Uongozi mtamu lakini mgumu
.So sad!! i am so sure kuwa Rais kikwete yupo katika wakati mgumu sana,pale watu uliowaamini wanaposhindwa kuwa waadilifu,
Mungu muongoze aweze kuivusha vyema Tanzania,
sometime we need to think positive and its negative . Uadilifu ni kitu kigumu sana tofauti na watu wanavyofikiria.kazi nzuri kwa waliofanikisha kujiuzulu kwa mawaziri..ila siku zote lazima tuelewe kwamba kwenye mwema hakosekani mbaya kuna wanaotaka changes kwa seek of the country and its people, ila ndani yake pia kuna wale wanaomendea kitu flani..so kazi imekamilika tunachotegemea ni mabadiliko ya kweli,tuache uchochezi utakaopelekea kuvunjika kwa amani.watanzania waungane kuleta mabadiliko lakini ni lazima kufanya maamuzi sahihi.tusieneze or kuandika upupu tu ambao mwisho wa siku utatuwasha wenyewe..Kweli kuna freedom of speech kuna wanaosema #mawaziri wameachia ngazi @ next Raisi!..unae chochea hivi jee umejiamini??lazima tukumbuke kuwa wapiganapo fahari wawili ziumiazo ni nyasi..so kabla ya kukurupuka lazima tufikirie wananchi wa kawaida ambao kila cku ndio waathirika wakubwa..Tuungane pamoja kuleta mabadiliko katika nchii yetu.lakini lazima tuelewe mabadiliko hayo hayaji kama ndoto ukilala utaota na kushtuka lazima tujipange.same na waliowezesha kujiuzulu kwa mawaziri naamini hawakuota tu na kukurupuka tu lazima wamejipanga wamejiamini na kushirikiana.Tuendelee kuwa na sauti mojà,kudumisha Amani na utulivu iliopo katika nchi yetu.Mungu ibariki Tanzania Mungu wabariki watanzani.
[ Read More ]
Mawaziri nane wajiuzulu.Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo, Waziri wa Viwanda na Biashara, Cyril Chami, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, Waziri wa Uchukuzi, Omar Nundu, Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige, Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi),George Mkuchika, Waziri wa Kilimo Chakula na Ushurika Jumanne Maghembe na Waziri wa Afya, Dk. Haji Mponda
[ Read More ]
Brigedia Jenerali, Adam clement Mwakanjuki wakati wa uhai wake akisalimiana na Waziri Mkuu Mizengo Pinda katika hospitali ya Lugalo Jijini Dar es Salaam.
Aliyekuwa Waziri wa zamani wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Brigedia Jenerali, Adam clement Mwakanjuki amefariki dunia katika hospitali ya Lugalo Jijini Dar es Salaam. Marehemu Mwakanjuki amefariki duani jana Alaasiri baada ya kuugua kwa mfupi. Hata hivyo haikuelezwa alikuwa akisumbuliwa na kitu gani lakini alifikishwa hospitalini mapema wiki hii.
Brigedia Jenerali Mwakanjuki ni miongoni miongoni mwa wanasiasa wakongwe hapa nchini ambaye alianza kazi ya siasa kabla ya mapinduzi ya Zanzibar ya januari 12, 1964 katika chama cha Afro shirazi (ASP) na baadae Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Marehemu Mwakanjuki aliwahi kuwa waziri wa kilimo na mifugo, waziri wan chi ofisi ya rais katiba na utawala bora, waziri wa nchi ofisi ya rais tawala za miko na vikosi vya SMZ na mumbe wa baraza la wawakilishi kwa muda mrefu.
Kwa mujibu wa familia ya marehemu wamesema kwamba taarifa ya mazishi itatolewa leo baada ya kukutana wanafamilia hiyo visiwani Zanzibar.
“Ni kweli Mjomba amefariki hivi punde dare s salaam na mipango ya mazishi itapangwa baada ya kikao cha familia yetu” alisema Vicky Mwakanjuki mtoto wa Dada wa Marehemu.
Wakati wa uhai wake Marehemu Mwakanjuki alikuwa waziri mwandamizi katika serikali ya Zanzibar katika wizara mbali mbali pamoja na kuwa mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya CCM (NEC).
