Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

Mwili wa Marehemu Haji Mohammed wapokelewa kwa Simanzi Zanzibar na Wapenzi wake na Wananchi katika Bandari ya Zanzibar.



Marehemu Haji Mohammed Kirembwe cha Siti Bint Saad, wakati wa uhai wake akiimba na kikundi cha gusagusa .

 Mtoto wa Kwanza wa Marehemu Haji Mohammed, akishindikizwa na nduga na jamaa waliofika katika bandari ya Zanzibar kupokea mwili huo leo jioni ukitokea Jijini  Dar-es- Salaam, 
Marehemu Haji Mohammed anatarajiwa kuzikwa kesho saa 4.00 asubuhi na sala ya maiti itafanyika Mskiti Nambari Muembetanga. 

Marehemu alikuwa Msanii kwa muda mrefu na Kikundi chake cha kwanza kujiunga kilikuwa Kikundi cha Taraab cha Malindi, akiwa ni mpiga kinanda na mtunzi na muimbaji katika kikundi hicho.Na hatimae kuanzisha kikundi  kilichojulikana kwa Jina la  East African Melody.

Akiwa Mkurugenzi wa Kikundi hicho na alikihamishia makazi ya Kikundi hicho katika Jiji la Dar-es-Salaam na kutoa burudani kwa Wapenzi wao.
Pia alianzisha Kikundi cha Gusagusa ambacho kilikuwa kikipiga nyimbo za zamani katika ukumbi wa DDC Kariakoo siku za week end hutowa burudani hiyo.
 Wananchi wakipokea jeneza la Marehemu Haji Mohammed katika bandari ya Zanzibar leo jioni.

[ Read More ]

Rais Kikwete awasili Nairobi kuhudhuria kuapishwa kwa Rais mpya wa Kenya, Uhuru Kenyatta



 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe mama Salma Kikwete wakipokea maua mara baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi tayari kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Nne wa Kenya Mhe Uhuru Muigai Kenyatta na Naibu Rais wake Mhe William Ruto katika uwanja wa michezo wa Kasarani leo April 9, 2013
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe mama Salma Kikwete wakilakiwa kwa heshima zote baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi tayari kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Nne wa Kenya Mhe Uhuru Muigai Kenyatta na Naibu Rais wake Mhe William Ruto katika uwanja wa michezo wa Kasarani leo April 9, 2013
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini kitabu cha wageni baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi tayari kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Nne wa Kenya Mhe Uhuru Muigai Kenyatta na Naibu Rais wake Mhe William Ruto katika uwanja wa michezo wa Kasarani kesho April 9, 2013. Mama Salma Kikwete na Balozi wa Tanzania nchini Kenya Dkt Batilda Burian wamesimama pembeni na wenyeji wao

PICHA NA IKULU
[ Read More ]

DR. SALIM AHMED SALIM AONGOZA MAADHIMISHO YA 19 YA MAUAJI YA KIMBARI YALIYOTOKEA NCHINI RWANDA YALIYOFANYIKA JIJINI DAR.



Maandamano ya raia wa Rwanda wanaoishi nchini Tanzania pamoja na wanafunzi wa shule mbalimbali za jijini Dar es Salaam wakijipanga katika ukumbi wa New World Cinema tayari kuanza maandamano ya kuadhimisha miaka 19 ya mauaji ya Kimbari ya Rwanda kuelekea ukumbi wa mikutano wa Mlimani City. (Picha na Zainul Mzige wa Mo Blog)
Picha juu na chini Umati wa maandamano yakielekea katika ukumbi huo.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo Dr. Salim Ahmed Salim njiani kuelekea kwenye ukumbi wa mikutano Mlimani City.
Mgeni rasmi Dr. Salim Ahmed Salim (wa tatu kulia) akiwa na balozi wa Rwanda nchini Tanzania Mh. Benjamin Ruganganzi (wa tatu kushoto) wakisubiri kupokea maandamo ya maadhimisho ya miaka 19 ya mauaji ya Kimbari ya Rwanda katika viwanja vya Mlimani City jijini Dar.

