Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

Kama DC Mstaafu Anatendwa Hivi,Mlalahoi Je?

-
Rehema Mwinyi.



Raymond Kaminyoge
TANGU Machi mwaka jana alipostaafishwa kazi na 
Rais Jakaya Kikwete, 
akiwa Mkuu wa Wilaya ya Mbalali, Mbeya,
Hawa Ngulume amekuwa 
haonekani hadharani wala kusikika kwenye vyombo vya
habari kama tulivyomzoea.

Tunakumbuka jinsi alivyoendesha operesheni ya 
kuwaondoa wafugaji 
katika Bonde la Ihefu wilayani humo na kusababisha 
habari zake kutawala
 kwenye vyombo vya habari na kusababisha malumbano 
makali kati ya 
wafugaji na wanamazingira.

Tunakumbuka pia alivyoendesha operesheni hiyo kwa 
yeye mwenyewe
 kutembea kwa miguu akisindikiza ng’ombe kuondoka 
kwenye bonde
 hilo hali iliyomfanya achukiwe na wafugaji hao lakini 
akapendwa na 
wanamazingira.

Tunashuhudia hivi sasa baada ya kuondoka kwa 
wafugaji kwenye 
bonde hilo, hali mazingira ni shwali kwani ukijani na
 uoto wa asili 
umeanza kurejea katika bonde hilo.

Hayo aliyafanya akiwa mkuu wa wilaya ya
 Mbalali kabla 
hajastaafishwa na kumpisha mwenzake Luteni 
Cosmas Kayombo.

Hayo yote yanakumbukwa na Ngulume, ambaye 
hivi sasa yuko katika
 hali mbaya kiafya nyumbani kwake Goba Kinzudi, 
jijini Dar es Salaam 
akisumbuliwa na maradhi ya vichomi na mapafu.

Hata hivyo, bado madaktari hawajathibitisha ni nini hasa 
kinachomsumbua 
kutokana na kukosekana kwa kipimo mbadala cha kupima 
kansa ya mapafu.

Mwananchi lilifika nyumbani kwake na aliamua kueleza 
yaliyokuwa
 moyoni mwake: “Nimeona bora nitumie chombo cha habari 
kufikisha
 ujumbe wa ugonjwa kabla sijafa.”

Anaongeza: “Kwa miezi mitatu sasa niko hoi kitandani,
 siwezi
 kutembea bila kusaidiwa, naiomba serikali inisaidie niweze 
kwenda India ambako kuna vipimo na tiba ya maradhi
 yanayonisumbua.”

Anasema ameamua kutumia gazeti hili ili kufikisha
 ujumbe kwa 
serikali na CCM kuhusu maradhi yanayomsumbua 
baada ya 
njia nyingine kushindikana.

“Nilipeleka taarifa kwenye chama changu kwamba 
naumwa nahitaji msaada,
 lakini sikujibiwa, pia nimefanya juhudi za kutaka 
kumwona Waziri Mkuu
 ili anisaidie lakini juhudi zangu hazikuzaa matunda,
 nimeamua nitumie 
chombo cha habari kabla sijafikwa na mauti,” anasema.

Ngulume ambaye ni kada maarufu wa CCM 
aliyetumikia nafasi ya 
ukuu wa wilaya kwa miaka 18, anasema maradhi 
yanayomsumbua 
yalianza baada ya kumalizika kwa mchakato wa kura za maoni 
za chama hicho.

Anasema aliomba ridhaa ya chama hicho 
kimsimamishe kuwa 
mgombea ubunge katika Jimbo la Singida Mjini
 lakini hakufanikiwa.

“Katika mchakato ule, Mohammed Dewji alishinda 
na mimi nikawa 
mshindi wa pili, niliporudi Dar es Salaam nikaanza
 kujiandaa kwenda 
kumpigia debe Dewji, kama ulivyo utaratibu wa chama chetu, 
ndipo nikaanza kuumwa ghafla,” anasema na kuongeza:

“Nilipenda kushiriki kwenye kampeni ili kuwasaidia 
wagombea mbalimbali 
wa chama changu lakini anadhani Mungu hakupenda
 nifanye hivyo.”

