Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

Guantanamo yamkuna kichwa Obama

-
Rehema Mwinyi.


Rais Barack Obama anasema Marekani itatafuta njia muafaka za kuwadhibiti wafungwa hatari ambao wamezuiliwa kwenye kambi ya Guantanamo huku akisisitiza kwamba kuwepo kwa gereza hilo ni hatua isiyo na mwelekeo.

Lakini alikiri kwamba baadhi ya wafungwa hao bado ni tishio kwa usalama wa Marekani.

Alipendekeza kwamba baadhi ya wafungwa hao wanaweza kuhamishiwa kwenye magereza ya Marekani katika mfumo mpya wa sheria ambao utaiwezesha Marekani kufunga kambi ya Guantanamo ifikapo mwaka 2010.

Lakini bunge la Marekani limepinga ombi la fedha la Rais Obama kugharamia kufungwa kwa kambi hiyo.

Baadhi ya wabunge walielezea mashaka yao kuhusu kupelekwa kwa wafungwa hao nchini Marekani.

Makamu wa rais wa zamani, Dick Cheney, alimjibu Rais Obama huku akitetea vikali mikakati ya usalama ya rais wa zamani George Bush.

Rais Obama alisema serikali yake itatathmini kila kesi ya wafungwa 240 ambao bado wamezuiliwa Guantanamo na kisha kuamua hatua gani watakayochukua.

Alisema baadhi yao watafikishwa mbele ya mahakama za kiraia za Marekani, wale ambao wamekiuka sheria za kivita watafikishwa mbele ya tume ya kijeshi, kuna wale ambao walikuwa wameachiliwa huru na mahakama halafu waliobaki huenda wakahamishwa hadi nchi nyingine.

Leave a Reply