Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

Matokeo Ya Kidato Cha Nne.

Matokeo ya Kidato cha nne 2009 yamewekwa hadharani leo huku takwimu zikionesha kuwa kiwango cha ufaulu kwa kidato cha nne yameshuka na yale ya mtihani wa maarifa(QT) kiwango kikiongezeka kwa asilimia 3.9 ukilinganisha na mwaka 2008.

Akitangaza matokeo hayo, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa, Dk Joyce Ndalichako (pichani) amepasha, mwaka 2009 ufauli kwa watahiniwa wa shule ni asilimia 72.51 ya watahiniwa 248,336 ikiwa imeshuka kwa tofauti ya asilimia 11.18 ukilinganisha na mwaka 2008 ambayo ilikuwa asilimia 83.69 na wale wa kujitengemea ni asilimia 54.12 ya watahiniwa 91,589 ikiwa imeshuka kwa asilimia 4.89 ya asilimia 59.01 ya mwaka 2008.

Kati ya watahiniwa 173, 323 waliofaulu, wasichana ni 74,696 (asilimia 67.59) na wavulana ni 98,627 kwa upande wa shule wakati kwa watahiniwa wa kujitegemea waliofaulu ni wasichana 25,044 na wavulana 24,433.

Dk. Ndalichako ametaja orodha ya wanafunzi wanafunzi bora 2009, ikiongozwa na msichana Imaculate Mosha wa Marian Girls akifuatwa na Gwamaka Njobelo wa Mzumbe.

Namba 3- Wolfgang Seiya wa Majengo ya Kilimanjaro 4- ni Vanessa Chilunda, 5 ni Faith Assenga na 6 ni Doreen Philbert wote wa Marian Girls 7 ni Zahra Meghji wa Usagara na 8 ni John Kimbari wa St. James Seminali, 9 ni Said Abdallh na10 ni Evans Lwanga wote wa Feza Boys.
Dk. Ndalichako alizitaja shule kumi bora zenye watahiniwa zaidi ya 35 ikiongozwa na Marian Girls ya Pwani ambayo mwaka 2008 ilikuwa ya pili na inafuatiwa na St. James Seminary ya Kilimanjaro, Don Bosco seminary ya Iringa ambayo mwaka 2008 ilikuwa nafasi ya nane imepanda hadi nafasi ya tatu.

Alisema sekondari ya wasichana ya St. Francis ya Mbeya ambayo mwaka 2008 ilishika nafasi ya kwanza imeshika nafasi ya nne na kufuatiwa na St. Mar’y Junior Seminary ya Pwani iliyonafasi ya tano huku Uru Seminary ya Kilimanjalo imeshuka nafasi tatu na kushika nafasi ya sita wakati sekondari ya wanaume ya Feza imepanda nafasi moja hadi nafasi ya saba.

Dk. Ndalichako alisema shule zilizoshika nafasi ya nane tisa na 10 ni Anwarite Girls, Maua Seminary na St Mary Goreti zote za Kilimanjalo.
Kwa upande wa shule zenye watahiniwa chini ya 35, Dk Ndaliachoka alisema kundi hilo linaongozwa na shule ya wasichana wa Feza ya Dar es Salaam na kufuatiwa na Mafinga Seminary ya Iringa, St. Joseph-kilocha Seminari ya Kilimanjaro iliyo nafasi ya tatu na nafasi ya nne ikishikwa na Queen of Apostle-Ushirombo ya Shinyanga.

Zingine kuwa ni Dungunyi Seminari ya Singida iliyonafasi ya tano na kufuatiwa na Rubya Seminary ya Kagera, Sengerema Seminary ya Mwanza iko nafasi ya saba na kufuatiwa na sekondari ya wasichana ya Bethelsabs ya Iringa huku Thomas More Machrina ya Dar es Salaam ikishika nafasi ya tinsa na Hellen’s pia ya Dar ikiwa nafasi ya 10.

