Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

R.I.P Whitney Houston.

 
Whitney Houston, who found fame as one of pop’s biggest voices, has died. She was 48.
Houston died Saturday afternoon, a representative for the singer told the Associated Press. Houston’s death comes on the eve of the Grammys and on the night of Clive Davis’ annual pre-Grammy gala, at which she performed last year and was expected to attend this year.
No cause of death has been announced and law enforcement sources said the singer was found in a hotel room at the Beverly Hilton, where emergency medical personnel were called sometime Saturday.

The Hilton is the scene for Davis’ annual gala. On Thursday, Houston dropped by the rehearsals to offer vocal tips for Brandy and Monica, who were slated to be one of the evening’s headliners.
Press, including The Times, were in attendance for a junket with the reunited R&B divas and Davis. Though Houston greeted people her with a warm smile, she appeared disheveled in mismatched clothes and hair that was dripping wet with either sweat or water.
The visibly bloated singer displayed erratic behavior throughout the afternoon -- flailing her hands frenetically as she spoke to Brandy and Monica, skipping around the ballroom in a child-like fashion and wandering aimlessly about the lobby. It was mentioned by a Grammy staffer that security personnel received calls of the singer doing handstands by the pool.
After leaving rehearsals, Houston returned to the ballroom -- with her teenage daughter Bobbi Kristina in tow -- as camera crews set up for interviews. The singer smelled of alcohol and cigarettes. A Grammy staffer said that during the interviews with Brandy, Monica and Clive, Houston was dancing just off camera to make the singers and Davis laugh. Grammy personnel expressed concern that she'd be caught on camera, and that reporters would write about her behavior.
Finally her daughter pulled Houston out of the room, and the singer skipped off. In our post of the event, we called Houston's behavior "loose and lively."
“She really loves and supports us both. For me, I went through a lot of very tumultuous moments and she would show up, not just with a phone call but physically when I needed,” Monica said when we asked about Houston coaching them. “That's something that I've carried with me, especially with all that she's been going through over the years herself. She's never turned her back on the people she cared about.”
Later that evening Houston appeared at Hollywood nightclub Tru, for fellow R&B singer Kelly Price’s pre-Grammy party. "Kelly Price & Friends Unplugged: For the Love of R&B" served as both a celebration and a jam session to preserve that genre, which was scaled back from eight categories to four this year.
Houston was billed as one of the evening’s special invited guests but after her appearance earlier it was shocking to see the singer arrive. More put together in her appearance, Houston briefly sang a duet with Price. In what has become her final performance, clips of the two singing a gospel hymn made the rounds because of the singer’s unsteady vocals.
SOURCE: Los Angeles Times
[ Read More ]

HATIMAE JAY-Z & BEYONCE WAMEWEKA PICHA ZA MTOTO WAO (BLUE IVY) KWENYE MITANDAO YA KIJAMII



                                   Mtoto Blue Ivy















                                Mtoto Blue Ivy.

                   Beyonce akiwa na Mwanae Blue Ivy


                     Jay-Z akiwa na mwanae  Blue Ivy

[ Read More ]

MANY CONGRATS.


Many  Congrats to  my Baby Sister Mariam Tawe  for great form 4 result ..beauty with purpose......Education is sexy.... i am so proud of you dear xoxo.....
[ Read More ]

DALILI ZA KUWA NA STRESS



Kuna mambo mengi au hali flani inaweza kuwa inajitokeza kwako mara kwa mara na usijue ni nini, au ukapuuzia lakini baadae ikaja kukuletea madhara makubwa. Ukiona mtu au kuhisi dalili zifuatazo, ujue ndio mwanzo wa stressKimbia ukapate msaada kabla mambo hayajaharibika 

1. Kutojiamini
 

2. Kujawa na mawazo mengi kichwani (Msongo wa mawazo)
3. Kuwazia mabaya wakati wote
4. Kuongea kwa sauti (Shouting)

5. Kula chakula au kunywa pombe kupindukia
6. Kushindwa kula (Kupoteza hamu ya chakula) 
7. Kushindwa kujichanganya na watu (Anti-Social)

8. Kusahau vitu mara kwa mara 
9. Kupata tabu ku concentrate katika mambo
 
10.Matatizo ya tumbo, mdomo kukauka, misuli kukaza na kutoka jasho mara kwa mara

11. Kuamka mapema 
12. Moyo kwenda mbio
 
13. Kusikia joto
 
14. Kichwa kuuma

YAFANYIE KAZI KABLA HUJACHELEWA

source jaydee.

