Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

JK Amtumia Salamu Za Pongezi Spika Anne Makinda

-
Rehema Mwinyi.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za Pongezi Mheshimiwa Anne Makinda kwa kuchaguliwa kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika salaam zake,Rais amesema,Spika Makinda amechaguliwa kwa sababu ya uwezo wake,uzoefu na umakini wake.“Ninakuahidi ushirikiano wangu katika shughuli zako za bunge na za kujenga nchi yetu kwa ujumla”Rais Amesema na kuongeza kuwa kuchaguliwa kwa Mama Makinda “Ni heshima kwa Chama Cha Mapinduzi, umejenga imani kubwa kwa wanawake na umewatia moyo na shauku ya kufanya kazi kwa ufanisi na ueledi katika jitihada zao za kushika nyadhifa mbalimbali za maamuzi.”Rais amesema na kumtakia kheri katika shughuli zake za kila siku.

Imetolewa na Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu
Dar-es-salaam.
12 Novemba, 2010

Leave a Reply