Dk Ndaliachoka alizitaja shule kumi za mwisho kwa watahiniwa 35 au zaidi kuanzia iliyoshika mkia kuwa ni Busi ya Dodoma, Milola ya Lindi, Misima ya Tanga, Kiwere ya Tabora, Potwe da ya Tanga, Masanze ya Morogoro, Mandawa ya Lindi, Msata ya Pwani, Chekelei ya Tanga na Jangalo ya Dodoma.

Alizitaja shule kumi za mwisho zenye watahiniwa chini ya 35 kuwa ni Kizara ya Tanga, Mungumbi ya Lindi, Songolo ya Dodoma, Nakuhukahuka na Marambo za Lindi, Dole ya Zanzibar, Ruponda na Mpunyule za Lindi, Ruvuma ya Singida na Viziwi Njombe ya Iringa.

“ Hapa sina mchanganuo wa ufaulu wa somo moja moja, ila somo la Civis watahaniwa wamefaulu sana wakati hisabati imeendelea kuwapiga chenga.”

Hata hivyo, Dk. Ndalichako alisema baraza hilo limesitisha matokeo ya watahiniwa 7, 242 ambao hawajalipa ada ya mtihani na wamepewa muda wa miaka mwili kulipa na kinyume cha hapo matokeo hayo yatafutwa.

“ Pia tumesitisha matokeo ya watahiniwa wawili wa kujitegemea kutokana na kuwa na sifa zao kufanana, nah ii tumeigundua dakika za mwisho, majibu yao yatatole hadi hapo watakapoleta uthibitisho. Haiwezekani kufanana majina, wamezaliwa mwaka mmoja na sifa zo za kidato cha pili zinafanana na tumeshawaandikia matokeo.”

Dk. Ndalichako alisema kuwa na hata wanafunzi wawili wakafanana kila kitu, ikiwa ni majina, tarehe na umri wa kuzaliwa,” alisema.
Baraza hilo pia limefuta matokeo ya watahiniwa 405 na watano wa mtihani maarifa(QT).

“ Baraza limegundua udanganyifu wa watahiniwa kuwa na skripti zenye miandiko tofauti au kuwa na miandiko tofauti katika skripiti ya somo moja na hili tumeshirikiana na taasisi ya kubaini miandiko.

“ Pia kunawale ambao wamekamatwa na ‘notes, na wale waliokutwa chooni wakisoma, waliokutwa na simu kwenye chumba cha mtihani. Lakini wapo ambao walibainika na mfano usio wa kawaida wa majawabu, kwa mfano kuna wengi wamefanana kila kitu labda badala ya kuandika ‘themselves’ wanaandika ‘them selves’.”

Dk. Ndalichako aliongeza kuwa: “ Pia kunawengi ambao swali la kemia ambao lilitakiwa kueleza jinsi ya kutenganisha kerosene na water wao wajibu jinsi ya kutenganisha alcohol na water, lakini kulikuwa na udanganyifu hatari sana wa watahiniwa kubadilisha namba za wenzao.”
Alisema kuwa watahiniwa 53 pia wamefutiwa kutokana na kutokuwa na sifa kutoka shule za Mkwese sekondari(25), Ruruma (15), Thaqalaini(6), Bishop Kisanji(5), St Vicent na Edmund Rice Sinon kila moja mmoja.

Dk Ndalichako alisema mwanafunzi mmoja wa shule ya sekondari ya Kadoto amefutiwa matokeo kwa kuandika matusi kwenye skripti ya somo la baiolojia ikiwa ni kinyme na kifungu cha 5(13) cha kanuni za mitihani.
Pia alisema kuwa Baraza liemevifutia usajili wa watahiniwa wa kujitegemea kwa Sinza Iteba na Dar es salaam Prime vya Dar es salaam kutokana na kuzidiwa uwezo wa kuwachukua watahiniwa wengi.