Dr. Salim Ahmed Salim akipokea rasmi maandamano hayo.
Mgeni rasmi katika maadhimisho ya 19 ya mauaji ya Kimbari ya Rwanda Dr. Salim Ahmed Salim akizungumzia kumbukumbu ya mauaji hayo ambapo amesema historia ipo kwa ajili yetu sote kujikumbusha yaliyopita ili tuweze kupanga yajayo na kuwa mauaji ya Kimbari ni mzigo wetu sote na tunapaswa kujifunza kutambua alama za watu wa jamii moja kuanza kuhitilafiana na kutafuta namna ya kuzitatua kabla hazijaleta athari.
Na pia alichukua fursa hiyo na kunukuu maneno yaliyowahi kusemwa na Baba wa Taifa wa Tanzania Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere " Ukweli ni kwamba kila sehemu ya Afrika ina ihitaji Afrika kwa pamoja na Afrika kama bara inahitaji kila sehemu ya bara la Afrika".
MC katika maadhimisho ya miaka 19 ya mauaji ya Kimbari Usia Nkhoma akirekebisha kipaza sauti wakati mgeni rasmi akizungumza wakati wa maashimisho hayo.
Wageni waalikwa wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi (hayupo pichani) wakati wa kumbukumbu ya maashimisho ya miaka 19 ya mauaji ya Kimbari Rwanda.
Kaimu Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Bw. Jama Gulaid ambaye pia ni Mkurugenzi Mkazi wa UNICEF akizungumza wakati maadhimisho ya miaka 19 ya mauaji ya Kimbari nchini Rwanda yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City ambapo amesema dunia nzima itakuwa na siku maalum ya kukumbuka wahanga wa mauaji ya Kimbari ya Rwanda kwa heshima ambayo ni alama ya kukumbuka athari za mauaji hayo na kuwa pamoja na walionusurika na kwa namna nyingine ni alama msingi ya kupongeza hatua zilizochukuliwa na jamii ya Wanarwanda kuungana pamoja.
Katika mazungumzo yake alinukuu maneno yaliyozungumzwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon " Katika maasdhimisho ya 19 ya mauaji ya Rwanda tunawakumbuka watu zaidi ya 800,000 wasio na hatia ambao walipoteza maisha yao na tutanendelea kuwaheshimu walionusurika na tutaendelea kuwa nao pamoja na kukemea wale wote waliohusika na tukio hilo, na kuwapongeza waliojitokeza kuzuia mauaji hayo yasiendelee".
Balozi wa Rwanda nchini Tanzania Mh. Benjamin Ruganganzi akitoa salamu zake kwa wageni waalikwa pamoja na watu waliohudhuria maadhimisho ya 19 ya mauaji ya Kimbari ya Rwanda na kuhakikisha kuwa wananchi wa Rwanda wataendelea kudumisha uhusiano na ushirikiano pamoja na nchini zingine za Afrika Mashariki ili kuhakikisha tukio kama hilo halitajirudia tena.
Sehemu ya wageni waalikwa wakiwemo mabalozi mbalimbali wakimsikiliza Balozi wa Rwanda nchini (hayupo pichani).
Msemaji wa Mahakama ya Umoja wa Mataifa ya Mauaji ya Rwanda (ICTR) Bw. Roland Ammousouga akitoa kauli yake wakati wa maadhimisho ya 19 ya mauaji ya Kimbari ya Rwanda ambapo amesema kwa miaka 19 iliyopita watu wanaweza wakajisifu kazi iliyofanywa na mahakama ya ICTR kwamba imetimiza kilio cha maelefu ya waathirika na kuwa imesaidia katika kuleta upatanishi na kuijenga upya Rwanda sambamba na kuhamasisha amani na ulinzi katika ukanda wa Afrika wa maziwa makuu, wakati haikufanikiwa kuwakamata wale wote waliohusisha na mauaji hayo kwa kutoa itumia Rwanda kuwatafuta wahusika 6 waiojulikana walipo ili waweze kukabiliana na kesi zinazowakabili kinachojionyesha hapa ni kwamba ICTR inaashiria kwamba mapambano dhidi ya mazingira ya wahusika wengine 3 hawawezi kukamatwa.
Umati wa watu waliofurika (chini) katika maadhimisho hayo wakiwemo wanafunzi wa shule ya sekondari Jitegemee (juu).
Mmoja wa viongozi wa Dini akiomba dua ya kuwarehemu walipoteza maisha katika mauaji ya Kimbari yaliyotokea nchini Rwanda.
Meza kuu ikiongozwa na mgeni rasmi Dr. Salim Ahmed Salim kuwasha mishumaa ikiwa ni ishara ya kuwakumbuka watu waliopoteza maisha wakati wa mauji ya Kimbari nchini Rwanda.
Kwa picha zaidi ingia hapa
[ Read More ]

