Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

RAISI KIKWETE ALIPO TEMBELEA ENEO LA TUKIO "GONGOLAMBOTO" LEO



Mungu ibariki Tanzania na watu wake.
Amri mkuu wa jeshi Raisi JK akizungumza na waandishi wa habari


 Waziri wa Ulinzi akizungumza na mkuu wa JWTZ na mnadhimu wa jeshi hilo
 Waathirika wakikimbia miji yaoo
 Hii ni nyumba moja wapo iliyo sambaratika kutokana na mabomu hayo
 Majeruhi wakipata huduma hospitali ya Temeke
Majeruhi akifikishwa hospitalini hapo Temeke huku akisaidiwa na wasamaria wema!!!

Mungu ibariki Tanzania na watu wake.
[ Read More ]

MILIPUKO YA MABOMU YATIKISA DAR E SALAAM.










Pichani baadhi ya Majeruhi wakiwasili Muhimbili. 
[ Read More ]

FEDHA BANDIA ZAINGIA KWENYE MZUNGUKO BONGO


KASHFA ya kukithiri kwa noti mpya bandia inazidi kuongezeka na sasa imebainika kuwa hata baadhi ya benki nchini zinashindwa kuzibaini na hivyo kujikuta zinaziingiza kwenye mzunguko.

Hali hiyo inatokana na Karani wa Fedha wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) Februari 14 kuchukua fedha benki ya CRDB tawi la Lumumba na bila kutambua hatimaye akagundua amepewa noti nyingi za Sh 10,000 zikiwa bandia.

Hata pale mmoja wa wafanyakazi wa TSN aliyepewa noti hizo alipokwenda kuweka baadhi ya noti hizo kwenye moja ya benki bila kujua kuwa ni bandia, karani wa benki hiyo alizipokea na kuzipitisha kwenye mashine na kuridhika kuwa ni halali.

Kitendo hicho kinaonesha kuwa mashine za benki hazizitambui noti hizo na hata wafanyakazi wenyewe wa benki yawezekana hawana utaalamu wa kutosha wa kutofautisha noti bandia na halali hasa za Sh 10,000.

Noti hizo ziligunduliwa na wafanyakazi waliopewa fedha hizo baada ya kuanza kuzitumia na kukataliwa mitaani ambapo jana baadhi yao walijikuta wakiwa na noti hizo.

Meneja wa Fedha wa TSN, Diana Lyatuu, alithibitisha kuchukuliwa fedha hizo kutoka benki ya CRDB tawi la Lumumba kwa kubadilishwa na hundi.

Noti nyingi ambazo zimezagaa ni zinazoishia na namba 366 na 362 ambazo ndizo wafanyakazi wengi wa TSN walikabidhiwa.

Mmoja wa wafanyakazi wa TSN, Nelly Mtema, alikamatwa na Polisi baada ya kuzitumia fedha hizo alizopewa ofisini kwa ajili ya kwenda kulipia bili ya maji katika ofisi za Kampuni ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO).

Akielezea tukio hilo, Mtema alisema Februari 15 asubuhi alikwenda Dawasco kulipia maji lakini akashangaa kuwekwa chini ya ulinzi kwa maelezo kuwa ana fedha bandia.

“Niliwakatalia kuwa si bandia kwani nililipwa ofisini, lakini nikapelekwa Polisi kituo cha Kimara,” alisema Mtema ambaye baada ya kuzichunguza noti hizo aligundua bandia zikiwa tatu za Sh 10,000.

Aliongeza kuwa baada ya sakata hilo, alilazimika kupiga simu ofisini, kufahamisha kuwa fedha alizopewa ni bandia na amekamatwa na polisi baada ya kuzitumia kulipia huduma ya maji.

“Ofisini walizungumza na polisi juu ya kuwapo tatizo hilo ndipo nikaachiwa,” alisema Mtema.
Mkurugenzi wa Masoko wa CRDB, Tully Mwambapa, alipoulizwa juu ya tatizo hilo, alisema ana uhakika asilimia 100 ya fedha hizo hazikutolewa na benki yake.

