Ni miaka kumi na tatu (13) tangu ututoke baba yetu mpendwa Mustafa Katuli.Unakumbukwa sana na watoto wako Farida,Othman,Maana,Khadija na Rehema. pia na Ndugu,jamaa na marafiki zako,Tulikupenda sana ila Mungu amekupenda zaidi. Allah akulaze mahala pema peponi. Amin.
Mcheza filamu mashuhuri sana duniani,Angelina Jolie amesema kwamba amekatwa matiti yake yote pamoja na kuondoa mfuko wake wa uzazi.
Kwenye taarifa aliyoandika kwenye gazeti la New York Times, Bi Jolie amesema alifanyiwa uchunguzi wa celi zake na kugunduliwa kwamba alikuwa katika hatari kubwa sana ya kupata saratani ya matiti. Ndipo akaamua kukatwa matiti yake mawili.
Taarifa zinazohusiana
Angelina mwenye umri wa miaka 37 na mama na watoto sita, alipoteza mamake mzazi kutokana na maradhi ya saratani ya matiti.
Anasema aliandika taarifa hiyo kuwahakikishia watoto wake kwamba hakuwa kwenye hatari ya kupata saratani tena.
Kulingana na Jolie madaktari walisema kuwa uwezekano wake kupata Saratani ya matiti ni asilimia 87 huku akiwa na asilimia 50 uwezo wake wa kuugua Sarati ya mfuko wa uzazi.
''Niliamua kuchukua hatua mwenyewe ili kuzuia uwezekano wowote wa kuugua Saratani hiyo,'' alisema Jolie.
Alisema kuwa shughuli hii ilianza mwezi Februari na kukamilika mwishoni mwa mwezi April.
Uwezekano wapunguzwa.
Katika taarifa iliyoandikwa na Bi Jolie na yenye kichwa, 'Uamuzi wangu wa kimatibabu', Bi Jolie alieleza kuwa mamake alipambana na Saratani kwa miaka kumi na kufariki akiwa na umri wa miaka 56.
Alisema kuwa alielewa fika kuwa siku moja atawahi kuugua Saratani na ndio maana akachukua uamuzi wa kufanyiwa upasuaji huo mgumu wa wiki tisa ambao ulihitaji kukatwa matiti.
Uwezekano wake wa kuugua saratani sasa umeshuka kutoka 87% hadi 5%.
Alimsifu mumewe Brad Pitt, kwa kumuunga mkono na kumfariji kwa kila aliyopitia, na kusema kuwa ametulizwa na kuwa wanawe hawakupata lolote katika matokeo ya uchunguzi wa madaktari tangu kufanyiwa upasuaji.
"ninahisi kuwa na nguvu kwa uamuzi niliofanya, na kwa kuwa ninasalia kuwa mwanamke hata baada ya kuondoa viungo hivyo,'' alisema Bi Jolie.
"kwa mwanamke yeyote anayesoma maneno haya, natumai ataweza kujua kuwa wanaweza kufanya uamuzi.''
Muigizaji huyo, ambaye ameshinda tuzo nyingi kwa uigizaji wake, pia ni mtunzi wa filamu na mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa anayehusika na harakati za kibinadamu.
Wakati alipokuwa anafanyiwa upasuaji, Bi Jolie alizuru Jamuhuri ya Kidremokrasia ya Congo pamoja na waziri wa mambo ya nje wa Uingereza William Hague.
Jolie pia alihudhuria mkutano wa mawaziri wa mambo ya nchi za kigeni wa G8, kuhamasisha dunia kuhusu dhulma za kingono katika maeneo ya vita.
Kaimu Balozi Mdogo wa Oman Zanzibar Saleh Suleiman, akisalimiana na Kiongozi wa Msafara wa Wajumbe wa Oman waliowasili Zanzibar leo kwa ajili ya matayarisho wa Mkutano wa Historia na Utamaduni wa Kiislam. unaotarajiwa kufanyika mwezi wa september 2013 Zanzibar.
BALOZI wa Oman nchini Tanzania Yussuf Al Bakar ( katikati) akiongozana na Ujumbe kutoka Nchini Oman ukiwasili Zanzibar kwa ajili ya matayarisho ya Mkutano wa Kimataifa wa utakaozungumzia Historia na Utamaduni wa Kiislam Zanzibar kulia Kiongozi wa Ujumbe huo Dk. Hamed Mohammed Al Dhawiyaniy, ni Mwenyekiti wa Taifa wa Mamlaka ya Makumbusho ya Taifa ya Oman. Na kushoto Kaimu Balozi Mdogo wa Oman Zanzibar Saleh Suleiman
Ujumbe wa Oman ukiwa katika ukumbi wa Wageni katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume wakibadilishana mawazo baada ya kuwasili Zanzibar leo.
Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Dkt. Haji Mwevura Haji,akizungumza katika mkutano na Ujumbe wa Oman, uliowasili Zanzibar kwa matayarisho ya mkutano wa Historia na Utamaduni wa Kiislam, kushoto Dk. Hamed Mohammed Al Dhawiyaniy, ni Mwenyekiti wa Taifa wa Mamlaka ya Makumbusho ya Taifa ya Oman,na kulia Mkurugenzi Mkuu wa Kitengo cha Historia ya Uislam Oman Dkt.Halit Eren.
Mkuu wa Msafara wa Ujumbe wa Oman uliowasili Zanzibar kwa matayarisho wa Mkutano wa Kimataifa utakaozungumzia Historia na Utamatudi wa Kiislam, Dk. Hamed Mohammed Al Dhawiyaniy, ni Mwenyekiti wa Taifa wa Mamlaka ya Makumbusho ya Taifa ya Oman,Zanzibar ina mahusiano ya Kihistoria na Mataifa ya Kiarabu katika historia na Utamaduni wa Kiislam.kulia Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Dkt. Haji Mwevura Haji na Mkurugenzi Mkuu wa Kitengo cha Historia ya Uislam Oman Dkt.Halit Eren,
Mkuu wa Skuli ya Kiswahili na Lugha za Kigeni Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar Dkt. Issa Haji Zidi, akitafsiri katika mkutano huo kutoka katika lugha ya Kiarabu, wakati wa mkutano huo wa matayarisho ya Mkutano wa Kimataifa wa Historia na Utamaduni wa Kiislam unaotarajiwa kufanyika Zanzibar mwezi wa September 2013.
Mkurugenzi Mkuu wa Kitengo cha Historia ya Uislam Oman Dkt.Halit Eren, akizungumza katika mkutano huo uliowashirikisha Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar SUZA,
Ujumbe wa Oman wakimsikiliza Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Dkt. Haji Mwevura Haji, akizungumza katika mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa SUZA Majestiki Zanzibar.
Ujumbe wa SUZA wakiwa katika Mkutano na Ujumbe kutoka Oman uliofika Zanzibar kwa maandalizi ya Mkutano wa Kimataifa wa Historia ya Uislam na Utamaduni wake baina ya Nchi hizi mbili.mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa mkutano Chuo Kikuu cha Taifa Kampasi ya Majestic Zanzibar.
![]() |
Jeneza la bibi likielekea msikiti kwa ajili ya kusaliwa |
![]() |
Mtangazaji Hassan Bond, Fid Q, Diamond Platnumz na Ruge Mutahaba wakiwa msibani nyumbani kwamarehemu bi Kidude, Zanzibar |
![]() |
Msanii Fid Q, Baraka cousin ya Marehemu Bi Kidude na Hassan Bond Mussa (FID Q ndo alikuwa msanii wa kwanza mkubwa kufika msibani kwa bibi) |
![]() |
Ruge mutahaba, Babu Tale and Guru. .......msibani kwa Bi Kidude |
![]() |
Guru G na Mh Bhaa mazikoni |
![]() |
Hassan na Fid Q wakiwa katika picha ya pamoja na familia ya Marehemu Bi Kidude |
![]() |
Sehemu ya umati wa Watu waliofika msibani Endelea kuwa nasi kwa tukio zima la maziko ya Bibi yetu |
BiKidude akipinga ngoma aina ya Uyango katika matamasha yanayofanyika Zanzibar katika viwanja vya Ngomekongwe
Mwaka 2005 huko Gateshead, Newcastle nchini Uingereza,Bi.Kidude alipokea tuzo yenye heshima kutoka World Music Expo (WOMEX) kwa mchango wake katika muziki na utamaduni wa Zanzibar. Katika kinyang’anyiro hicho aliwashinda wanamuziki mahiri kama Peter Gabriel, Miriam Makeba na wengineo. Bi.Kidude anasema hawezi kuacha kuimba mpaka siku atakapoiaga dunia kwani akiimba anajihisi kuwa binti wa miaka 14!Mwaka jana, kampuni ya nchini Uingereza iitwayo ScreenStation kwa kushirikiana na Busara Promotions walitoa documentary iitwayo “As Old As My Tongue-The Myth and Life of Bi.Kidude” inayoelezea historia nzima ya maisha yake. Unaweza kuona dakika kama saba hivi za documentary hiyo hapa chini.Anasema yeye anakunywa na pia anavuta,lakini zaidi ya yote anaweza kuimba bila hata kutumia spika ya mdomo yaani microphone.
