Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

WAZANZIBARI WATUHUMIWA KUGHUSHI KWENYE ATM - CARDIFF

-
Rehema Mwinyi.

Polisi wa mji wa Cardiff nchini Uingereza wanawachunguza walimu watatu kutoka Zanzibar ambao wanahusishwa na mpango wa kujaribu kughushi katika moja ya mashine za ATM.

Mashine hiyo iliwekwa kifaa kinachoweza kukopi namba za siri (PIN numbers) na kuwekwa katika mtaa mmoja wa Working huko mjini Cardiff. Polisi walijulishwa kuwepo kwa mpango huo na kuwakamata watu watatu wenye umri wa miaka 51, 28 na 20 tarehe 18 Septemba 2010.

Inasemekana walimu hawa walikuja Uingereza katika mradi unaodhaminiwa na British Council na walikuwa chini ya Sazani Associates ambayo ni NGO iliyoratibu ujio wao.

Hata hivyo Sazani associates walipeleka malalamiko rasmi kwa Polisi kwani Walimu hawa walikwenda Cardiff kwa ajili ya kufanya shopping kununua zawadi na si vyenginevyo. Na waliachiwa siku ya pili yake bila ya kushitakiwa.

Mkurugenzi wa Sazani Associates Cathryn Akl Kanaan alisisistiza kwamba NGO yao inajihusisha zaidi na elimu pamoja na kusaidia sehemu za vijijini katika nchi masikini.

Chanzo . walesonline.co.uk

Leave a Reply