“Sisi tuna sheria inayomtaka mteja ahesabu na ahakiki fedha zake kabla ya kuondoka dirishani, itakuwaje keshia aondoke ndipo tupokee malalamiko ya kuwapo fedha bandia?” Alihoji Mwambapa.

Keshia wa TSN alipoulizwa alisema hakuona haja ya kuhakiki fedha hizo kwa vile anaiamini benki hiyo kwani amefanya nayo kazi kwa siku nyingi. Hata hivyo, Mwambapa alisema: “Benki yangu ina sera ya kutoaminiana katika mambo ya fedha.”

Alijitetea kuwa kila dirisha lina kamera inayochukua mwenendo wa matukio ya kuanzia asubuhi hadi jioni yanayofanywa na karani aliyepo kwenye dirisha husika. “Ndiyo maana nasema fedha hizo hazikutoka kwetu,” alisema
[ Read More ]

After 18 days of protest and nearly 30 years in power, Mubarak steps down


 
Egyptians celebrated in thousands after Vice President of Egypt, Omar Suleiman officially confirmed that Hosni Mubarak steps down as president and the country is now in the control of the army until the next election.

 
After 18 days of protesting starting from social networks like Facebook and Twitter, this is a true revolution.

 


 
Celebrations with fireworks at Tahrir Square

Barack Obama said in his statement from the White House that Egypt will never be the same again and in London David Cameron describing it as "precious moment of opportunity".

 

[ Read More ]

MAHAFALI YA NANE YA CHUO KIKUU CHA ZANZIBAR - ZANZIBAR UNIVERSITY




 Wahitimu wa somo la Law and Shariah wakitunukiwa Shahada ya digrii ya somo hilo,wakati wa mahafali ya nane katika Chuo kikuu cha Zanzibar Tunguu,yaliyofanyika jana
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Ali Mohamed Shein,akimpongeza Mtoto wake Asha Ali Mohamed Shein,wakati wa kutunukiwa Shahada ya Digrii ya Law & Shariah,katika mahfali ya nane,yaliyofanyika jana katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Zanzibar Tunguu,wilaya ya Kati,Mkoa wa Kusini Unguja.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Ali Mohamed Shein akiweka jiwe la msingi katika majengo mojawapo ya Chuo kikuu cha Zanzibar alipohudhuria mahafali ya nane ya chuo hicho.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Ali Mohamed Shein akiongozana na wakuu wa Chuo cha Zanzibar alipohudhuria mahafali ya nane ya chuo hicho.


Baadhi ya wahitimu wa katika mahafali ya nane ya chuo kikuu cha Zanzibar Tunguu,wakiwa katika maandamano wakati wa sherehe za mahafli yaliyofanyika chuoni hapo jana,na kuhudhuriwa na viongozi wakuu wa akiwemo,Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein.
[ Read More ]

UZINDUZI WA TAMASHA LA SAUTI YA BUSARA ZANZIBAR


BENDI ya Kikosi cha Askari Magereza wakiongoza Maandamano ya Uzinduzi wa Tamasha la Sauti ya Busara Zanzibar  likipita mitaani  wakati wa sherehe zahizo.


 WASANII wa Kikundi cha Ngoma ya Benbati nao hao wakijukuika.
WASANII wakishiriki maandamano ya Uzinduzi.


 NAO  wacheza ngoma ya Mbwa kachoka(beni) wakiwa katika maandamano ya uzinduzi wa Tamasha la Busara Zanzibar.

WASANII wa ngoma ya Benbati nao hawako nyuma katika maonesho ya Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar wakiwa katika Uzinduzi.
WANAWAKE  wakiwa  katika Vazi la kucheza Ngoma ya Mwanadenge wakipita mitaani katika uzinduzi wa tamasha la Sauti ya Busara Zanzibar.