Tangu mwaka 2007 Marehemu Mwakanjuki hakuonekana katika harakati za siasa baada ya kupata ajali mbaya akitokea Dodoma kwenda Dar es Salaam katika eneo la Morogoro ambayo ilisababisha kuvunjika sehemu zake za viungo.
Licha ya juhudi za kupatiwa matibabu ndani na nje ya nchi lakini hakuweza kurudi katika hali yake ya kawaida ambapo wakati wa tukio inatokezea alikuwa akiendesha gari lake mwenyewe pamoja na mwanawe.
Mwakanjuki pia alikuwa afisa mwandamizi katika jeshi la wananchi wa Tanzania na kufikia cheo cha Brigedia Jenerali na ameongoza brigedi mbali mbali ikiwemo pia kuwa miongoni mwa waanzilishi wa jeshi la kujenga taifa JKT.
Hadi kufikia mwaka 2010 Marehemu alikuwa waziri wa mawasiliano a uchukuzi Zanzibar pamoja na kuwa mjumbe wa NEC hadi mauti yanamkuta.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(kulia) akizungumza na Viongozi wa Wilaya ya Wete na Micheweni Pemba, katika mkutano wa majumuisho ya ziara aliyoifanya katika Wilaya hizo zilizo katika Mkoa wa Kaskazini Pemba, iliyomalizika jana kwa mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete,(kushoto) katibu Mkuu Kiongozi Dk.Abdulhamid Yahaya Mzee na Waziri wa Bishara,Viwanda na Masoko Nassor Ahmed Mazrui.
Baadhi ya Viongozi wa Wilaya ya Wete na Micheweni Pemba,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, alipokuwa akizungumza na Viongozi hao katika mkutano wa majumuisho ya ziara aliyoifanya katika Wilaya hizo zilizo katika Mkoa wa Kaskazini Pemba, iliyomalizika jana kwa mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete
Wabunge wa Afrika Mashariki, Makongoro Nyerere na Shy-Rose Bhanji wakipongezana muda mfupi baada ya kuchaguliwa bungeni mjini Dodoma.
*****
[ Read More ]
*****
Kitendawili cha nani ataiwakilisha Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki kimetenguliwa jana baada ya Wabunge wa Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania kuwateua wagombea hao.
Bunge lilipiga kura jana kuwachagua wabunge tisa kutoka Chama tawala CCM na kambi ya Vyama vya Upinzani.
Katika uchaguzi huo CCM iliyokuwa na wagombea 24 walioshinda ni pamoja na Charles Makongoro Nyerere, , Shy-Rose Bhanji, Adam Kimbisa, Abdullah Ali Hassan Mwinyi, Bernard Murunya,Janet Mmari na Angela Kizigha
Akitangaza matokeo hayo Msimamizi wa Uchaguzi huo ambaye pia ni Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashilillah alisema Bhanji alishika nafasi ya pili katika kundi la kwanza (wanawake) akipata kura 120 akitanguliwa na Angela Kizigha aliyepata kura 166. Wote ni kutoka CCM.
Wengine waliogombea katika kundi hilo ni Rose Mwalusamba wa CUF ambaye licha ya kujitoa alipata kura saba, Fancy Haji Nkuhi (57), Dk Goodbertha Kinyondo (32), Janet Mmari (119) na Janet Mbene (87).
Katika kundi la pili kutoka Zanzibar, Abdullah Ali Hassan Mwinyi alirejea tena katika bunge hilo baada ya kuongoza kwa kupata kura 227 akifuatiwa na Mariam Ussi Yahya (91).
Katika kundi hilo, Septuu Nassor Mohammed na Dk Said Gharib Billal walishindwa kurejea katika bunge hilo baada ya kuambulia kura 74 na 88 mtawalia. Wengine walioshindwa ni Dk Ahmada Hamid Khatibu (36), Dk Haji Mwita Haji (11), Khamisi Jabir Makame (6) na Zubeir Ali Maulid (39).
Katika kundi la vyama vya upinzani, mbali ya Dk Masha wengine walioshindwa ni Anthony Komu wa Chadema (93), Juju Danda wa NCCR-Mageuzi (23), Micah Mrindoko wa TLP (66) na Mwaiseje Polisya wa NCCR-Mageuzi (42).
