoipata Chuo Kikuu cha Daressalaam katika fani ya elimu na pia stashahada aliyoipata katika Chuo cha Diplomasia hapo Dar. Huko mitaani hujulikana kama mtoto wa mkulima na mkwezi alizaliwa shamba Makunduchi Wilaya ya Kusini, Mkoa wa Kusini Unguja.

Mheshimiwa Nahodha ni Kijana msomi wa Chuo Kikuu mwenye shahada, mtaalamu wa lugha, mwanadiplomasia, mwandishi, mwenye kipaji na mwerevu. Historia yake haioneshi kuwa na dhamana yoyote kubwa kabla ya kujitosa katika siasa na kugombania uwakilishi katika jimbo lake na kuibuka mshindi. Kilichobakia baada ya hapo ni historia kwani nyota yake ghafla ilipaa kutoka Ofisa Habari katika Wizara ya Habari mpaka Waziri kiongozi.

Ameweza pia kuweka historia kwamba yeye ndiye Waziri Kiongozi aliyeikwaa nafasi hii akiwa na umri mdogo aliyedumu muda mrefu kupita Mawaziri viongozi wote waliopita na pia kuwa Waziri Kiongozi wa mwisho katika Historia ya Zanzibar inayoendelea kwa kuwa cheo hiki tayari kimefutwa katika katiba ya Zanzibar.

Mheshimiwa Nahodha wakati wa uongozi wake kama Waziri Kiongozi, vijana walitarajia mengi kutoka kwake kama ambapo wazee walitarajia mageuzi ya kiutendaji. Sijui ni wepi waliofaidika na ndoto zao ila tu udiplomasia ulishika hatamu katika matendo yake na hata katika kuchukua maamuzi. Wakati wa maamuzi mazito hakuonekana msimamo wake na wala katika muda aliokuwapo madarakani hakuna jambo ambalo tunaweza kulitaja na kulinasibisha na jitihada zake binafsi kulitetea au kulisimamia jambo lililopelekea kunasibishwa na upole na yeye kudai si upole bali ni urasimu wa kimadaraka na aliwahi kunukuliwa akikataa masuala ya papo kwa papo katika Baraza la Wawakilishi akidai hawezi kuyazungumzia mpaka awasiliane na mkuu wake wa kazi Mheshimiwa Rais. Kauli hii ilitafsiriwa na wachambuzi wa Siasa kwamba anaonekana kama ni kondakta tu na si dereva, uledi tu ni si nahodha aliyepewa usukani kulipeleka jahazi.

Waliosomea udiplomasia huwa ni vigumu kuwajua misimamo yao kwani si rahisi kuweza kuwatambua wamesimamia wapi hasa kutokana na kauli zao kutokuwa na utashi wa kupendelea upande mmoja. Na ndivyo alivyokuwa Mheshimiwa Nahodha kwa muda wote wa utendaji wake.

Na hili pia halikumzuia kufikiria kuin’garisha zaidi nyota yake kwa kuingia katika kinyan’ganyiro cha urais 2010 ambapo jina lake lilivuka kisiwandui na kuweza kufika Dodoma lakini kwa bahati mbaya halikurudi huku akinasihiwa kwamba bado kijana ana muda zaidi wa kujijenga kisiasa kama ‘walivyoombwa’ kina Jakaya 1995 na Bilal 2005.

Aligombea tena uwakilishi katika jimbo lake na kushinda kwa kishindo huku wengi wakijiuliza mantiki na sababu ya mtu kama yeye aliyefikia cheo cha Uwaziri kiongozi kugombea kiti cha uwakilishi kwani ni kama kujishushia hadhi (demotion).

Kulipotangazwa viongozi wakuu wa serikali ya umoja wa kitaifa jina la Mheshimiwa Nahodha halikuwemo ila siku chache baadae tukasikia kuchaguliwa mbunge wa kuteuliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika Serikali ya Muungano.Na lilipotajwa baraza la mawaziri wa Muungano jina la Mhe Nahodha lilikuwamo kwa kuteuliwa Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi.