 WASANII hao na mambo ya asili ya Muafrika  wakionesha  katika uzinduzi wa tamasha.
MSANII   Mkongwe wa Zanzibar Halikuniki akiwa na Zumari kupiota wote wakiwa katika Uzinduzi huo wakipita barabara ya Malindi kuelekea katika Viwanja vya Ngome Kongwe.
 HIVI  ndivyo ilivyo katika uzinduzi wa Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar.
WASANII wakiwa katika maandamano ya Uzinduzi wa Tamasha wakiwa katika mavyazi ya kiasili ya Afrika  wakiwa katika maandamano wakipita katika mitaa ya Michezani.
 WATALII wakipata picha ya Kumbukumbu ya Tamasha la Sauti ya Busara kwa Mwaka 2011 ili kuweka kumbukumbu yao walivyotembelea Zanzibar.
WASANII wa Ngoma ya Kiluwa wakiwa katika  maandamano ya  Uzinduzi wa Tamasha la Sauti ya Busara Zanzibar. 
WATALII wakiangalia Maandamano ya Tamasha la Busara yakipita barabara ya Forodhani ikiwa ni ufunguzi wa Tamasha hilo. 
[ Read More ]

UKWELI KAMILI KUHUSU VICHANGA WALIOFUKIWA SHIMO MOJA


Sakata la watoto wachanga 10 waliofukuliwa na jeshi la polisi katika shimo moja maeneo ya Mwananyamala, Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam wiki iliyopita limeingia katika sura mpya baada ya mama zao kujulikana.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili katika Hospitali ya Mwananyamala  kunakotajwa kwamba ndiko maiti za watoto hao wachanga zilikotoka, umebaini kwamba wazazi wanaohusika na tukio hilo wanafahamika na wako katika makundi matatu.

MAKUNDI MATATU
Chanzo chetu cha habari ndani ya hospitali hiyo kimedai kuwa kundi la kwanza lililotajwa kuhusika ni machangudoa wanaopata mimba lakini hawako tayari kulea watoto, hivyo kufika hospitalini hapo kwa nia ya kutoa. 

Imedaiwa kuwa machangudoa hao wanapofika hospitalini hapo huongea na baadhi ya wauguzi ambao baada ya kukubaliana kiasi cha fedha, huwawekea maji ya uchungu kisha kujifungua watoto wafu ambao hubaki hospitalini hapo kwa makubaliano kuwa watazikwa na watumishi kwa malipo maalumu.

Aidha, chanzo hicho kiliendelea kudai kwamba, zoezi la kutoa mimba hufanyika kwa siri. Imeelezwa kuwa  machangudoa hao wameshajenga  uhusiano mzuri na baadhi ya wauguzi ambapo wamekua wakiwapa fedha  kuanzia shilingi 30,000 na kuendelea ili kuharibu mimba bila uongozi wa juu wa hospitali kujua.
Imeelezwa kuwa gharama za kuchimba kaburi na kuzika watoto hao wachanga ni kati ya shilingi 20,000 hadi 25,000 ambazo mwenye mtoto hutozwa.

“Siku hizi hata mitaani huwezi kukuta maiti za watoto wachanga zikiwa zimetupwa kwenye mifuko ya plastiki kama ilivyokuwa zamani. Hii ina maana  kwamba wameshagundua kuwa hospitali ni kituo chao cha kutolea mimba,” kilisema chanzo hicho.

Aidha, kundi lingine lililotajwa kuhusika na vitendo hivyo ni wanafunzi wa sekondari na vyuo vikuu ambao wamekua wakijihusisha na ngono zembe, hivyo kupata ujauzito.

“Kimbilio lao ni hospitalini ambapo wamekua wakitolewa mimba kwa siri na ndiyo maana hata rekodi za watoto saba waliofukuliwa na polisi hazipo kwenye kumbukumbu za Hospitali ya Mwananyamala,” kilidai chanzo hicho.

Kundi la tatu linalohusishwa na maiti hizo za vichanga ni wazazi wasio na uwezo, wanaojifungulia njiani au hospitalini hapo na kwa bahati mbaya watoto wao kufariki. 

Wazazi hao hushawishiwa na baadhi ya wauguzi kutoa fedha kati ya shilingi 20,000 na 25,000 kwa ajili ya kuchimba kaburi na kuzikia kichanga kilichofariki.