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO WA SIKU TATU WA MWAKA KUHUSU TAFITI ZA SERA NA MAENDELEO WA REPOA DAR



 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia washiriki wa mkutano wakati akifungua ramsi mkutano wa siku tatu wa mwaka kuhusu Tafiti za sera na Maendeleo wa Repoa, ulioanza leo April 3, 2013 katika Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam
 Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakiwa ukumbini humo wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifungua ramsi mkutano wa siku tatu wa mwaka kuhusu Tafiti za sera na Maendeleo wa Repoa, ulioanza leo April 3, 2013 katika Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya viongozi wakati akiwasili kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Kunduchi Beach, kufungua ramsi mkutano wa siku tatu wa mwaka kuhusu Tafiti za sera na Maendeleo wa Repoa, ulioanza leo April 3, 2013 katika Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam
 Mwenyekiti wa CUF Prof. Ibrahim Lipumba, akichangia wakati wa mkutano mkutano wa siku tatu wa mwaka kuhusu Tafiti za sera na Maendeleo wa Repoa, ulioanza leo April 3, 2013 katika Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam. Mkutano huo umefunguliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano wa siku tatu wa mwaka kuhusu Tafiti za sera na Maendeleo wa Repoa, baada ya kuufungua mkutano hio, ulioanza leo April 3, 2013 katika Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam. Picha na OMR

Kikao cha Baraza la Wawakilishi Zanzibar.

 Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Pandu Ameir Kificho akitoka katika Ukumbi wa Baraza baada ya kuahirisha Kikao cha asubuhi, kwa ajili ya mapumziko na kurudi jioni kuendelea na kuchangia miswada iliowakilisha katika Kikao hicho.  
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akibadilisha mawazo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha Omar Yussuf Mzee, wakitoka ukumbi wa mkutano baada ya kuahirishwa kikao cha asubuhi.
 Mwakilishi wa Donge na Waziri wa Ardhi Maji Nishati na Makaazi Juma Ali Shamuhuna, akimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Fatma Ferej,  
 Wajumbe wakibadilisha mawazo nje ya Ukumbi wa Baraza.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Maji Nishati na Makaazi Mustafa Aboud Jumbe akizungumza na Wajumbe wa Baraza baada ya kikao cha asubuhi kuahirishwa wakiwa katika viwanja vya Baraza, kushoto Mwanasheria wa Mkuu Zanzibar Othman Masoud na Mwakilishi wa MjiMkongwe Ismail Jussa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Mwakilishi wa Dimani Dk. Mwinyihaji Makame na Mwakilishi wa Bububu kulia Hussein Ibrahim Makungu (BHAA) wakitoka katika ukumbi wa baraza baada ya kuahirrishwa kwa kikoa cha asubuhi cha maswali na majibu na kujadili mswada wa Sheria ya Uundwaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma ya Maji na Nishati. Zanzibar
[ Read More ]