Katika kundi la nne la Tanzania Bara, Kimbisa ambaye aliwahi kuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam aliongoza kwa kupata kura 210 akifuatiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa zamani wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Bernard Murunya aliyepata kura 135 na Makongoro kura 123.
Walioshindwa katika kundi hilo ni Dk Edmund Mndolwa (42), Elibariki Kingu (31), Dk Evans Rwaikiza (78), Mrisho Gambo (75) na Siraju Kaboyonga (38) wote kutoka CCM na John Lifa Chipaka wa Tadea (8).
Wengine waliogombea katika kundi hilo ni Rose Mwalusamba wa CUF ambaye licha ya kujitoa alipata kura saba, Fancy Haji Nkuhi (57), Dk Goodbertha Kinyondo (32), Janet Mmari (119) na Janet Mbene (87).
Katika kundi la pili kutoka Zanzibar, Abdullah Ali Hassan Mwinyi alirejea tena katika bunge hilo baada ya kuongoza kwa kupata kura 227 akifuatiwa na Mariam Ussi Yahya (91).
Katika kundi hilo, Septuu Nassor Mohammed na Dk Said Gharib Billal walishindwa kurejea katika bunge hilo baada ya kuambulia kura 74 na 88 mtawalia. Wengine walioshindwa ni Dk Ahmada Hamid Khatibu (36), Dk Haji Mwita Haji (11), Khamisi Jabir Makame (6) na Zubeir Ali Maulid (39).
Katika kundi la vyama vya upinzani, mbali ya Dk Masha wengine walioshindwa ni Anthony Komu wa Chadema (93), Juju Danda wa NCCR-Mageuzi (23), Micah Mrindoko wa TLP (66) na Mwaiseje Polisya wa NCCR-Mageuzi (42).
Katika kundi la nne la Tanzania Bara, Kimbisa ambaye aliwahi kuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam aliongoza kwa kupata kura 210 akifuatiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa zamani wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Bernard Murunya aliyepata kura 135 na Makongoro kura 123.
Walioshindwa katika kundi hilo ni Dk Edmund Mndolwa (42), Elibariki Kingu (31), Dk Evans Rwaikiza (78), Mrisho Gambo (75) na Siraju Kaboyonga (38) wote kutoka CCM na John Lifa Chipaka wa Tadea (8).
Twaha Taslima wa Cuf na Nderakindo Kessy wa NCCR-Mageuzi walichaguliwa kwa upande wa vyama vya upinzani. Taslima alipata kura 175 na Kessy kura 113.
Kabla ya uchaguzi wa jana, upinzani ulikuwa na nafasi moja katika bunge hilo ambayo ilikuwa inashikiliwa na Dk Fortunatus Masha wa UDP ambaye alianguka baada ya kupata kura 58.
Kabla ya uchaguzi wa jana, upinzani ulikuwa na nafasi moja katika bunge hilo ambayo ilikuwa inashikiliwa na Dk Fortunatus Masha wa UDP ambaye alianguka baada ya kupata kura 58.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ametoa wito kwa wananchi wa Zanzibar hasa wakulima wa zao la karafuu kutoweka fedha zao majumbani na badala yake waweke kwenye mabenki yaliopo nchini kwa ajili ya usalama wa fedha zao.
Dk. Shein aliyasema hayo mara baada ya kutoa zawadi ya vyeti maalum kwa wanunuzi bora wazalendo wa zao la karafuu msimu huu wa mwaka 2011-2012, hafla iliyofanyika huko katika uwanja wa Jamuhuri, Wete Pemba.
Katika maelezo yake, Dk. Shein alisema kuwa ni vyema wakulima baada ya kuuza karafuu zao waweke fedha zao benki badala ya majumbani kwani inasemekana fedha nyingi walizozipata wananchi katika kuuza karafuu wameiweka majumbani.
Alisema kuwa ni jambo la busara kuweka fedha zao katika benki yoyote wanayoitaka wenyewe ikiwemo benki yao ya PBZ na hata benki nyenginezo kwa ajili ya usalama wa fedha zao na hata wao wenyewe.