JESHI LA POLISI 
Tayari jeshi la polisi nchini katika uchunguzi wake hospitali hapo limebaini majina ya wazazi watatu ambao maiti za watoto wao ni kati ya zile zilizofukuliwa wiki iliyopita.

Wazazi hao wametajwa kuwa ni Ruth Mtanga aliyejifungulia njiani Januari 27, mwaka huu na Furaha Rajabu, mkazi wa Manzese aliyejifungua Januari 24 mwaka huu ambaye kumbukumbu zinaonesha kuwa maiti ya mtoto wake ilichukuliwa siku hiyo hiyo na mtu aliyetajwa kuwa ni Zuberi Idrisa, baba mzazi wa marehemu.

Mzazi mwingine ni Regina Samwel, mkazi wa Kimara aliyejifungua hospitalini hapo mtoto mfu. Hata hivyo kumbukumbu katika chumba cha maiti hazioneshi mwili huo kuingia wala kutolewa.

Aidha, kati ya maiti 10 za watoto zilizofukuliwa, saba hazina kumbukumbu kama walizaliwa au kufia hospitalini hapo na kuzua utata kutokana na zote kukutwa zimeviringishwa kwenye shuka moja la Hospitali ya Mwanyamala, moja ikiwa imekaa zaidi ya siku tano kabla ya kuzikwa. 

Polisi wanamshikilia mmoja kati ya viongozi wa chumba cha kuhifadhia maiti hospitaini hapo kwa uchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hilo. 

MTANDAO HARAMU
Taarifa hizo zilieleza kwamba mtandao haramu uliopo hospitalini hapo ni mkubwa kwani unawajumuisha baadhi ya wauguzi, wafanyakazi wa chumba cha kuhifadhia maiti na madaktari.

“Hiki kilichotokea ni kama kutimia kwa usemi wa wahenga kuwa ‘za mwizi ni  arobaini’ kwa sababu biashara hii haramu haikuanza leo. Ninaliomba jeshi la polisi liendelee na uchunguzi, watabaini mengi mazito,” kilisema chanzo hicho.

Kiliendelea kusema kwamba, kulingana na makundi hayo matatu, wazazi wanaoweza kujitokeza ni wale waliojifungua wakiwa njiani au hospitalini na kwa bahati mbaya watoto wao wakafariki dunia.

“Machangudoa na wanafunzi hawawezi kujitokeza na inaonekana kuwa maiti saba ambazo wazazi wao hawajulikani wala hakuna kumbukumbu katika vitabu vya Hospitali ya Mwananyamala ni zao,” kilisema chanzo hicho.

USHAWISHI WA WAUGUZI
Habari zaidi zinadai kuwa wauguzi ndiyo wenye ushawishi mkubwa kwa  wafiwa ili waache maiti zao kwa makubaliano ya kuacha fedha kwa ajili ya kununulia sanda, kuchimba kaburi na kuzika.

Hata hivyo, imedaiwa kuwa hakuna maiti ya mtoto anayezikwa kaburi lake peke yake na badala yake wote hufukiwa kwenye shimo moja ambalo halina kina kirefu.

Hata hivyo, uongozi wa Hospitali ya Mwananyamala umelaumiwa kwa kutokagua kwa umakini chumba cha kuhifadhia maiti kwani inadaiwa kuwa kuna sehemu maalum iliyotengwa kwa ajili ya kuweka miili ya watoto wachanga wakisubiri wawe wengi ndipo wapelekwa kufukiwa katika shimo moja.

HATUA YA SERIKALI
Akizungumza na gazeti hili jana, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana alisema ripoti ya tume iliyoundwa bado haijakabidhiwa kwake lakini akaahidi kwamba atakapoipata ataitolea ufafanuzi.

Naye Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Polisi Kinondoni, Charles Kenyela alisema jana kuwa uchunguzi unaendelea na kuhusu maiti za watoto, hawajazikwa na zoezi hilo litafanyika mara baada ya upelelezi kukamilika.