Utata wagubika kwa anayedaiwa kumuuwa Padri



omar-musa
Utata umegubika suala la mtu anayedaiwa kumuua kwa kumpiga risasi Padre Evarist Mushi wa Kanisa Katoliki baada ya ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) Zanzibar kuinyima Polisi kibali cha kumfikisha mahakamani.
Mtu huyo, Omar Mussa Makame wa Zanzibar alitarajiwa kupandishwa kizimbani juzi, lakini ofisi ya DPP ilikataa hiyo hiyo juzi kutoa kibali kwa Polisi kufanya hivyo. Omar aliwahi kugombea ujumbe wa Baraza la Wawakilishi kupitia Chama cha Wananchi (CUF) jimbo la Rahaleo mwaka 2010.
Awali Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa alisema jana kuwa wameshindwa kumfikisha mahakamani mtuhumiwa huyo kwa vile DPP hakuwapa kibali.
Alipulizwa sababu ambazo zimemfanya DPP asitoe kibali hicho, alisema ni vyema akaulizwa yeye mwenyewe kwani ndiye aliyetoa sababu hizo.
Mkurugenzi wa Mashitaka Zanzibar, Ibrahim Mzee Ibrahim alipofuatwa ofisini kwake jana ilielezwa kuwa yuko kwenye mkutano na mwandishi wa habari hizi akalazimika kumuandikia juu ya suala hilo kupitia kwa Katibu Muhtasi wake.
Alijibu kwa njia ya maandishi majibu yake yakiwa na maneno matatu tu: “Kamuone Kamishna Mussa”.
Alipoandikiwa tena kuwa Kamishna Mussa ndiye aliyesema uulizwe wewe kwani ndiye uliyetoa sababu alijibu kupitia kwa Katibu Muhtasi wake: “Yeye (Kamishna) anazijua sababu kwanini hataki kuzisema? Nendeni kwake mukamuulize”.
Alipoulizwa mara ya pili juu ya majibu hayo ya DPP Ibrahim, Kamishna Mussa alisema kwamba yeye hawezi kujibu mambo ya mtu mwingine.
“Ndio majibu yake ninayo, lakini yeye (DPP) ndiye aliyetoa sababu kwa hiyo ndiyo yeye anayetakiwa kuzisema sio mimi, nadhani hii ndiyo haki, aseme mwenyewe,” alisema Kamishana Mussa.
Mtuhumiwa huyo yuko mikononi mwa Polisi tangu Machi 17 mwaka huu alipokamatwa kuhusiana na mauaji hayo ya Padre Mushi aliyeuawa Februari 17 mwaka huu wakati akienda kuongoza ibada katika Kanisa la Mtakatifu Teresia liliopo Beit el Raas nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
Katika hatua nyengine Mahakama Kuu Zanzibar imeamuru kuletwa mahakamani kwa mtuhumiwa wa mauaji ya Padri Evaristus Mushi, jumatatu ijayo ili kuweza kusikiliza shauli lililofunguliwa juzi na mawakili wa upande wa mlalamikiwa la kutofishwa mahakamani kwa mteja wao ndani ya saa 24 baada ya kukamatwa.
Mtuhumiwa huyo Omar Mussa Makame (37)aliyekuwa mgombea uwakilishi wa Jimbo la Rahaleo katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 kupitia tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF) bado anashikiliwa na polisi Zanzibar, anatetewa na Kampuni ya Uwakili ya AJM Solicitors and Advocate.
Juzi mchana wakili wa Kampuni hiyo Abdalah Juma Mohamed aliwakilisha mahakama kuu ya Zanzibar maombi ya Habeas Corpus application chini ya kifungu cha 390 cha Sheria ya Makosa Jinai sura ya 7 ya mwaka 2007 inayomtaka mtu anayemshikila mtu mwingine au chombo chochote bila kumfikisha mahakamani kwa saa 24 aeleze mahamaka sababu za kushikilia mtu bila kumfikisha mahakamani au amwachie huru.
Mawakili hao walimtumia summons Mkurugenzi wa Mkosa ya Jinai Zanzibar (DCI) na jana Naibu wake Kamishina Msaidizi wa Polisi Yusuf Ilembo alifika mbele ya Jaji Isack Mkusa, kusikiliza shauli hilo.
Mawakili wa Kujitegemea upande wa mlalamikiwa waliokwakilishwa na Shabani Juma Shabani pamoja na Shaibu Ibrahim waliiomba mahakani hiyo iamuru kuachiwa kwa mteteja wao .
Hata hivyo jaji Mkusa alisema, kutokana na maombi hayo kuletwa chini ya kiapo vi vema pia Upande wa serikali nao ukapewa muda wa kujiandaa kuweza kujibu hoja hizo chini ya kiapo.
Baada ya kusikilza pande zote mbili Jaji Mkusa chini ya kifungu cha sheria section 8 ya mwaka 2006 inatoa nafasi kwa mtu kupewa dhamana lakini kwa jinsi mahakama itakanyoona inafaa.
Lakini wakati huo huo muhusika naye aletwe mahakamani wakati wa kusikiliza shauri lake ‘application’ kulingana na section 8.
Padre Mushi aliyekuwa Paroko wa Parokia ya Kanisa la Minara Miwili Zanzibar aliuawa asubuhi ya February 17 mwaka huu kwa kupigwa risasi wakati akijiandaa kuendesha ibada katika kanisa la Mtakatifu Theresia nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Kuuawa kwa risasi kwa Pandri Mushi, kulitanguliwa pia na shambulizi kama nilo kwa Padri Padri Ambrose Mkenda pia wa Kanisa Katokiki Zanzibar mwezi desemba mwaka jana ambaye alijeruhiwa taya ya kulazwa kwa siku kadhaa katika hospitali ya Taifa Muhimbili.
Wakati huo huo Ofisi ya DCI Zanzibar, imesema bado inasumbiri pia majarada mawili ya kesi ya kumwagiwa tindikali kwa 6 Nov 2012 kwa Katibu wa Mufti wa Zanzibar, Sheikh Fadhil Soraga, pia lile la Padri Ambrose Mkenda ambayo bado yapo kwa DPP ili kuwafikisha mahakamani watu wanaotunumiwa na makosa hayo mbao kwa sasa wako nje kwa dhamana.
Chanzo: Mwananchi
[ Read More ]