Picha hii ni kwa hisani ya Marcel Mutsaers aliyompiga Bi.Kidude wakati wa Tamasha lijulikanalo kama Festival Mundial kule Tilburg-Uholanzi mwezi June mwaka 2006.
Umri wake halisi haujulikani. Kinachojulikana ni kwamba ana umri zaidi ya miaka 90 na hivi sasa sio ajabu akawa ameshafikisha umri wa miaka 100! Amekuwa muimbaji tangu miaka ya 1920 akiwa ni mfuasi wa Sitti Bin Saad mmojawapo wa waimbaji wa mwanzo kabisa wa taarabu visiwani Zanzibar.
Hivi leo anatambulika na kuheshimika kama malikia wa taarabu na mambo ya unyago asiye na mpinzani. Alizaliwa katika kijiji cha Mfagimaringo katika familia ya watoto saba. Jina alilopewa na wazazi wake alipozaliwa ni Fatuma Binti Baraka kabla jina maarufu la Bi.Kidude halijashika baadaye alipoanza kuwa maarufu katika uimbaji.Wazazi wake walikuwa ni wafanyabiashara ya kuuza nazi enzi hizo za Zanzibar iliyokuwa chini ya utawala wa wakoloni.
Katika mahojiano mbalimbali aliyofanya na vyombo tofauti tofauti vya habari ulimwenguni Bi.Kidude anasema alianza kuimba akiwa na umri mdogo wa miaka 10. Anasema uimbaji alijifunza kutoka kwa Sitti binti Saad tena kwa kujificha nje ya nyumba na kumsikiliza Sitti binti Saad akiwaimbia wageni ambao mara nyingi walikuwa wakipelekwa pale na yeye Bi.Kidude.
Akiwa na umri wa miaka 13 tu hakuwa na jinsi bali kukimbilia Tanzania bara(Tanganyika enzi hizo) ili kuepuka kuozeshwa kwa nguvu. Akiwa Tanzania bara alizunguka kila kona ya nchi akiwa muimbaji katika makundi mbalimbali ya muziki wa taarabu likiwemo lile maarufu la Egyptian Musical Taarab. Baadaye alihamia nchini Misri kwa kifupi kabla hajarejea kisiwani Zanzibar mahali ambapo anaishi mpaka hivi leo.
Mbali na uimbaji Bi.Kidude pia ni mfanyabiashara.Anauza “wanja” na “hina” ambazo anazitengeneza mwenyewe. Pia ni mtaalamu wa dawa za mitishamba lakini zaidi ya yote yeye ni Mwalimu wa “unyago” ambapo anacho chuo chake mwenyewe huku akijivunia rekodi kwamba katika wanafunzi wake wote hakuna ambaye ameshawahi kupewa talaka na mumewe. Pengine hii ndio sababu mwaka 2004 ulipozuka umbea kwamba Bi.Kidude amefariki dunia wakati alipokuwa katika ziara ndefu ya kimuziki Ulaya na Mashariki ya mbali, kila mtu kisiwani Zanzibar alishikwa na butwaa na majonzi! Kwa bahati nzuri habari za “kifo” chake zilikuwa ni uzushi tu.
Waumini wa Dini ya Kiislam wakisoma hitma kumuombea Marehemu Haji Mohammed, katika msikiti wa Nambar Muembetanga asubuhi ya leo kabla ya kusaliwa maiti , ikiongozwa na Shekh. Nurdini.
Waumini wa dini ya Kiislam wakiusalia mwili wa marehemu Haji Mohammed Omar katika Msikiti Nambari muembetanga,
Wananchi wakiwa katika mstari wakati wa kubeba jeneza la marehemu Haji Mohammed, wakati likiwa katika maeneo ya michezani kwa ajili ya kwenda makaburi katika kijiji cha Shakani kwa ajili yamaziko.
Marehemu Haji Mohammed Kirembwe cha Siti Bint Saad, wakati wa uhai wake akiimba na kikundi cha gusagusa .