Wiki iliyopita, watoto wachanga 10 waliofukiwa kwenye shimo moja walifukuliwa na polisi ambapo serikali iliunda tume kuchunguza tukio hilo na wakati wowote kuanzia leo taarifa ya uchunguzi huo itatolewa.

Hata hivyo, tume hiyo imepondwa vikali na baadhi ya wananchi hata kabla ya kutoa taarifa yake kwa madai kwamba asilimia kubwa ya wajumbe wake ni watumishi wa idara ya afya inayolalamikiwa. Watu wana wasiwasi kuwa wanaweza kuficha mambo mengi.

“Tangu lini kesi ya nyani akapewa ngedere na haki ikapatikana? Hii tume ni kiini macho, nia yao ni kupunguza hasira za watu,” alisema Juma Omari, mkazi wa Mwananyamala. 
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Lucy Nkya, wiki iliyopita alilaani kitendo hicho cha kufukiwa viumbe hao na kusema kuwa kwa kawaida watoto wanaozaliwa na kufa wakiwa na miezi mitano na kuendelea huwa wanahesabiwa kuwa ni viumbe, hivyo wanastahili kuzikwa kwa heshima zote. 


source:global puplisher
[ Read More ]

RAIS JK AVUNJA UKIMYA KUHUSU DOWANS



Ndugu Wana-CCM na Ndugu Wananchi;Jambo ninalotaka kulizungumzia sasa sikutaka kulizungumza kwa sababu Waziri Mkuu alishalifafanua baada ya semina ya Wabunge wa CCM na hata Mheshimiwa John Chiligati, Katibu wa Siasa na Uenezi Taifa alishalizungumzia. Sikuona umuhimu wa kufanya hivyo kwa sababu viongozi wenzangu hao wameelezea kwa ufasaha uamuzi wa Kamati Kuu na ule wa kikao cha pamoja cha Wabunge wa CCM.

Lakini, yapo maneno mengi ati mbona Rais yupo kimya sana, hatujamsikia kusema chochote? Niseme nini zaidi na hao wote wameshasema kwa niaba yangu. Wapo wanaosema nipo kimya kwa sababu nahusika na Downs na ati ndiyo mwenyewe hasa. Wapo wanaosema niko kimya au nashindwa kuchukua hatua, kwa sababu marafiki zangu wamehusika. Nawalinda. Kwa sababu hiyo, nikaona nami nisema angalau watu wanisikie lakini sina la ziada ni yale yale yaliyokwishasemwa.

Kwanza niseme wazi kwamba ule msemo wa wahenga wa akutukanae hakuchagulii tusi hapa umetimia. Napenda kuwahakikishia wana-CCM na wananchi wenzangu kuwa sina uhusiano wowote wa kimaslahi kwa namna yoyote ile na kampuni ya Dowans. Sina hisa zozote wala manufaa yoyote yale. Pia sina ajizi wala kigugumizi cha kuchukua hatua kwa sababu ya rafiki yangu au hata kama angekuwa ndugu yangu kahusika. Maamuzi yaliyofanywa na Kamati Kuu na Kamati ya Chama ya Wabunge wa CCM yalifanywa chini ya uogozi wangu. Ni uthibitisho tosha wa ukweli huo. Waliokuwepo kwenye vikao hivyo wanajua ukweli wa haya ninayosema. Ningekuwa na maslahi au hofu tusingefanya uamuzi ule.

Wana-CCM Wenzangu na Wananchi Wenzangu;Kama mtakavyokumbuka tulipoingia madarakani nchi ilikuwa na tatizo kubwa la ukame mkali sana ambao haujawahi kutokea. Mavuno ya chakula yalikuwa mabaya tukawa na njaa kali na watu 3,776,000 walilazimika kuhudumiwa na Serikali. Aidha, mito mikubwa na midogo ikapungukiwa sana maji na mingine kukauka kabisa. Matokeo yake ni mabwawa yetu yote ya kuzalisha umeme yakakosa maji hivyo uzalishaji wa umeme ukaathirika vibaya sana na nchi ilikuwa gizani.