MCHUMBA WA PREZZO, GOLDIE WAFARIKI DUNIA




Goldie Harvey enzi za uhai wake.
Goldie akiwa na mchumba wake Prezzo.
MWANAMUZIKI kutoka nchini Nigeria, Goldie Harvey ambaye pia ni mchumba wa msanii Prezzo amefariki dunia.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari vya nchini Nigeria, Goldie amefariki dunia akiwa hopitalini nchini humo muda mfupi baada ya kutoka nchini Marekani alipohudhuria tuzo za Grammys. Prezzo hakupatikana kudhibitisha tukio hilo,…
Goldie Harvey enzi za uhai wake.
Goldie akiwa na mchumba wake Prezzo.
MWANAMUZIKI kutoka nchini Nigeria, Goldie Harvey ambaye pia ni mchumba wa msanii Prezzo amefariki dunia.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari vya nchini Nigeria, Goldie amefariki dunia akiwa hopitalini nchini humo muda mfupi baada ya kutoka nchini Marekani alipohudhuria tuzo za Grammys. Prezzo hakupatikana kudhibitisha tukio hilo, lakini mtu anayesimamia uwekaji habari katika ukurasa wa Facebook wa msanii huyo alidhibitisha kuwa msanii huyo amefariki dunia usiku wa kuamkia leo na kuandikia hivi “Kwa masikitiko makubwa napenda kuwataarifu wote kuwa Goldie amefariki dunia muda mfupi baada ya kuwasili jijini Lagos akitokea Marekani. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi,” Alisema mwekaji habari huyo.
Sababu zilizopelekea kifo cha msanii huyo mpaka sasa bado hazijafahamika.
[ Read More ]

