Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

11 wafariki katika tamasha Morocco

-
Rehema Mwinyi.


Watu wasiopungua 11 wamefariki katika mji mkuu wa Morocco, Rabat, baada ya kukanyagana katika tamasha ya kimataifa ya muziki ya Mawazine.

Kulingana na waandishi habari, inadhaniwa kwamba watu wengine 40 walijeruhiwa baada ya uzio wa senyenge kuporomoka.

Tukio hilo lilifanyika usiku wa Jumamosi, wakati zaidi ya watu 70,000 walijaa pomoni katika uwanja wa michezo wa Hay Nahda, kumtizama mwanamuziki wa Morocco, Abdelaziz Stati.

Katika tamasha mwaka huu walioshiriki ni pamoja na Kylie Minogue, Khaled na Alicia Keyes.

Wadadisi wanasema kwamba tamasha hiyo ya wiki moja ya Mawazine ni kati ya mipango ya Morocco ya kuimarisha sifa nzuri za nchi hiyo ili taifa hilo lionekana ulimwenguni kwamba linakwenda sambamba na maendeleo ya kisasa.

Kulingana na maafisa wa polisi, wanawake watano, wanaume wanne, na watoto wawili, ndio waliofariki kati hali hiyo ya mkanyagano.

Leave a Reply