Ili kukabiliana na tatizo hilo ushauri ulitolewa na TANESCO nasi tukaukubali kuwa wakodishe mitambo ya kuzalisha umeme kutoka nje. Serikali tukaombwa kugharamia ukodishaji huo. Taratibu za kisheria zikafanywa, tenda zikatangazwa na washindi wakapatikana Aggreco, Richmond na Alstom. Kampuni za Aggreco na Alstom zilileta mitambo yao kwa wakati lakini kampuni ya Richmond ikawa inasuasua. Wakati huo huo maneno mengi yakawa yanazagaa kuhusu Richmond kutostahili kupewa tenda kwa sababu ya kutokuwa na uwezo kwa kampuni hiyo na kampuni hiyo kutokuwa hai. Ikadaiwa kuwa wamepewa tenda kwa sababu ya kubebwa na baadhi ya viongozi Serikalini. Maneno hayo yalifanya Wizara ya Fedha wasite kutoa fedha za kuanzia kwa kampuni hiyo. Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini wakati ule alipokuja kuniomba niingilie kati ili kampuni hiyo ilipwe malipo ya awali (down payment) nikataa na kumwambia Waziri aachane nao kwani kampuni hiyo ni ya mashaka. Hivyo kampuni ya Richmond haikulipwa down payment, wakashindwa kutimiza mkataba. Maneno yakazidi kadri makali ya kukosa umeme yalivyoendelea kuuma.

Baada ya hapo kampuni ya Richmond ikauza mkataba wake kwa kampuni ya Dowans ambayo ilileta mitambo na uzalishaji wa umeme ukafanyika na kupunguza kabisa makali ya mgao. Tuhuma kuhusu Richmond ziliendelea kulindima mpaka hatimaye Tume ya Bunge ikaundwa na kugundua kuwa Kampuni iliyouziwa haikuwa hai na ni ya mfukoni. Hatima ya Tume hiyo tunaijua sote. Aliyekuwa Waziri Mkuu na Mwawaziri wawili waliwajibika. Zile tuhuma za yeye kuwa ndiye mwenye kampuni hazikuthibitika lakini aliwajibika kwa sababu yeye ndiye aliyetoa kauli ya kukubali ipewe tenda ili kuepusha nchi isiwe gizani.

Miezi kadhaa baadaye, likazuka sakata la Dowans ifutiwe mkataba kwa hoja kuwa wamerithi mkataba na kampuni ambayo haikupata kihalali mkataba wake. Kamati ya Bunge ilisema hivyo na wanasheria wa TANESCO pia walishauri hivyo. TANESCO ikavunja mkataba. Dowans hawakuridhika, wakashitaki kwenye Baraza la Usuluhishi kama yalivyo masharti ya mkataba waliotiliana sahihi. Madai yamesikilizwa na TANESCO imeonekana ni mkosaji hivyo wakatozwa fidia ya Dola za Marekani 64 milioni.

Taarifa hiyo imetushtua wengi. Niliuliza na kupewa ushauri mbali mbali. Wapo
waliosema lazima tulipe, wapo waliosema tusilipe, wapo waliosema tusiharakishe kulipa kwani kuna uwezekano wa kutokulipa kwa kutumia sheria. Uamuzi wangu ukawa tusiharakishe kulipa, tutafute njia za kuepuka katika kulipa. Ndiyo maana ya taarifa ya Mheshimiwa Chiligati na ile ya Waziri Mkuu.

Ni mzigo mkubwa mno kwa TANESCO kubeba, hivyo tufanye kila tuwezalo tuepuke kulipa. Tumewataka wanasheria wetu wasaidiane na wale wa TANESCO kuhakikisha hilo halitokei. Nataka kuwahakikishia kuwa na mie ni miongoni mwa wale wasiotaka TANESCO ilipe, hivyo kauli za kuhusika na Dowans inanishangaza maana nisingeamua hivyo katika Kamati Kuu na Kamati ya Wabunge wa CCM. Ama kweli akutukanae hakuchagulii tusi.
[ Read More ]