Amesema kuwa bilioni 71 zimetumika katika kununua karafuu Unguja na Pemba, hali ambayo imewapelekea wananchi walio wengi kufaidika na fedha hizo kutokana na kuuza karafuu zao katika vituo vya ZSTC. Alisema kuwa sheria ya karafuu itatengenezwa upya ili iweze kukidhi haja pamoja na mazingira yaliopo hivi sasa.
Rais Dk. Shein aliwapongeza wananchi kwa kushirikiana na serikali katika kuhakikisha zao hilo wanawauzia Shirika la ZSTC na kueleza kuwa lengo la Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, ni kuwa na bajeti itakayokuwa haina tegemezi kutoka upande wowote.
Aidha, Dk. Shein alilitaka Shirika la ZSTC kuhakikisha linatafuta mbinu za kuviimarisha vituo vya kununulia karafuu kwa kuhakikisha vinatoa huduma muhimu zikiwemo vyoo, samani, maji, umeme na huduma nyenginezo.
Pamoja na hayo, Dk. Shein aliwaeleza wananchi na wakulima wa zao la karafuu kuwa Serikali itafanya juhudi ya kuhakikisha kuwa barabara kadhaa hasa zile zinazoelekea katika maeneo yanayozalisha karafuu kwa wingi zinatengezwa japo kwa kiwango cha kifusi ili iwe rahisi kusafirisha zao hilo wakati wa mvua na hata wa jua.
Dk. Shein alisema kuwa serikali itaanzisha mfuko wa kuendeleza zao la karafuu na kuupitia upya utaratibu wa kuwapa fidia wananchi pamoja na kuhakikisha kwwamba mapungufu yote yaliokuwepo kabla ya kusita utaratibu huo yanafayiwa kazi.
Pia, Dk. Shein aliupongeza Mkoa wa Kaskazini Pemba kwa kuongeza idadi kubwa ya zao la karafuu ambalo zimenunuliwa na ZSTC mwaka huu na kufikia tani 2285 ambapo mwaka jana karafuu zilizonunuliwa katika Mkoa huo zilikuwa tani 25 tu.
Dk. Shein alimpongeza Waziri ya Biashara pamoja na watendaji wake kwa hatua iliyofikiwa ya mafanikio pamoja na kupongeza Kikosi kazi maalum, vikosi vya ulinzi na usalama pamoja na wananchi wenyewe ambao pia walichangia kupambana na magendo.
Sambamba na hayo, Dk. Shein alieleza kuwa mbali ya zao la karafuu pia, sekta ya utalii nayo imefanikiwa kutokana na wageni wegi kuja kutembelea Zanzibar na kusisitiza kuwa mikopo iliyokopeshwa Zanzibar uwezo wa kuilipa yote upo na Zanzibar hivi sasa inakopesheka na hakuna aliyepata hasara huku serikali ikiwa imepata fedha ambazo zitatumika kwa ajili ya kuimarisha maendeleo nchini.
Wauzaji waliopewa vyeti hivyo maalum ni kutokana na kuuza zao hilo kwa ZSTC ni Bwana Hamad Said Hamad,Said Ali Juma, Hussein Khamis Jabu na Mohammed Issa Salim ambapo Mkoa Bora ni Mkoa wa Kusini Pemba na Wilaya Bora ni Wilaya ya Wete.
Na kwa upande wa Shehia, Shehia bora ya kwanza ni Shehia ya Selem, ikifuatiwa na Shehia ya Finya, Mtambile na Ziwani.
Wakati huo huo, Dk. Shein ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya CCM Taifa aliweka jiwe la msingi Tawi la CCM Kinyasini na kuwataka wana CCM kujitolea kuimarisha kazi za chama ikiwa ni pamoja na kuchangia ujenzi wa Matawi.
Aidha, Dk.Shein aliwasihi wana CCM kujua kwamba Wazanzibari wote ni wamoja hivyo itikadi za vyama zisiwagombanishe jambo la muhimu ni kuelewa kuwa Serikali ni moja lakini kila mmoja anachama chake na kusisitiza kuwa katika serikali hamna upinzani na kuwataka Wana CCM kutobweteka na badala yake waendelee kukimarisha chama hicho.