UTOAJI WA VITAMBULISHO VYA TAIFA KWA UPANDE WA ZANZIBAR AWAMU YA KWANZA


06246Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipokea Kitambulisho cha Taifa kutoka
kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Perera Ame Silima,wakati wa
  Utoaji wa vitambulisho vya Taifa,awamu ya  kwanza kwa upande wa
Zanzibar,katika  hafla iliyofanyika jana  viwanja vya Baraza la
Wawakilishi Chukwani, Nje ya Mji wa Zanzibar,[Picha na Ramadhan
Othman,Ikulu.]
IMG_0018Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraz la Mapinduzi
Dk.Ali Mohamed Shein,akikaribishwa na Mkurugenzi Mkuu wa vitambulisho
vya Taifa,Dicson Maimu,alipowasili katika viwanja vya Baraza la
Wawakilishi Chukwani, Nje ya Mji wa Zanzibar,katika Utoaji wa
vitambulisho vya Taifa,awamu ya  kwanza kwa upande wa Zanzibar.[Picha
na Ramadhan Othman,Ikulu.]
IMG_9473Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji,akiweka
kidole Gumba kufanya uhakiki katika mashine maalum,wakati wa Utoaji wa
vitambulisho vya Taifa,awamu ya  kwanza kwa upande wa Zanzibar,katika
hafla iliyofanyika jana katika  viwanja vya Baraza la Wawakilishi
Chukwani, Nje ya Mji wa Zanzibar,[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
IMG_9486Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Pandu Ameir
Kificho,akiweka kidole Gumba kufanya uhakiki katika mashine
maalum,wakati wa Utoaji wa vitambulisho vya Taifa,awamu ya  kwanza kwa
upande wa Zanzibar,katika hafla iliyofanyika jana katika  viwanja vya
Baraza la Wawakilishi Chukwani, Nje ya Mji wa Zanzibar,[Picha na
Ramadhan Othman,Ikulu.]
IMG_9496Baadhi ya Viongozi na Wananchi,na Wafanyakazi wa
Mamlaka ya vita mbulisho wakiwa katika hafla ya  Utoaji wa
vitambulisho vya Taifa,awamu ya  kwanza kwa upande wa Zanzibar,katika
hafla iliyofanyika jana katika  viwanja vya Baraza la Wawakilishi
Chukwani, Nje ya Mji wa Zanzibar,[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
IMG_9511Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania,Jenerali Devis
Mwamunyange, akiweka kidole Gumba kufanya uhakiki katika mashine
maalum,wakati wa Utoaji wa vitambulisho vya Taifa,awamu ya  kwanza kwa
upande wa Zanzibar,katika hafla iliyofanyika jana katika  viwanja vya
Baraza la Wawakilishi Chukwani, Nje ya Mji wa Zanzibar,[Picha na
Ramadhan Othman,Ikulu.]
IMG_9735Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,(kushoto) akimkabidhi kitambulisho
Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi,wakati wa   Utoaji wa
vitambulisho vya Taifa,awamu ya  kwanza kwa upande wa Zanzibar,  hafla
ilifanyika jana katika  viwanja vya Baraza la Wawakilishi Chukwani, Nje
ya Mji wa Zanzibar,[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
IMG_9741Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,(kushoto) akimkabidhi kitambulisho Jaji
Mkuu wa Tanzania,Mohamed Chande Othman, wakati wa   Utoaji wa
vitambulisho vya Taifa,awamu ya  kwanza kwa upande wa Zanzibar,katika
hafla iliyofanyika jana  viwanja vya Baraza la Wawakilishi Chukwani,
Nje ya Mji wa Zanzibar,(kushoto) Naibu waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi Perera Ame Silima,[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.] 
IMG_9753Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,(kushoto) akimkabidhi kitambulisho Jaji
Mkuu wa Zanzibar,Omar Othman Makungu,wakati wa   Utoaji wa
vitambulisho vya Taifa,awamu ya  kwanza kwa upande wa Zanzibar,katika
hafla iliyofanyika jana katika  viwanja vya Baraza la Wawakilishi
Chukwani, Nje ya Mji wa Zanzibar,[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
IMG_9779Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,(kushoto) akimkabidhi kitambulisho Mama
Maria Nyerere,wakati wa   Utoaji wa vitambulisho vya Taifa,awamu ya
kwanza kwa upande wa Zanzibar,  hafla ilifanyika jana katika  viwanja
vya Baraza la Wawakilishi Chukwani, Nje ya Mji wa Zanzibar,[Picha na
Ramadhan Othman,Ikulu.]
[ Read More ]

