Rais Horst Köhler wa Ujerumani amesema kwamba Ujerumani imestawi kuwa nchi yenye uwazi na ya kimataifa katika historia yake ya miaka 60.
Rais Köhler amesema hayo mjini Berlin leo katika maadhimisho ya miaka 60 tokea kuundwa kwa shirikisho la Jamhuri ya Ujermani.
Amesema katika miaka 60 iliyopita Ujerumani limekuwa taifa lenye uwazi kwa dunia .Ameeleza kuwa Ujerumani imeshiriki katika juhudi za kuunda jumuiya za Umoja wa Ulaya na pia imeshsiriki katika kuweka malengo ya kisiasa ya jumuiya hizo.
Amesema Ujerumani imekabiliana na uhalifu uliotendwa na mafashisti na imefikia maridhiano na taifa la kiyahudi.
Rais Köhler ameeleza kuwa wajerumani wamejifunza kutokana na historia na ndiyo sababu kwamba wakati wote itapinga maovu ya chuki dhidi ya wayahudi,ubaguzi ,na chuki dhidi ya wageni.
Juu ya katiba ya Ujerumani iliyoweka msingi wa demokrasia nchini, rais Köhler amesema kuwa hati hiyo ni mwenge wa wa uhuru.Ameeleza kuwa katiba hiyo iliwapa wajerumani wa upande wa mashariki, matumaini.
Kuhusu medani ya kimataifa rais Köhler amesema kuwa Ujerumani imeshirikiana na nchi inayofungamana nazo katika kuletekeleza majukumu ya ya kimataifa.
Imesaidia katika kutatua migogoro mbalimbali duniani na kwamba Ujerumani imetoa mchango wake katika kulinda amani na haki za binadamu duniani.