Wizara aliyokabidhiwa Nahodha ni moja katika wizara zinazodaia kuwa ni za Muungano na mojawapo katika wizara nyeti na yenye majukumu mazito ya kusimamia Polisi, Uhamiaji, Magereza, Zimamoto na kadhalika. Ni wizara ambayo tukiangalia Mawaziri kutoka Zanzibar waliobahatika kuisimamia huko nyuma walikabiliwa na changamoto nyingi kufikia wengine kujiuzulu kama alivyofanya Ali Hassan Mwinyi miaka ya sabini. Ali Ameir Mohammed anaikumbuka vizuri wizara hii ambayo ingawa inaitwa ya Muungano ila ndani yake kuna idara ambazo si za Muungano kama Magereza na Zimamoto.

Na hapa ndipo tunapotarajia kumuona the Real Captain –Nahodha wa kweli kama lilivyo jina lake na wengi watarajie vitendo pia kwani hana tena uuledi sasa tayari uNahodha umepata mwenyewe. Tena si Nahodha wa ngarawa, dau, mashua au jahazi sasa ni nahodha wa meli haswa iitwayo M.V mambo ya ndani.

Kama kujijenga zaidi kisiasa na kukomaa hii ni changamoto atakayokabiliana nayo katika kuisimamia Wizara yenye kashkash na mikeke ya kila aina na kila siku. Wizara isiyokupa muda wa kupumua wala kutafakari kwa kina na tayari ameshaanza kuyaona kwani migomo ya wanafunzi hiyo hapo, ikifuatiwa na migomo ya wafungwa na mahabusu inayonukia huku Jeshi la Polisi likiangazwa angazwa kwa ‘ukimya’ wake kwa mambo mengi na karibuni vitendo vya Polisi wenye vyeo vikubwa kuhamishwa vituo vya kazi kwa kupotea vidhibiti – madawa ya kulevya, migomo ya wanafunzi Chuo Kikuu cha Dodoma ambapo inadaiwa kuwa wanafunzi waliouawa baada ya Polisi kutumia nguvu myingi, maandamano ya CUF kudai katiba mpya. Haya yametokea katika kipindi cha miezi miwili tu tokea kuteuliwa kwake.

Mazingira ya kazi pia yanatofautiana na alipokuwa Waziri Kiongozi kwani kule visiwani hakukuwa na changamoto za waandishi, wasomi, viongozi wa makanisa,viongozi wa misikiti, jumuiya za kiislamu, wadadisi na magazeti lukuki yakiangalia kila kinachojiri hata kama kasindano kameanguka basi hufuatiliwa kulikoni. Visiwani mambo yalikuwa mswano kule hewalla bwana tu na likitokea basi pongezi ndizo zitakazotawala kuliko lawama.

Majuzi aliripotiwa kugomea chakula kilichoandaliwa katika mkutano na Wazimamoto wanaojitegemea ambao pia alikutana na matatizo kibao kutoka kwa wazima moto na lawama za wananchi kiwango kikubwa wanachotozwa kupata huduma hii ambao kimsingi hawana uwezo nayo.

Tokea kuteuliwa kwake tumesikia maagizo mengi yakitoka na mpaka sasa bado hatujapata kusikia au kuona udhaifu wake kiutendaji ila maagizo tu yatatosheleza kuwafanya watendaji wengine wachacharike? Tumesikia maagizo kwa wakimbizi, kwa wahamiaji, kwa vitambulisho vya taifa na mara nyingi huwa tunajiuliza vipi Mawaziri kutoka Zanzibar wanaweza kuyasimamia maslahi ya kizanzibari ndani ya Muungano kwa kuyapa kipaumbele na kuelekeza maendeleo nchini mwao.

Hivyo kwa wale wanaotaka kumuona na kumjua the real Captain, karibuni kwenye Mv Mambo ya Ndani tumuone Nahodha - si wa jina tu bali na vitendo pia.

Kama kweli Meli imepata mwenyewe au vyenginevyo time will tell.

Mdau
[ Read More ]