Ngulume ambaye amewahi kuwa mkuu wa wilaya 
mbalimbali 
zikiwemo za Kinondoni, Bagamoyo na Kibaha 
anasema baada ya
 kuumwa amekuwa akipata tiba za aina tofauti
 lakini hazijamsaidia.

“Nasikia maumivu makali tumboni, utadhani kuna 
msumeno unakata 
viungo vyangu, usiku kucha sipati usingizi ni maumivu tu
 ndiyo yanayotawala
 mwili wangu,” anasema.

Anasema amekwishatibiwa kwenye Hospitali za Lugalo,
 Ocean Road na 
Imtu zote za Dar es Salaam lakini mbali ya kutopata nafuu, 
hali yake 
inazidi kuwa mbaya siku hadi siku.

“Katika hospitali ya Ocean Road nilitakiwa kupima 
kama mapafu
 yana maji ili kuthibitisha kama ni kansa ya mapafu 
lakini kipimo kilichopo 
kinatakiwa kukaa katika kinywa nami sina pumzi, 
hivyo ikashindikana
 kupima,” anasema.

Anaongeza kuwa hadi sasa hawezi kuweka wazi 
kuhusu maradhi 
yanayomsumbua kwa vile vipimo mbadala ya
 vile vya kuwekwa
 katika kinywa vinapatikana nje ya nchi.

“Ndiyo maana naomba msaada wa kwenda 
kutibiwa nje kwani 
nikipimwa ndipo naweza kupata tiba ya uhakika,”
 anasema kwa taabu.

Anasema katika kuhangaika kutafuta tiba aliwahi
 kwenda katika
 Hospitali ya Taifa ya Muhimbili lakini cha 
kushangaza alikaa 
kuanzia saa 8.00 mchana hadi saa 11.00 jioni
 bila kuhudumiwa.

“Ndipo mtu mmoja anayenifahamu alipopita 
nilipoketi akanisalimia
 kwa kuniita mheshimiwa. Muuguzi mmoja jina
 ninalihifadhi
 akaja kutaka kunihudumia, nikamwambia ina maana 
siwezi kuhudumiwa
 hadi niwe mheshimiwa? Nikaondoka kwa hasira 
nikakataa kuhudumiwa,”
 anasema.

Siku moja baada ya kuzungumza na gazeti hilo,
 Ofisi ya Waziri
 Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, 
(Tamisemi) aliyokuwa
 akifanya kazi chini yake ilitoa tamko la kusimamia
 matibabu yake nje ya nchi.

Ujumbe wa maofisa wa Tamisemi ulifika 
nyumbani kwa mkuu huyo 
wa zamani wa wilaya kumjulia hali. Hatua 
hiyo imekuwa faraja
 kwa Ngulume ambaye anasema ingawa 
bado ana maumivu makali, 
amefurahi kwani kuna maofisa kutoka 
Tamisemi waliomtembelea 
na kumpa matumaini kwamba huenda 
akaenda nje kutibiwa.

“Baada ya gazeti lenu kuandika habari zangu, 
ujumbe wa Tamisemi 
umefika nyumbani kwangu kuniangalia na
 kuniahidi kwamba utafanya
 mipango kwa kushirikiana na Wizara ya 
Afya na Ustawi wa Jamii ili
 niweze kwenda nje kutibiwa,” alisema.

Alisema mbali na ujumbe huo, watu wengi ambao 
hawakuwa na
 taarifa zake, wameanza kumtembelea na wengine
 kumpigia simu 
wakimuombea kwa Mungu ili aweze kupona maradhi
 yanayomsumbua.

“Nawashukuru waandishi wa mwananchi, kwani nyie ndiyo 
mlioujulisha 
umma kuhusu hali ya afya yangu, ninaomba kwa Mungu
 usiku kucha ili 
niweze kufanikiwa kutibiwa kwani maumivu ninayoyapata
 ni makali.

CHANZO: Mwananchi

Leave a Reply