[ Read More ]

Watoto 4750 Wanaishi Mazingira Magumu Wete



WATOTO 4750 kutoka shehia 22 za wilaya ya Wete wanaishi katika mazingira magumu mno, utafiti uliofanywa na kitengo cha hifadhi ya mtoto Pemba, umebainisha.

Afisa kutoka kitengo cha hifadhi ya mtoto Pemba, Raya Said aliliambia gazeti hili katika mahojiano maalum kwamba, watoto hao walibainika katika kaya zote zilizo ndani ya wilaya hiyo.


Alisema hao ni wale wanaoishi katika mazingira magumu mno, ambao hawana msaada wala usaidizi wowote, ambapo miongoni mwao wapo pia wanafunzi wa kike.

Shehia zilizoandikisha rekodi ya juu ni Kojani ambapo watoto 186 wakiwemo wanawake 83 wanaishi katika mazingira ya kusikitisha.

Shehia nyengine ni Kigongoni yenye watoto 386 wakiwemo wanawake 201, Mtambwe kaskazini watoto 281 wakiwemo wanaume 117, Pembeni watoto 121, Gando (126), Junguni (100) na Kisiwani watoto 115.

Raya alisema tatizo kubwa linalowakabili watoto hawa ni huduma muhimu za kijamii ikiwemo chakula cha uhakika, mavazi, malazi na matunzo kutoka kwa familia zao, hali iliyowafanya wengi kuishi katika maisha ya kukata tamaa.

Aidha alisema baadhi ya watoto hawana sare za skuli na wale walionazo zimechakaa mno.

Hali hiyo imewafanya watoto wengi kukatisha masomo na kujishughulisha na ajira mbadala ambazo ni hatari kwa afya zao.

Afisa huyo alisema baadhi ya familia zimekuwa zikiwatumia watoto hao kama mtaji; kwa kwenda kufanya kazi ili waendeshe familia zao ikiwemo kupara samaki.

Aliziomba asasi za kiraia za kitaifa na kimataifa kushirikiana na kitengo chake kusaidia kumkomboa mtoto na kumuweka katika mazingira bora kielimu na kiafya.
[ Read More ]

Wanafunzi 19 Waozeshwa Waume, Wapewa Mimba Chake



WANAFUNZI 19 walipewa mimba na kuozeshwa waume katika skuli 9 za wilaya ya Chake kuanzia mwaka 2008 hadi mwaka uliopita, wakiwemo wanafunzi wawili wa darasa la tano na saba kutoka skuli za Vitongoji na Pujini ambao wote walipewa mimba.

Kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Pemba, wanafunzi sita walipewa mimba au kuolewa katika skuli ya Ndagoni mwaka 2008 pekee.


Aidha wanafunzi wengine watatu wa kidato cha tatu kutoka skuli ya Kilindi na mmoja wa kidato cha kwanza kutoka skuli ya Pujini walikutwa na masaibu kama hayo mwaka 2009.

Hali kama hiyo ilitokea mwaka 2010 katika skuli za Vikunguni, Chanjamjawiri, Shamiani, Uwandani na Birikau, ambapo jumla ya wanafunzi watano wa kuanzia darasa la saba hadi kidato cha pili walipewa ujauzito au kuozeshwa waume.

Kwa mwaka uliopita jumla ya kesi nne zimeripotiwa katika skuli za Vikunguni, Pujini, Shamiani na Vitongoji ambapo wanafunzi watatu wa darasa la tano, saba na kidato cha pili walipewa ujauzito na mmoja wa kidato cha tatu kupewa mume.