Pia, aliweka jiwe la msingi katika Afisi ya la CCM Jimbo la Tumbe na kupata maelezo juu ya ujenzi wa tawi hilo ambalo aliahidi kuunga mkono kumalizia ujenzi wake ambapo katika ujenzi wa Tawi la Kinyasini, Dk. Shein aliahidi kutoa msaada wake kwa kuliezeka tawi hilo pamoja na kutia madirisha na mlango wa nyuma wa mbele na kutia rangi
nilijiskia furaha na bado najiskia vizuri to be one in million of students ambao nao wangependa
watokee kwenye gazeti hii.wapo watakao ona its just a simple thing but for me its Big, na anyone atakae hisi ivyo basi ujue huyo ni hater ambao hana nafasi kwenye maisha yetu.kutokana na ndoto zangu za wapi nataka niwe.so yes i did it baby. kwasababu "hata mbuyu nao ulianza kama mchicha,so who knows?may be this is the beginning? nnachoweza kusema ni kuwa usikae chini kutegema mungu akutendee miujiza kumbuka kuwa ilikua zamani enzi za mitume tu.so you have to go out there and do something remarkable.
think big,dream big.
in Allah i trust.
Kuna wanaokupenda na kukubali na kudhihirisha upendo wao wa dhati kwako ukiwa bado hai.Pia kuna wanaokupe na kukubali.ila wanashindwa kuzihirisha upendo wao kwako.hadi pale utakapo kufa..lakini pia kuna wanaokuchukia ila wanajifanya wanakupenda ukiwepo bado hai ila ndio maadui zako wakubwa! Binadamu tumeekewa mipaka na ni ngumu kuweza kuwajua watu wa makundi haya matatu..ila Mungu ni muona yote na yeye anajua zaidi.
Fc neno la leo ni kipengelea kipya ambacho kitawashirikisha wadau mbali mbali wa blog hii.ukiwa na ujumbe au neno lolote nimekukaa na unataka ku share nasi pamoja na kufikisha ujumbe kwa jamii yetu. tafadhali tutumie ujumbe wako kupitia.
email:fromcoast1@hotmail.com
twitter:@fromcoast
nasi tutalieka hapa itapendeza zaidi kama utatumia jina au picha yako (lakini ni hiari sio lazima.)
ahsante adm.
[ Read More ]
email:fromcoast1@hotmail.com
twitter:@fromcoast
nasi tutalieka hapa itapendeza zaidi kama utatumia jina au picha yako (lakini ni hiari sio lazima.)
ahsante adm.
Tahadhari yatolewa juu Tishio La Tsunami Bahari Ya Hindi Baada Ya Tetemeko La Ardhi Lenye Ukubwa Wa Magnitude 8.7 Chini Ya Bahari Kuitikisa Indonesia.
Sea levels indicate a Tsunami was been generated. It is estimated to reach the Kenyan Coastline of Mombasa at 17:06 hrs, and the Tanzanian Coastlines of Lindi at 17:07hrs, & Dar es Salaam at 17:10hrs
Msanii maarufu wa filamu hapa nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’ leo amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu jijini Dar es Salaam na kusomewa shitaka la mauaji.
Lulu alipandishwa kizimbani kwa usiri mkubwa akitokea Kituo cha Polisi cha Oysterbay alikokuwa akishikiliwa na kupandishwa kizimbani moja kwa moja bila kuwekwa mahabusu ya mahakama hiyo kama iwavyo kwa washitakiwa wengine wanaosubiri kusomewa kesi zao.
Baada ya kupandishwa kizambani alisomewa shitaka lake na Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama hiyo, Elizabeth Kaganda ambapo alisema Mnamo Aprili 7 mwaka huu majira ya saa saba za usiku maeneo ya Sinza Vatican jijini Dar es Salaam Elizabeth Michael (18) alimuua Steven Kanumba. Katika kesi hiyo mshitakiwa hakutakiwa kujibu lolote isipokuwa alinyoosha kidole na kupinga umri uliotajwa kuwa ana miaka 18 na kusema umri wake ni miaka 17. Baada ya kusomewa shitaka hilo, Lulu alipelekwa gerezani Segerea na kesi yake itasikilizwa tena aprili 23 mwaka huu.
source.GPL
The US Geological Survey said Wednesday the quake was centered 20 miles beneath the ocean floor around 308 miles from the provincial capital of Banda Aceh.