Chanzo cha habari hii www.habarileo.co.tz
[ Read More ]

Mamia Wamzika Imran Mtui Mjini Moshi

Jeneza lenye mwili wa hayati Imran kijana aliyeuawa India hivi karibuni likitoka msikitini kuelekea katika makaburi ya Njoro mjini Moshi jana. Marehemu Imran alizikwa bila kuwa na kichwa. Picha na mdau Dixon Busagaga wa Moshi.
Mtanzania aliyeuawa India azikwa bila kichwa
Na Charles Ndagulla na
Dixson Busagaga, Moshi
VILIO, simanzi na majonzi jana vilitawala mazishi ya Mtanzania Imran Mtui (31) aliyeuawa kikatili nchini India hivi karibuni, katika mazishi yaliyofanyika makaburi ya Njoro Manispaa ya Moshi.

Mwili wa marehemu huo ulizikwa bila kichwa huku pia ukidaiwa kuwa na majeraha mengi mwilini kuanzia miguuni na kwenye paja lake karibu na kiuno huku kiwiko cha mkono wa kulia nacho kikidaiwa kunyofolewa.

Mwili huo uliwasili mjini moshi usiku wa kuamkia jana baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es salaam, ukitokea nchini India huku gharama zote za kuusafirisha zikibebwa na serikali ya Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari jana kabla ya mazishi, kaka wa marehemu, Maliki Mtui, alisema kuwa wameshtushwa na kifo cha ndugu yao hasa kutokana na marehemu kutokuwa na historia ya ugomvi.

Kwa mujibu wa kaka huyo, mwili huo pia umeonekana kuwa na alama za kamba kwenye mikono yake hali ambayo inaonyesha marehemu kabla ya kuuawa alifungwa kamba ili asiweze kujitetea.

Tukio hilo la kusikitisha linadaiwa kutokea katika mji wa Bangalore nchini India ambako marehemu alikuwa tayari amehitimu masomo yake ya biashara na utawala (Business Administration) na tayari alikuwa akijiandaa kurejea nyumbani.

Kaka huyo wa marehemu aliwaambia waandishi wa habari kuwa mdogo wake huyo alipatwa na mkasa huo akiwa njiani kuelekea mjini ambako rafiki yake wa kike ambaye pia ni Mtanzania aishie visiwani Zanzibar alikuwa akisoma.

“Niliwasiliana naye siku ya tukio kabla hajapatwa na mauti haya nikamuuliza anatarajia kurudi lini nyumbani akanijibu angerudi mapema na rafiki yake alikuwa akimsubiri lakini hakuweza kutokea” alisema.

Pamoja na kuishukuru serikali ya Tanzania kugharamia kuusafirisha mwili wa marehemu mdogo wake, Mtui ameitaka pia serikali kuwathamini raia wake walioko nje ya nchi kwa kufuatilia taarifa zao pindi wanapokumbwa na matukio kama hayo ya kuuawa kwa mdogo wake.

Naye msemaji wa familia ya marehemu Mtui ambaye pia ni shekhe wa msikiti wa Majengo, Shekhe Said Khatibu, alisema kuwa serikali haiwathamini raia wake walioko nje na ndiyo maana serikali haijatoa tamko rasmi kulaani mauaji hayo.

Shekhe huyo pia alisema katika kile kinachoonyesha kuwa idara za serikali zimelala, serikali imeshindwa kutuma hata mwakilishi kwenye mazishi hayo ambayo tukio lake lina utata.

Aidha, alipinga taarifa zote zilizotolewa na madaktari nchini India kwamba marehemu alifariki dunia kwa ajali ya treni na kusisitiza kuwa taarifa hizo sio za kweli.
                                             

source:michuzi.                                                                              







[ Read More ]

HABARI YA MSIBA..