Aidha kesi 113 zinazohusisha ubakaji, mimba, kuozeshwa waume na ukatili mwengine wa kijinsia ziliripotiwa katika wizara ya Ustawi wa Jamii Pemba katika kipindi cha Julai 2010 hadi Juni 2011.

Mkoa wa Kusini Pemba uliandikisha kesi 67 zikiwemo sita za ubakaji na 32 za utelekezaji watoto.

Afisa Mipango Wizara ya Ustawi wa Jamii, Maendeleo ya Wanawake na Watoto Pemba, Salama Mbarouk Khatib , alisema tatizo hilo zaidi limechangiwa na ushawishi wa kundi rika.

Alisema baadhi ya wanafunzi wa kike wamekuwa wakiwashawishi wenzao kuanzisha uhusiano wa kimapenzi ili waweze kufaidika na fursa walizonazo wao.

Alisema changamoto nyengine ni kukosekana huduma muhimu katika skuli zenye dakhalia, ambapo mtoto wa kike hulazimika kutafuta chakula kwa gharama zake, akiwa mbali ya wazazi wake, ambao hata hivyo wengi hushindwa kuwakamilishia mahitaji kwa sababu ya umaskini.

Salama alisema baadhi ya wazazi wamekuwa ving'ang'anizi kwa kulazimisha watoto wao kuolewa hata kama wao hawako tayari.

"Tumeshuhudia wazazi wakimsusa mtoto wao na kufikia hatua ya kumfichia sare zake na mabuku kuyachoma moto kwa sababu tu amekataa kuolewa," alisema.

Mkuu wa wilaya ya Chake Chake, Mwanajuma Majid Abdalla kwa upande wake, alisema katika miaka ya nyuma tatizo hilo pia lilikuwa linachangiwa na walimu ambao walikuwa wakiwadhalilisha wanafunzi wa kike kingono.

Hata hivyo, alisema wilaya kwa kushirikiana na taasisi nyengine wamekabiliana na walimu hao kwa kuwakumbusha kuzingatia maadili yao.

Alisema wilaya kwa ushirikiano na maafisa wa elimu na kutoka wizara ya jinsia wamefanikiwa kuzivunja ndoa nyingi, ambazo ziliwahusisha wanafunzi wa kike.

Afisa Mipango, Sera na Utafiti kutoka wizara ya Elimu Pemba, Khamis Ali alisema tatizo la mimba, ndoa za kushurutishwa zimekuwa zikipungua kutokana na mwamko walionao wanafunzi pamoja na wazee wengi.

Aidha alisema kukosekana huduma za dakhalia pia inaweza kuwa moja ya vyanzo vya matukio hayo, ambayo yanaathiri maendeleo ya elimu ya mtoto wa kike.
[ Read More ]

Kidongochekundu Dispensary Yafungiwa

BODI ya Ushauri wa hospitali Binafsi imeifungia hospitali moja na kutoa onyo kwa hospitali nne kutokana matatizo ya mbali mbali ikiwemo ukosefu wa wafanyakazi wa kutosha pamoja na mazingira yasiyo salama ya utoji huduma za afya.

Msaidizi Mrajis wa Bodi ya Ushauri wa Hospitali Binafsi, Dk. Shaaban Seif Mohammed aliitaja hospitali iliyofungiwa ni Kidongoochekundu Dispensary na zilizopewa onyo kali ni Hassan Clinic, SDA Dispensary, Jang’ombe Dispensary pamoja na Kwamchina Dispensary.


Alitaja miongoni mwa makosa yaliyobainika ni pamoja na kutowasilisha vielelezo vya wafanyakazi wao pamoja na uchafu wa takataka za mabomba ya sindano ambayo yametumika kwa muda mrefu bila kutupwa sehemu husika.