Said, an official at Indonesia's Meteorology and Geophysics Agency who goes by only one name, said a tsunami warning has been issued.
Indonesia straddles a series of fault lines that makes the vast island nation prone to volcanic and seismic activity.
A giant 9.1-magnitude quake off the country on December 26, 2004, triggered a tsunami in the Indian Ocean that killed 230,000 people, nearly three quarter of them in Aceh.
Source: AP
Kuna uwezekano mkubwa ya baadhi ya watu kupoteza maisha katika msiba huu kutokana na watu kukanyagana! Japo hakuna taarifa kamili!!na huku baadhi ya watu wakiimba nyimbo uku wakikimbia haya ni baadhi ya maneno... "polisi tunamtaka lulu huyo aliyeua
Imeshindikana kabisa kwa jeneza kuingizwa makaburini Kinondoni.Kamati iko busy kuangalia nini cha kufanya
na jeff msangi.twitter.
[ Read More ]
na jeff msangi.twitter.
Mkuu wa majeshi 1988 hadi 1994 General Ernest mwita kyaro afariki dunia.akiwa njiani kuelekea bugando.
[ Read More ]
Msalaba Mwekundu wakiwa stand by na pia msaada unahitajika
Watu wameisha anza kuzima na msalaba mwekundu umeanza kazi yao
Watu wengi wanazidiwa na kuzimia.Jamaa wa Red Cross wanajitahidi kadiri wanavyoweza.They are doing an amazing job
Ni majonzi
Mgeni Rasmi Mama Salma alipowasili msibani na waombolezaji wengine
Mbunge wa Mbeya Mjini Mh. Joseph Mbiliyini alipowasili viwanjani hapo
Mheshimiwa Joseph Mbilinyi akiongea na wanahabari
Nnape Nnauye akiongea na wanahabari juu ya msiba huu
Umati wa watu
Millard Ayo & Ephraim Kibonde ndo wanedesha shughuli
Huyu ni kibaka akiwa amenaswa hapo msibani
Jukwaa likfanyiwa maandilizi
Mheshimiwa Joseph Mbilinyi akiongea na wanahabari Nnape Nnauye akiongea na wanahabari juu ya msiba huu Umati wa watu Millard Ayo & Ephraim Kibonde ndo wanedesha shughuli Huyu ni kibaka akiwa amenaswa hapo msibani
Kwa habari zilizo tufikia na aliyepo eneo la tukio (Viwanja vya Leaders) ambako mwili wa marehemu Steven Kanumba uliwasili majira ya saa tatu kwa ajili ya misa na kuagwa.
Zoezi la kuaga limeshindikana kwa upande wa umati mkubwa wa wananchi waliohudhuria hapo baada ya viongozi pekee kupata fursa ya kuaga na kufuatiwa fujo na polisi kushindwa kudhibiti kulingana na idadi kubwa ya waombolezaji.
Hivyo mwili wa msanii huyo maarufu wa filamu unaelekea kuzikwa katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam huku gari iliyobeba mwili wake ikisukumwa na wananchi waliojipanga barabarani kuelekea makaburini.
Huu ni umati wa watu unao elekea makaburini
Gari lililo beba mwili wa marehemu Steven Kanumba likielekea makaburini
picha na jeff masangi.
mama wa marehemu akiwasili uwanjani hapo
eneza lililobeba mwili wa Marehemu limewasili.Watu wanalia kwa uchungu sana.Wengi wanagombania kuligusa
Kwa mbele
red cross wakiwa uwanjani hapo kutoa huduma.
Msanii nyota wa filamu nchini, Steven Kanumba amefariki kutokana na tatizo la mtikisiko wa ubongo linalojulikana kitaalamu kama BRAIN CONCUSSION, taarifa za kitabibu zimeeleza.
Taarifa hizo za ndani, zimepatikana jana baada ya jopo la madaktari bingwa watano wa hospitali ya taifa Muhimbili kuufanyia uchunguzi mwili wa marehem, zimeeleza kuwa tatizo hilo linaweza kumfanya mtu apoteze maisha mara moja au baada ya siku kadhaa.Mmoja wa madaktari hao ambae aliomba jina lake lisitajwe gazetini alisema waligundua tatizo hilo baada ya kumfanyia uchunguzi huo kwa zaidi ya masaa mawili.