Binti wa Marehemu Rashid Kawawa , Habiba Kawawa amefariki  jioni ya Leo siku chache kabla ya arobaini ya baba yake katika hospitali Ya Taifa ya Muhimbili majira ya saa kumi na Mbili Jioni….
Msiba upo nyumbani kwa Marehemu Habiba huko Tegeta
Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi..Amin..
[ Read More ]

Mwili Wa Imran Mtui Wawasili Dar Leo, Wasafirishwa Kuelekea Moshi Kwa Mazishi



Jeneza lililobeba mwili wa marehemu Imran Mtui likiingizwa kwenye gari tayari kwa kusafiri kwenda Moshi.
Dada wa marehemu na waombolezaji wakilia kwa uchungu wakati jeneza likiingizwa kwenye gari tayari kwa kusafirisha mwili kwenda moshi Mjini kwa mazishi. 


Rais Mstaafu wa Chama cha Wanafunzi waishio Bangalore (TASABA) Bw. Baraka Kange akizungumza na waandishi wa habara mara wakati wakisubiri kupokea mwili wa Mwanafunzi aliyeuwa nchini India katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) leo. Kushoto kwake ni Babu wa marehemu, Balozi Abubakar Abrahim.

source:michuzi.
[ Read More ]

MOTHER, DAUGHTER, SON COMMIT SUICIDE


  In a heart-rending incident, three members of a family committed suicide by consuming poison in Bogadi near here last night.
The deceased have been identified as Mangalamma (48), wife of Shivanna, her son Bhyrava (28) and daughter Lakshmi (22), wife of Swamy.
They allegedly ended their lives in their house behind Government School on Bogadi. Lakshmi is survived by two sons Preetham, 7, and Varun, 3. Her husband Swamy is said to be the main reason behind the trio taking the extreme step. The incident came to light when a neighbour Anitha reportedly went to the house of Mangalamma at about 6 am today.
Preetham opened the door for Anitha who found the three persons lying dead. She then informed neighbours who in turn alerted the Police.
Lakshmi, who was married to Swamy 7 years ago, was being constantly ill-treated by her husband who had turned into an alcoholic two years ago. Swamy, who owns a chicken stall in Bharathi Nagar, is said to have been assaulting Lakshmi and two children almost everyday. Attempts to reconcile the couple went in vain, according to neighbours.
Lakshmi, apparently fed up with her husband's ill-treatment, is said to have left for her parents' house along with her two children on Jan. 29.
Her father Shivanna, also said to be an alcoholic and totally non-chalant about his family affairs, was reportedly sleeping outside the house when the family members consumed poison last night.
[ Read More ]

Wanne wa familia moja wateketea kwa moto wa jenereta

WATU wanne wa familia moja wamekufa kwa moto baada ya jenereta lililokuwa limefungiwa katika moja ya chumba ndani ya nyumba hiyo kupasuka na kuwaka moto
Tukio hilo la kusikitisha limetokea usiku wa kuamka leo, huko maeneo ya Kibwenzini Zanzibar wakati watu hao wakiwa wamelala ndani humo.

Ilidaiwa kuwa jenereta hilo liliripuka majira ya saa 11 za alfajiri na kuzua moto uliosababisha vifo hivyo.

Ilidaiwa kuwa familia hiyo ilinunua jenereta hilo kwa ajili ya matumizi ya nyumbani kutokana na kukosekana kwa umeme visiwani Zanzibar.

Katika ajali hiyo waliopoteza maisha walitajwa kuwa ni Safia Shabani, Ahmed Shaban na mtoto ambaye hakuweza kupatikana jina lake, akiwemo na msichana wa kazi Sikudhani Nasorro.