Mtoto wa Kwanza wa Marehemu Haji Mohammed, akishindikizwa na nduga na jamaa waliofika katika bandari ya Zanzibar kupokea mwili huo leo jioni ukitokea Jijini Dar-es- Salaam,
Marehemu Haji Mohammed anatarajiwa kuzikwa kesho saa 4.00 asubuhi na sala ya maiti itafanyika Mskiti Nambari Muembetanga.
Marehemu alikuwa Msanii kwa muda mrefu na Kikundi chake cha kwanza kujiunga kilikuwa Kikundi cha Taraab cha Malindi, akiwa ni mpiga kinanda na mtunzi na muimbaji katika kikundi hicho.Na hatimae kuanzisha kikundi kilichojulikana kwa Jina la East African Melody.
Akiwa Mkurugenzi wa Kikundi hicho na alikihamishia makazi ya Kikundi hicho katika Jiji la Dar-es-Salaam na kutoa burudani kwa Wapenzi wao.
Pia alianzisha Kikundi cha Gusagusa ambacho kilikuwa kikipiga nyimbo za zamani katika ukumbi wa DDC Kariakoo siku za week end hutowa burudani hiyo.
Wananchi wakipokea jeneza la Marehemu Haji Mohammed katika bandari ya Zanzibar leo jioni.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe mama Salma Kikwete wakipokea maua mara baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi tayari kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Nne wa Kenya Mhe Uhuru Muigai Kenyatta na Naibu Rais wake Mhe William Ruto katika uwanja wa michezo wa Kasarani leo April 9, 2013
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe mama Salma Kikwete wakilakiwa kwa heshima zote baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi tayari kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Nne wa Kenya Mhe Uhuru Muigai Kenyatta na Naibu Rais wake Mhe William Ruto katika uwanja wa michezo wa Kasarani leo April 9, 2013
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini kitabu cha wageni baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi tayari kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Nne wa Kenya Mhe Uhuru Muigai Kenyatta na Naibu Rais wake Mhe William Ruto katika uwanja wa michezo wa Kasarani kesho April 9, 2013. Mama Salma Kikwete na Balozi wa Tanzania nchini Kenya Dkt Batilda Burian wamesimama pembeni na wenyeji wao
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe mama Salma Kikwete wakilakiwa kwa heshima zote baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi tayari kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Nne wa Kenya Mhe Uhuru Muigai Kenyatta na Naibu Rais wake Mhe William Ruto katika uwanja wa michezo wa Kasarani leo April 9, 2013
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini kitabu cha wageni baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi tayari kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Nne wa Kenya Mhe Uhuru Muigai Kenyatta na Naibu Rais wake Mhe William Ruto katika uwanja wa michezo wa Kasarani kesho April 9, 2013. Mama Salma Kikwete na Balozi wa Tanzania nchini Kenya Dkt Batilda Burian wamesimama pembeni na wenyeji wao
PICHA NA IKULU
Maandamano ya raia wa Rwanda wanaoishi nchini Tanzania pamoja na wanafunzi wa shule mbalimbali za jijini Dar es Salaam wakijipanga katika ukumbi wa New World Cinema tayari kuanza maandamano ya kuadhimisha miaka 19 ya mauaji ya Kimbari ya Rwanda kuelekea ukumbi wa mikutano wa Mlimani City. (Picha na Zainul Mzige wa Mo Blog)
Picha juu na chini Umati wa maandamano yakielekea katika ukumbi huo.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo Dr. Salim Ahmed Salim njiani kuelekea kwenye ukumbi wa mikutano Mlimani City.
Mgeni rasmi Dr. Salim Ahmed Salim (wa tatu kulia) akiwa na balozi wa Rwanda nchini Tanzania Mh. Benjamin Ruganganzi (wa tatu kushoto) wakisubiri kupokea maandamo ya maadhimisho ya miaka 19 ya mauaji ya Kimbari ya Rwanda katika viwanja vya Mlimani City jijini Dar.
Dr. Salim Ahmed Salim akipokea rasmi maandamano hayo.
Mgeni rasmi katika maadhimisho ya 19 ya mauaji ya Kimbari ya Rwanda Dr. Salim Ahmed Salim akizungumzia kumbukumbu ya mauaji hayo ambapo amesema historia ipo kwa ajili yetu sote kujikumbusha yaliyopita ili tuweze kupanga yajayo na kuwa mauaji ya Kimbari ni mzigo wetu sote na tunapaswa kujifunza kutambua alama za watu wa jamii moja kuanza kuhitilafiana na kutafuta namna ya kuzitatua kabla hazijaleta athari.
