Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

Mwanajeshi Dar afa ajalini

-
Rehema Mwinyi.


Askari mmoja wa Jeshi la Wananchi Tanzania, JWTZ, mwenye cheo cha Kapteni, aliyetambuliwa kwa jina la Robert Makongoro, 31, amefariki dunia papo hapo baada ya gari alilokuwa anaendesha kugongwa na gari lingine katika barabara ya Sam Nujoma Jijini Dar es Salaam.

Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Mark Kalunguyeye amesema ajali hiyo ilitokea jana mishale ya saa 10:30 jioni eneo la Super Star kwenye makutano ya barabara inayotokea Sinza Makaburini.

Amesema mwanajeshi huyo aligongwa na gari lenye namba za usajili T 792 ARX aina ya Suzuki, iliyokuwa ikiendeshwa na Joanes Kacheche, 41, akitokea Mwenge kuelekea maeneo ya Ubungo.

Kamanda Kalunguyeye amesema gari la Joanes lilipofika maeneo hayo, lilivaana na la mwanajeshi lenye namba za usajili T 715 AZX aina ya Toyota Carina lililokuwa likitokea Sinza Makaburini.

Amesema gari la mwanajeshi liligongwa upande wa dereva.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Lugalo.

Kamanda amesema Polisi wanamshikilia dereva Joanes kwa uchunguzi zaidi na endapo atabainika ana makosa hatua zaidi za kisheria zitachukuliwa.

Leave a Reply