Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

Obama aanza ziara mashariki ya kati

-
Rehema Mwinyi.


Rais wa Marekani Barack Obama amewasili nchini Saudi Arabia katika mwanzo wa ziara yake mashariki ya kati, inayolenga kuimarisha uhusiano baina ya Marekani na nchi za Kiislamu.

Bwana Obama alitarajiwa kuwa mjini Riyadh kwa muda wa saa nne kabla ya kuelekea nchini Misri, ambako atatoa hotuba muhimu mjini Cairo.

Anasema anataka kuanzisha mdahalo na waislamu , kuondosha hali ya kutoelewana na kufufua mashauriano ya amani ya mashariki ya kati.

Hii ni ziara ya kwanza ya rais Obama katika eneo hilo, mbali na kupitia Iraq muda mfupi mwezi Aprili.

Saudi Arabia ndiyo inayodhamini mpango wa kipekee wa amani kwa uhusiano kati ya nchi za kiarabu na Israel, ingawa kwa sasa hivi mazungumzo yamekwama.

Misri inahusika sana katika matatizo ya WaPalestina , kwa kuwa msuluhishi kati ya Israel na kundi la Hamas kwenye ukanda wa Gaza.

Bwana Obama alipata mapokezi ya taadhima mjini Riyadh kabla ya kufanya mazungumzo na mfalme Abdulla.

Bwana Obama hakutarajiwa kutoa taarifa yoyote mjini Riyadh, lakini lakini siku ya Alhamisi anatarajiwa kutoa hotuba katika chuo kikuu cha Cairo nchini Misri, ambayo mwandishi wa BBC anasema ni mojawapo ya hotuba muhimu sna za rais Obama kama rais wa Marekani.

Safari ya rais Obama mashariki ya kati haijumuishi Israel, lakini muda mfupi kabla ya kuondoka kuelekea Saudi Arabia alikutana na waziri wa ulinzi wa Israel Ehud Barak mjini Washington.

Akizungumza na BBC kabla ya ziara hiyo, rais Obama alisema anaamini Marekani '' itaweza kufufua tena mashauriano ya kufana'' kati ya Israel na Palestina.

Alisema ziara hiyo inakusudiwa kutoa fursa kwa Marekani na nchi za kiislamu kusikilizana zaidi.

Ziara hiyo ya mashariki ya kati imekuja huku kukiwa na taarifa zilizodaiwa kutoka kwa viongozi wa Al Qaeda, ukiwemo ujumbe ulionakiliwa kutoka kiongozi mkuu wa kundi hilo Osama Bin Laden.

Kwenye kanda hiyo iliyoonyeshwa na Televisheni ya Ki-Arabu ya al-Jazeera , Bin Laden anamlamu rais Obama na mtangulizi wake George W Bush kwa kukuza chuki dhidi ya Marekani.

Leave a Reply