Hadi habari hii inarushwa hewani, kamanda wa Polisi wa wilaya husika hakuweza kupatikana kuongelea juu ya tukio hilo juhudi zaidi zinafanyika ili kuweza kupata maelezo yake.
[ Read More ]

RIPOTI RASMI YA KIFO CHA BWANA “IMRAN MTUI”

Mnamo siku ya jumapili ya tarehe 31/01/2010, majira ya 9:30 alasiri uongozi wa wanafunzi waishio Bangalore India (TASABA) tulipokea taarifa ya kusikitisha kutoka kwa ndugu wa karibu wa marehemu kuwa kaka yetu mpendwa IMRAN MTUI kuwa tena duniani.
Mnamo majira ya saa tatu usiku mwenyekiti wa jumuiya ya wanafunzi waishio Bangalore (TASABA) Mh. Fidelis Msomekela aliwasiliana na ubalozi wa Tanzania New Delhi kuwafahamisha juu ya msiba wa mpendwa kaka yetu marehemu IMRAN MTUI.
Tarehe 1/02/2010 ofisi ya Ubalozi ilituma mwakilishi wake anayesimamia maswala ya wanafunzi India ili kusaidiana na serikali ya wanafunzi waishio Bangalore kujua chanzo zaidi juu ya kifo cha marehemu Imran Mtui.
Tarehe 2/01/2010, Mwakilishi wa ubalozi pamoja a mwenyekiti wa jumuiya ya wanafunzi Bangalore (TASABA) walifika katika kituo cha polisi kiitwacho ‘Cantonment Railway Police’ ili kupata ripoti kamili juu ya chanzo cha kifo cha marehu Imran Mtui. Ripoti ya polisi ilieleza kuwa mnamo majira ya saa 3:35 asubuhi mkaguzi wa reli alitoa taarifa kwa msismamizi mkuu wa reli kuwa ameona mwili wa marehemu IMRAN MTUI pembeni ya reli K.M No. 339/700-800 karibu na KRISHNARAJAPURAM LOCO SHED (MAHADEVAPUR, BANGALORE).
Taarifa za awali za polisi zinaeleza kuwa chanzo cha kifo cha marehemu Imran Mtui ni Ajali ya kawaida, uchunguzi zaidi unaendelea ili kujua chanzo kamili cha kifo cha ndugu yetu marehemu IMRAN MTUI.
Taratibu zote za kusafirisha mwili wa marehemu IMRAN MTUI zimekamilika, kesho (3/01/2010) majira ya jioni, mwili wa marehemu IMRAN MTUI utasafirishwa kuelekea nyumbani Tanzania kupitia kampuni la shirika la ndege la Emirates mpaka Dar es Salaam na baadae kusfirishwa kuelekea Killimanjaro kwa mazishi.
Uongozi wa Jumuiya ya wanafunzi waishio Bangalore (TASABA) unatoa shukrani za dhati kwa ubalozi wa Tanzania New Delhi kwa ushirikiano na msaada mkubwa walioutoa ili kufanikisha taratibu zote za kisheria na kutoa usafiri wa kumsafirisha ndugu yetu maarehemu IMRAN MTUI mpaka nyumbani kwao Kilimanjaro. Pia uongozi wa Jumuiya ya wanafunzi waishio Bangalore (TASABA), unatoa shukrani za dhati kwa wale wote walioungana na familia ya ndugu yetu mpendwa marehemu IMRAN MTUI kwa hali na mali.
Jumuiya ya wanafunzi waishio Bangalore (TASABA),unaomba wanajumuiya wote kuwa watulivu na kuacha kutoa habari za kizushi juu ya kifo cha marehemu IMRAN MTUI kwa kuwa uchunguzi zaidi bado unaendelea na mpaka sasa hakuna mtuhumiwa yoyote Yule anaye shutumiwa au kushikiliwa na polisi juu ya kifo hicho.
Uongozi wa wanafunzi waishio Bangalore (TASABA) unatoa pole kwa familia ya marehemu IMRAN MTUI. Mungu aiweke mahali pema peponi roho ya ndugu yetu mpendwa marehemu IMRAN MTUI. Amin

Fidelis Msomekela
President – TASABA
[ Read More ]

SURA ZA HUZUNI NA MAJONZI - BANGALORE-INDIA.

Baadhi ya wanafunzi waliokusanyika katika msiba huo wakiwa na nyuso za huzuni.