Na pia alichukua fursa hiyo na kunukuu maneno yaliyowahi kusemwa na Baba wa Taifa wa Tanzania Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere " Ukweli ni kwamba kila sehemu ya Afrika ina ihitaji Afrika kwa pamoja na Afrika kama bara inahitaji kila sehemu ya bara la Afrika".
MC katika maadhimisho ya miaka 19 ya mauaji ya Kimbari Usia Nkhoma akirekebisha kipaza sauti wakati mgeni rasmi akizungumza wakati wa maashimisho hayo.
Wageni waalikwa wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi (hayupo pichani) wakati wa kumbukumbu ya maashimisho ya miaka 19 ya mauaji ya Kimbari Rwanda.
Kaimu Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Bw. Jama Gulaid ambaye pia ni Mkurugenzi Mkazi wa UNICEF akizungumza wakati maadhimisho ya miaka 19 ya mauaji ya Kimbari nchini Rwanda yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City ambapo amesema dunia nzima itakuwa na siku maalum ya kukumbuka wahanga wa mauaji ya Kimbari ya Rwanda kwa heshima ambayo ni alama ya kukumbuka athari za mauaji hayo na kuwa pamoja na walionusurika na kwa namna nyingine ni alama msingi ya kupongeza hatua zilizochukuliwa na jamii ya Wanarwanda kuungana pamoja.
Katika mazungumzo yake alinukuu maneno yaliyozungumzwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon " Katika maasdhimisho ya 19 ya mauaji ya Rwanda tunawakumbuka watu zaidi ya 800,000 wasio na hatia ambao walipoteza maisha yao na tutanendelea kuwaheshimu walionusurika na tutaendelea kuwa nao pamoja na kukemea wale wote waliohusika na tukio hilo, na kuwapongeza waliojitokeza kuzuia mauaji hayo yasiendelee".
Balozi wa Rwanda nchini Tanzania Mh. Benjamin Ruganganzi akitoa salamu zake kwa wageni waalikwa pamoja na watu waliohudhuria maadhimisho ya 19 ya mauaji ya Kimbari ya Rwanda na kuhakikisha kuwa wananchi wa Rwanda wataendelea kudumisha uhusiano na ushirikiano pamoja na nchini zingine za Afrika Mashariki ili kuhakikisha tukio kama hilo halitajirudia tena.
Sehemu ya wageni waalikwa wakiwemo mabalozi mbalimbali wakimsikiliza Balozi wa Rwanda nchini (hayupo pichani).
Msemaji wa Mahakama ya Umoja wa Mataifa ya Mauaji ya Rwanda (ICTR) Bw. Roland Ammousouga akitoa kauli yake wakati wa maadhimisho ya 19 ya mauaji ya Kimbari ya Rwanda ambapo amesema kwa miaka 19 iliyopita watu wanaweza wakajisifu kazi iliyofanywa na mahakama ya ICTR kwamba imetimiza kilio cha maelefu ya waathirika na kuwa imesaidia katika kuleta upatanishi na kuijenga upya Rwanda sambamba na kuhamasisha amani na ulinzi katika ukanda wa Afrika wa maziwa makuu, wakati haikufanikiwa kuwakamata wale wote waliohusisha na mauaji hayo kwa kutoa itumia Rwanda kuwatafuta wahusika 6 waiojulikana walipo ili waweze kukabiliana na kesi zinazowakabili kinachojionyesha hapa ni kwamba ICTR inaashiria kwamba mapambano dhidi ya mazingira ya wahusika wengine 3 hawawezi kukamatwa.
Umati wa watu waliofurika (chini) katika maadhimisho hayo wakiwemo wanafunzi wa shule ya sekondari Jitegemee (juu).
Mmoja wa viongozi wa Dini akiomba dua ya kuwarehemu walipoteza maisha katika mauaji ya Kimbari yaliyotokea nchini Rwanda.
Meza kuu ikiongozwa na mgeni rasmi Dr. Salim Ahmed Salim kuwasha mishumaa ikiwa ni ishara ya kuwakumbuka watu waliopoteza maisha wakati wa mauji ya Kimbari nchini Rwanda.
Kwa picha zaidi ingia hapa