Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

Mwanamke Amuua Mpenzi Wake Kwa Kumkalia

-
Rehema Mwinyi.


Mwanamke mmoja nchini Marekani mwenye uzito wa kilo 136 amepandishwa kizimbani kwa kosa la kumuua mpenzi wake aliyezaa naye watoto watatu kwa kumkalia hadi alipofariki.

Taarifa ya polisi wa Cleveland nchini Marekani ilisema kuwa mwanamke huyo aliyejulikana kwa jina la Mia Landigham na mpenzi wake Mikal Middleston-Bey walikuwa kwenye mzozo wa ndani ya nyumba mnamo mwezi wa nane mwaka jana.

Taarifa zaidi zilisema kuwa mzozo huo ulikuwa mkubwa sana na kupelekea Mia aliyekuwa na uzito wa kilo 136 wakati huo kurushiana makonde na Mikal.

Mia alifanikiwa kumwangusha chini Mikal ambaye alikuwa mwembamba sana mwenye mwenye uzito wa kilo 54.4 tu. Mia alimkalia Mikal kwa dakika kadhaa aliponyanyuka Mikal alikuwa hapumui tena na alifariki dakika chache baadae.

Kufuatia tukio Mia alipandishwa mahakamani juzi jumatano na kuhukumiwa kwenda jela miaka mitatu na kufanya kazi za kuitumikia jamii kwa masaa 100.

Mia alikiri kosa lake la kumuua bila kukusudia mpenzi wake huyo ambaye amezaa naye watoto watatu. Mia pia aliiomba radhi familia ya marehemu kwa kusababisha kifo chake.

Wakili wa Mia aliiambia mahakama kuwa uhusiano wa Mia na Mikal ulikuwa na historia ya migogoro mingi na alimuomba jaji ampunguzie adhabu Mia kwa kuwa hana historia ya makosa ya jinai.

"Napenda kusema kuwa naomba radhi na nimehuzishwa na yaliyotokea natamani ningekuwa na uwezo wa kuurudisha uhai wake", alisema Mia.

source nifahamishe.com

Leave a Reply