"tulianza kuufanyia uchunguzi mwili wa marehemu kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa 6:45 mchana na tukagundua kuwa marehemu alifariki kutokana na mtikisiko wa ubongo kwa kitaalamu Brain Concussion" alisema. Kanumba alipata mtikisko huo ambao husababisha kufeli kwa mfumo wa upumuaji (cardio-respiratory failure) "kilichomuua hasa ni mtikisiko wa ubongo, ambao endapo unatokea katika sehem ya nyuma ua ubongo (cerebram), huua kwa haraka" alisema daktari huyo na kuongeza kuwa mtikisiko wa ubongo wa nyuma husababusha matatizo ya mfumo wa upumuaji na hilo limeonekana katika mwili wake.
"Baada ya ubongo wake kutikiswa kwa nguvu, mfumo wa upumuaji unafeli na ndio maana tumekuta kucha za kanumba zikiwa na rangi ya blue, huku mapafu yake yakiwa yamevilia damu na kubadilika kuwa kama maini, hizo ni dalili za kufeli kwa mfumo wa upumuaji"
"Mtu aliepata mtikisko wa ubongo huweza kutokwa na mapovu mdomoni na hukoroma kabla ya kukata roho na ndivyo ilivyokuwa kwa Kanumba kabla hajafariki.
Daktari mwingine alieshiriki katika uchunguzi huo ambae pia aliomba jina lake lisitahwe alisema ubongo wa mwigizaji huyo umevimba na kushuka karibu na uti wa mgongo na hivyo kuathiri mfumo wa upumuaji. Alisema sehemu ya maini na maji maji ya machoni ya marehemu, vimepelekwa kwa mkemia mkuu wa Serikali ili kubaini endapo kuna sumu au kitu kingine katika mwili huo
Wanawake wawili wafanyabiashara wa nchini wametiwa mikononi mwa walinzi wa raia na mali zao mjini Morogoro wakidaiwa kukwapua kitita cha fedha kiasi cha Shilingi milioni 4.4 za kitanzania.
Taarifa za kipolisi kutoka Moropgoro zinapasha kuwa wanawake hao walikwiba fedha hizo mali ya Jackson Edson mkazi wa mjini Morogoro alipo fika kuweka fedha benki ya CRDB , Morogoro.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Adolfina Chialo , aalitanabaisha hayo na kuwataja watuhumiwa hao kuwa ni Iren Kharim na Jane Ndunilo kutoka jiji laNairobi, Kenya.
Chialo alitoa taarifa hizo kuwa tukio lilitendeka siku ya Aprili 4 mishale ya saa 4 asubuhi CRDB tawi la Morogoro katika mitaa ya Masika na Ngoto.
Wanawake hao majasiri wanadaiwa kufanya wizi huo kwa njia ya aina yake ambayo watu wote tunaoingia benki yatupasa kuwa makini nayo ya kuombwa msaada wa kufanyiwa kitu au kuelekezwa.
“Watuhumiwa hao waliomba msaada kutoka kwa mfanyabiashara huyo wa kuwajazia fomu lakini na wakati wakipatiwa msaada huo walivuta bahasha yenye fedha hizo iliyokuwa mezani na kuondoka,”alisema Kamanda wa Polisi.
kamanda wa Polisi anasema ni Polisi jamii tu ndio iliyo okoa bulungutu hilo la fedha baada ya watu waliopo ndani ya Benki kuwataiti wakisaidiana na askari wa benki.
Baade watuhumiwa walipelekwa katika kituo cha Polisi cha kati kilichopo mjini hapa kwa mahojiano zaidi na pindi uchunguzi wa Kipolisi utakapo kamilika watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani kujibu mashtaka yao.
[ Read More ]
Taarifa za kipolisi kutoka Moropgoro zinapasha kuwa wanawake hao walikwiba fedha hizo mali ya Jackson Edson mkazi wa mjini Morogoro alipo fika kuweka fedha benki ya CRDB , Morogoro.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Adolfina Chialo , aalitanabaisha hayo na kuwataja watuhumiwa hao kuwa ni Iren Kharim na Jane Ndunilo kutoka jiji laNairobi, Kenya.