Just in:

Inna lillahi waina ilaihi rajiun.

Ajali ya boti iliyokuwa ikitokea Pangani Tanga imezama watu wanane wamefariki wakiwemo watoto watatu. Na watu kumi na moja wamepotea baharini. Wengine wameokolewa na boti ilikuwa na jumla ya watu 35. Chombo hicho kimezama kutokana na hali ya hewa ya upepo,Mammlaka ya hali ya hewa jana mwanzoni mwa week hii imetoa tahadhari ya kuwepo kwa mvua kubwa na upepo.
[ Read More ]

Gas City: Hospitali ya Apollo kujengwa Kilwa


Wananchi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa, mkoani Lindi na wakaazi wa mikoa ya kusini kwa ujumla, wanatarajia kunufaika na ugunduzi wa gesi katika visiwa vya Zafaran na Lavan vilivyopo wilayani huo. Kampuni ya Statoil kutoka nchini Norway ikishirikiana na Exxon Mobil imegundua gesi katika Visiwa vya Zafaran na Lavan vilivyopo Kitalu namba 2, Ukanda wa Pwani ya Tanzania, hususan Pwani ya Kilwa mkoani Lindi. Kutokana na ujio wa wageni hao, Watanzania hususan wakazi wa Kilwa, Lindi na Mtwara kwa jumla hawana budi kupata faida za moja kwa moja na zingine zisizo za moja kwa moja ikiwemo gesi hiyo kutumika kutengeneza umeme utakaopatikana kwa uhakika na kuuzwa kwa wananchi wote. 
Akizungumza mjini Kilwa Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Kilwa, Adoh Mapunda amesema kuwa, madiwani, watendaji na mkuu wa wilaya wamekaa na kutafakari kwa kina juu ya faida ya kudumu itakayoonekana wilayani humo kutokana na ujio wa mradi wa gesi. Amefafanua zaidi kuwa mradi huo ni ujenzi wa hospitali ya kimataifa itakayolingana na ile ya Apollo nchini India ambayo viongozi mbalimbali duniani hukimbilia kwenda kutibiwa ambayo itajengwa na mwekezaji na itaendeshwa na taasisi nyingine ya kimataifa huku halmashauri ikiwa na hisa za kupata gawiwo la kila mwaka kutokana na faida. Mpango huo unatekelezwa kupitia utaratibu uliopo katika mikataba kwa wawekezaji kuhusu uwajibikaji na ushiriki katika masuala ya kijamii. Amesema kuwa, tayari Statoil imetenga Sh18 bilioni kuanza ujenzi wa hospitali hiyo mjini Kilwa wakati wowote kuanzia mwaka huu ambapo michoro ya hospitali hiyo ipo tayari huku ikitarajia madaktari bingwa kutoka ndani na nje ya nchi na itakuwa na wafanyakazi wataalamu, pamoja na wahudumu ambao wengi watatoka Halmashauri ya Kilwa.

[ Read More ]