Sura za Huzuni na Majonzi kwa wanafunzi wa India waliopo Bangalore na Wenzao wa Mysore baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Muwakilishi wa Ubalozi Mr. Amon Mwamunenge juu ya maendeleo ya uchunguzi na taratibu za kusafirisha mwili wa Marehemu Imran Mtui kurudi nyumbani kwa ajili ya mapumziko ya amani.
[ Read More ]

Mwanafunzi Mtanzania, Imran Mtui auawa India



Habari zilizopo katika blogu ya Watanzania waishio Bangalore (TASABA), pia katika mtandao wa Twitter zinathibitisha kuwa, mwanafunzi wa Kitanzania, Imran Mtui (31) aliyekuwa anasoma katika Chuo kishiriki Cha Chuo Kikuu cha Bangalore nchini India, amekutwa amekufa huku mwili wake ukiwa hauna kichwa.
Taarifa zinasema kuwa mwili huo ulikutwa kando kando ya reli katika eneo la Shivajinagar katika mji wa Bangalore ukiwa hauna kichwa huku mguu mmoja ukiwa umejeruhiwa vibaya.Balozi wa Tanzania nchini India, John Kijazi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.

"Mimi nilipata taarifa hizo juzi jioni ambapo jana tulifanya kikao na wenzangu na kumtuma Ofisa wetu Mzee Amon Mwamanenge na mwanasheria wetu wamekwenda huko kupata undani wa tukio hilo," alisema Balozi Kijazi.

Alisema kuwa kwa sasa hawezi kutoa picha kamili lakini mwili wa kijana huyo umekutwa ukiwa hauna kichwa na mguu umebondeka. Kijana huyo aliyefariki alikuwa amemaliza Shahada ya Usimamizi wa Biashara (BBM) na alitambulika kwa jina la Imran Mtui. Aliwahi kuwa Mtunza Fedha wa Chama Cha Wanafunzi wa Kitanzania Waishio Bangalore (TASABA).

Habari hizi zimedhibitishwa na mdogo wa marehemu, Issa Mtui, kwa njia ya simu akiwa safarini kuelekea Marangu, Moshi. Alieleza kuwa mwili wa marehemu unategemewa kuwasili nchini Alhamisi ya wiki hii kwa ajili ya taratibu za mazishi ambayo yatafanyikia Marangu.
Imrani ni wa pili kuzaliwa kati ya watoto wanne kwenye familia hiyo. Inadaiwa kuwa kabla mauti haijamkuta alitarajiwa jana angekuwa amerejea nchini baada ya kuwa amechukua vyeti vyake vya masomo ambavyo alikuwa akivisubiri baada ya kuhitimu masomo yake.

Polisi nchini India wanaendelea na jitihada za kuwatafuta watuhumiwa wa tukio hilo.
[ Read More ]

TANGAZO..

TAARIFA KAMILI YA KAMATI YA KUFUATILIA MSIBA WA KAKA YETU IMRAN MTUI CHINI RAIS WA TASABA NA MUWAKILISHI WA UBALOZI MR.AMON MWAMANENGE ITATOLEWA BAADAE USIKU HUU.TAARIFA ITAHUSISHA TAARIFA ZILIZOTOLEWA NA POLISI,HOSPITALI NA KAMPUNI YA RELI KUHUSU KIFO CHA KAKA YETU IMRAN MTUI.TUNAOMBA RADHI KWA KUCHELEWESHWA KWA TAARIFA KWANI TULIKUA HATUWEZI KUZUNGUMZA LOLOTE MPAKA TUPATE RIPOTI RASMI YA KAMATI HII AMBAYO IMECHELEWA KUTOKANA NA SABABU ZILIZO NJE YA UWEZO WAO.TUNAKUMBUSHA YA KWAMBA TUSINGEWEZA KUANDIKA TETESI TULIZO SIKIA KUHUSIANA NA MSIBA HUU KWANI ZILIKUA NI TAARIFA ZISIZO RASMI.

TASABA SPOKESMAN
JUMANNE MTAMBALIKE
[ Read More ]