Chialo alitoa taarifa hizo kuwa tukio lilitendeka siku ya Aprili 4 mishale ya saa 4 asubuhi CRDB tawi la Morogoro katika mitaa ya Masika na Ngoto.
Wanawake hao majasiri wanadaiwa kufanya wizi huo kwa njia ya aina yake ambayo watu wote tunaoingia benki yatupasa kuwa makini nayo ya kuombwa msaada wa kufanyiwa kitu au kuelekezwa.
“Watuhumiwa hao waliomba msaada kutoka kwa mfanyabiashara huyo wa kuwajazia fomu lakini na wakati wakipatiwa msaada huo walivuta bahasha yenye fedha hizo iliyokuwa mezani na kuondoka,”alisema Kamanda wa Polisi.
kamanda wa Polisi anasema ni Polisi jamii tu ndio iliyo okoa bulungutu hilo la fedha baada ya watu waliopo ndani ya Benki kuwataiti wakisaidiana na askari wa benki.
Baade watuhumiwa walipelekwa katika kituo cha Polisi cha kati kilichopo mjini hapa kwa mahojiano zaidi na pindi uchunguzi wa Kipolisi utakapo kamilika watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani kujibu mashtaka yao.
Hayati Steve Kanumba ni miongoni mwa wasanii maarufu wa Tanzania wenye nyota za umaarufu (Tanzania Walk of Fame) ndani ya ukumbi wa Dar Live jijini Dar Es salaam ambapo mara baada ya kifo chake wafanyakazi wa ukumbi huo na mashabiki wake wameweka mashada ya maua,kadi na kuwasha mishumaa kama ishara ya kuomboleza kifo chake.
...baadhi ya staff wa Dar Live wakiwasha mshumaa kwenye nyota ya Kanumba
...Nyota ya Kanumba ilivyo ndani ya Dar Live katika sehemu ya Tanzania Walk of Fame.
picha na abdallah mrisho.
Ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATC) imeanguka katika uwanja wa ndege wa Kigoma ikiwa katika matayarisho ya kupaa.Habari zinasema kwamba abiria wote pamoja na wafanyakazi wa ndege hiyo wamenusurika.
WAKATI MAOMBOLEZO YA MSIBA YAKIENDELEA VIONGOZI MBALIMBALI WAKIFIKA KUTOA MKONO WAPOLE AMBAPO LEO MHESHIMIWA PREZIDAR J.K ALIFIKA NYUMBANI KWA KANUMBA KUTOA MKONO WA POLE, NA KESHO ASUBUHU WAZIRI MKUU MHESHIMIWA PINDA ANATARAJIWA KUFIKA KUTOA MKONO WA POLE KABLA YA KUELEKEA MKOANI DODOMA KWA AJILI YA BUNGE LINALOANZA JUMANNE
RATIBA YA MAZISHI IMETOLEWA RASMI AMBAPO MAZISHI YAMEPANGWA KUFANYIKA SIKU YA JUMANNE KAMA ILIVYOKUWA IMEPANGWA, MAREHEMU ATAAGWA KATIKA VIWANJA VYA LEADERS CLUB AMBAPO KUANZIA SAA 4 SHUGHULI ZA MISA NA KUAGA MWILI ZITAANZA NA KISHA MAREHEMU ATAZIKWA KATIKA MAKABURI YA KINONDONI JIJINI.
R.I.P KANUMBA
MAMA MZAZI WA MAREHEMU AMESHAFIKA JIJINI NA AMETOA BARAKA ZOTE ZA MAZISHI YAFANYIKE HAPAHAPA JIJINI
MSALABA MWEKUNDU WAPO NA KAZI YAO INAONEKANA KWANI WATU WANAZIMIA MARA KWA MARA NAO WANAONEKANA KUFANYA KAZI YAO KWA USTADI
sisi tulimpenda bali mungu kampenda zaidi
MISA ZINAENDELEA HAPO HAPO NYUMBANI KWA MAREHEMU,HILI NI KUNDI LA WANAKWAYA WA KANISA ALILOKUWA ANASALI KANUMBA
KAMA KAWAIDA MASHABIKI WA KANUMBA WAKO NJE WAKIFUATILIA MSIBA WA KIPENZI CHAO
source 8020..