Akizungumzia kwa hospitali iliyofungwa na pamoja na kukuta mfanyakzi mmoja anaefanya kazi zote za kiuguzi pamoja na kidaktari jambo ambalo linaweza kuhatarisha zaidi utoaji wa huduma bora za matibabu kwa wagonjwa wanaofika hospitalini hapo.

Alifahamisha pia kuwa hospitali ya kwa Mchina na DSA Dispensary Jang’ombe ndio zilizobainika kuwa na kasoro nyingi ikiwemo uchakavu wa majengo hasa kuta za ndani pamoja na sehemu ya kufungia vidonda kuwa sakafu yake imechimbika jambo ambalo linaweza kupelekea maambukizi ya maradhi zaidi kwa wagonjwa.

Alisema Bodi hiyo imetoa muda wa mwezi mmoja kwa wamiliki wa hospitali hizo kurekebisha kasoro hizo kwa lengo la kutoa huduma zenye ubora wa hali ya juu kwa mujibu wa taratibu za kisheria.

Alisema vitendo vinavyofanywa na baadhi ya hospitali Binafsi si vizuri na vinaenda kinyume na maadili ya utoji wa huduma za Afya hali inayoweza kurudisha nyuma maendeleo ya serikali katika kuimarisha huduma za afya kwa jamii.

Ametoa tahadhari kwa wananchi kuwa waangalifu wanapokwenda hospitali hizo kuwa na kuacha mara moja kutumia hospitali ambazo zina kasoro za utoaji huduma za afya.

Alifahamisha bodi inazifanyia ukaguzi wa mara kwa mara hospitali hizo ili kuhakikisha zinafanya marekebisho ya kasoro walizonazo na iwapo watakaidi bodi haitasita kuwachukulia hatua kali za kisheria ikiwemo kuzifungia moja kwa moja.

Alisema serikali imekuwa ikichukua juhudi kadhaa katika kuhakikisha hospitali binafsi zinatoa huduma zenye ubora kwa wananchi kwani zinasaidia sana katika kupunguza misongamano kwenye hospitali za serikali.
[ Read More ]

Mawakili Wataka Kesi ya Mv Spice Kupelekwa Mahakama Kuu Malumbano ya sheria yatawala mahakamani

UPANDE wa utetezi unaoisimamia kesi ya washitakiwa wa kuzama kwa meli ya Mv. Spice Islanders, imemshauri Kaimu Mrajis wa Mahakama Kuu Zanzibar, Essaya Kayange, kuihamishia kesi hiyo Mahakama Kuu ili maamuzi ya kisheria yaweze kupatikana.

Upande huo wa utetezi ulidai kuwa, katika kesi hiyo kuna baadhi ya mambo ya msingi ambayo mahakama hiyo haina uwezo wa kuyatoa kwa mujibu wa sheria, badala yake lazima yatolewe na Mahakama Kuu.

Hayo yameelezwa na wakili wa kujitegemea Masumbuko Lamwai, mbele ya Kaimu Mrajis huyo wakati kesi hiyo inayowakabili watuhumiwa 11 akiwemo Mwakilishi wa Jimbo la Muyuni Jaku Hashim Ayoub, kufikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa.


Watuhumiwa hao ni Said Abdallah Kinyanyite, Abdallah Mohammed Ali, Yussuf Suleiman Issa (Kassu), Simai Nyange Simai, Haji Vuai Ussi, Abdallah Mohammed Abdallah, Juma Seif Juma, Hassan Mussa Mwinyi, Salim Said Mohammed Battashy, Mohammed Hasnuu Makame pamoja na Jaku Hashim Ayoub.

Lamwai alisema kuwa, kuna mambo mengi yanahitajika kuzungumzwa katika kesi hiyo, lakini inashindikana kutokana na uwezo ulionao mahakama hiyo ambayo haitaweza kuyatolea maamuzi.

Alisema kuwa, kwa mujibu wa sheria kesi hiyo ilikuwa ifikishwe Mahakama Kuu ambayo ndiyo yenye mamlaka ya kuisikiliza na sio Mrajis wa mahakama, na kama suala ni mahakama tu basi ilikuwa isikilizwe na mahakama ya mkoa.

Kwa upande mwengine akiungana na hoja za wakili Hamid Mbwezelani juu ya suala zima la kutokamilika kwa upelelezi wa kesi hiyo wakili Lamwai alisema kuwa hoja hizo hazina msingi mahakamani hapo.

Alidai kuwa Tume ya Uchunguzi iliyofanya uchunguzi wake ilikuwa na Jaji wa Mahakama Kuu pamoja na Mwendesha Mashitaka wa serikali, ambao wao ndio wanaowashuku watuhumiwa wa kesi hiyo, lakini Mwendesha Mashitaka huyo huyo anadai kuwa upelelezi wake bado haujamilika.

“Mheshimiwa kesi hii haikuletwa mahakamani kwa misingi ya kisiasa ya kuwapoza wananchi waliofikwa na maafa, bali imekuja kwa misingi ya kisheria, na kama ipo kwa misingi ya kisiasa basi haipaswi kuwepo hapa”, alisema Lamwai.

Alisema kuwa, kimsingi upelelezi wake tayari umeshafanywa na Tume hiyo, na pendekezo lake linaheshimika kwa ushahidi wao na hakuna wa chini yake akatoa hoja zake za kupingana na hizo.

Alisema kuwa, suala hilo la kutokamilika kwa upelelezi ni sawa na kuwatia hatiani watuhumiwa hao kabla ya kutiwa hatiani na mahakama.

Mapema wakili Hamid Mbwezeleni aliiambia mahakama hiyo kwa kudai kuwa wanashindwa kuelewa ni uchunguzi gani unaofanywa juu ya kesi hiyo wakati ripoti yake tayari imeshatolewa.

“Sizushi kama uchunguzi umefanywa na ripoti yake kutolewa na miongoni mwa wachunguzi ni Jaji Mkuu na kuamua watuhumiwa wafikishwe mahakamani, kwani hawakuwa na shaka kwa tuhuma walizokuwa nazo ndiyo maana wakaamua kuwaleta mahakamani”, alisema wakili Mbwezeleni.

Hivyo alisema kuwa suala la kutokamilika kwa upelelezi halina mashiko, na kuiomba mahakama hiyo ilikatae ombi lao hilo na kama kuna ulazima wa kukubaliwa, basi watuhumiwa hao waondolewe udhia wa kwenda na kurudi mahakamani, hadi watakapokamilisha upelelezi wao.

Akijibu hoja hizo, Mwendesha Mashitaka wa kesi hiyo Mohammed Khamis, Mwanasheria wa serikali kutoka Ofisi ya DPP, alisema kuwa suala la uchunguzi uliofanywa na Tume hauhusiani kabisa na upelelezi wa upande wa mashitaka.

Alifahamisha kuwa, Tume iliyoundwa kutafuta chanzo cha ajali imetoa mapendekezo mengi ya kisheria na ya kiutendaji na si lazima yafuatwe, na kwa msingi huo mapendekezo yote hayo jukumu la kuamua nani ashitakiwe na nani asishitakiwe lipo kwa Mkurugenzi wa Mashitaka.

Aidha alisema kuwa, ijapokuwa Mwendesha Mashitaka wa serikali alikuwemo katika Tume hiyo, lakini uwepo wake huo hauhusiani kabisa na utendaji wake huo bali alikuwa ni Katibu wa Tume hiyo.

“Tume imetoa maoni yake na Ofisi imetimiza wajibu wake, sisi tunajenga upelelezi ambao utaishawishi mahakama na si kufuata maoni ya Tume ni vitu viwili tofauti visivyoingiliana kiutendaji, na mahakama inafahamu hilo”, alisema Mwanasheria huyo wa serikali.

Baada ya hoja za pande mbili hizo, hakimu Essaya Kayange ambaye pia ni hakimu wa mahakama ya mkoa Vuga aliiahirisha kesi hiyo hadi Machi 7 mwaka huu kwa maamuzi.
Mbali ya mawakili hao upande wa utetezi pia ulikuwa ukisimamiwa na wakili Abdallah Juma pamoja na Kepteni Bendera.

Katika kesi hiyo, watuhumiwa wote hao wanakabiliwa na mashitaka ya uzembe na kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo hali iliyosababisha kuzama kwa meli ya Mv. Spice Islanders na kuua watu 203, Septemba 10 mwaka jana.
[ Read More ]

Baridi kali yaua zaidi ya watu 160 Ulaya



 

Baridi iliyoleta kizaazaa barani Ulaya imekwishaua watu 164, huku watu wanaoishi katika nchi za Ukraine na Italia wakiwa katika shida kubwa ya kukabiliana na viwango vya baridi ambavyo vimevunja rekodi barani Ulaya.

 
Vijiji vyote vilivyopo katika eneo la mashariki ya Ulaya vilipoteza mawasiliano hapo jana kutokana na baridi kali na theluji, huku maelfu ya wakaazi wake wakishindwa kutoka nje ya nyumba zao.

Hali ya hewa hiyo ambayo haijashuhudiwa kwa miongo kadhaa sasa barani Ulaya, ilisababisha pia barabara kutopitika, usafiri wa ndege na reli kushindwa kufanya kazi na matumizi ya gesi kupanda ghafla katika eneo hilo.
Na wakati watabiri wa hali ya hewa wakionya kutokea kwa baridi kali zaidi siku za usoni, maelfu ya watu nchini Ukraine wanatafuta hifadhi ili kuepukana na theluji hiyo iliyokwishaua jumla ya watu 101, mpaka kufikia leo asubuhi.
Mmoja wa watu wasio na makazi nchini Ukraine katika baridi kali.Mmoja wa watu wasio na makazi nchini Ukraine katika baridi kali.Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Afya kutoka mjini Kiev, takriban watu 1,600 wameomba uangalizi wa kitabibu baada ya kupatwa na homa kali inayoathiri mfumo wa upumuaji na wengine kupata ganzi miguuni kutokana na baridi hiyo kali iliyofikia kiwango cha nyuzi za celisiasi 35 chini ya sifuri.
Na huko mjini Warsaw, Poland watu tisa wamethibitishwa kupoteza maisha baada ya kemikali aina ya zebaki kushuka mpaka kufikia nyuzi za selisiasi 32 chini ya sifuri ambayo ni sawa na nyuzi joto za Fahrenheit 25.6 chini ya sifuri.
Idadi hiyo mpya inaongeza vifo vilivyosababishwa na baridi nchini Poland kufikia watu 29, tangu juma lililopita.
Na mjini London, Uingereza Ofisi inayoshughulikia utabiri wa hali ya hewa imetangaza hali hiyo kuendelea katika maeneo mengi zaidi na theluji itaendelea kuanguka kwa kiwango kikubwa zaidi mjini Kiev, hii leo.
Aidha, Utabiri wa hali ya hewa unaonesha mji wa Berlin hapa Ujerumani utapatwa na theluji kali na baridi itafikia nyuzi joto za selisiasi kumi chini ya sifuri.
Na hofu zaidi inapanda kwa watu wasiokuwa na makazi hasa wale wanaoishi mitaani na kulala barabarani. Shirikisho la Kimataifa la Msalaba Mwekundu na jumuiya zake ziko katika harakati za kuwatafutia ufumbuzi watu hao.
Mwakilishi wa shirikisho hilo Zlatko Kovac, ameliambia Shirika la Habari la Ufaransa kuwa watu hao wasio na makazi wamejikuta taabani na bila tahadhari yoyote na wako katika hali mbaya kwa sasa.
Nchi zilizoathirika na baridi hilo ni pamoja na Italia, Poland, Ukraine, Bulgaria, Romania, Ujerumani, Uingereza na Urusi.

[ Read More ]

TUMUOMBEENI VENGU JAMANI





   Watanzania  tumuombeeni Vengu  apone haraka he is still in coma.so sad jamani.tumuombee sana.
[ Read More ]