Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

Wakenya matatani Morogoro kwa Wizi

Wanawake wawili wafanyabiashara wa nchini wametiwa mikononi mwa walinzi wa raia na mali zao mjini Morogoro wakidaiwa kukwapua kitita cha fedha kiasi cha Shilingi milioni 4.4 za kitanzania.
Taarifa za kipolisi kutoka Moropgoro zinapasha kuwa wanawake hao walikwiba fedha hizo mali ya Jackson Edson mkazi wa mjini Morogoro alipo fika kuweka fedha benki ya CRDB , Morogoro.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Adolfina Chialo , aalitanabaisha hayo na  kuwataja watuhumiwa hao kuwa ni Iren Kharim na Jane Ndunilo kutoka  jiji laNairobi, Kenya.

Chialo alitoa taarifa hizo kuwa tukio lilitendeka siku ya Aprili 4 mishale ya saa 4 asubuhi CRDB tawi la Morogoro katika mitaa ya Masika na Ngoto.
Wanawake hao majasiri wanadaiwa kufanya wizi huo kwa njia ya aina yake ambayo watu wote tunaoingia benki yatupasa kuwa makini nayo ya kuombwa msaada wa kufanyiwa kitu au kuelekezwa.
“Watuhumiwa hao waliomba msaada kutoka kwa mfanyabiashara huyo wa kuwajazia fomu lakini na wakati wakipatiwa msaada huo walivuta bahasha yenye fedha hizo iliyokuwa mezani na kuondoka,”alisema Kamanda wa Polisi.

kamanda wa Polisi anasema ni Polisi jamii tu ndio iliyo okoa bulungutu hilo la fedha baada ya watu waliopo ndani ya Benki kuwataiti wakisaidiana na askari wa benki.
Baade watuhumiwa walipelekwa katika kituo cha Polisi cha kati kilichopo mjini hapa kwa mahojiano zaidi na pindi uchunguzi wa Kipolisi utakapo kamilika watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani kujibu mashtaka yao.
[ Read More ]

TANZANIA WALK OF FAME.

 

 
Hayati Steve Kanumba ni miongoni mwa wasanii maarufu wa Tanzania wenye nyota za umaarufu (Tanzania Walk of Fame) ndani ya ukumbi wa Dar Live jijini Dar Es salaam ambapo mara baada ya kifo chake wafanyakazi wa ukumbi huo na mashabiki wake wameweka mashada ya maua,kadi na kuwasha mishumaa kama ishara ya kuomboleza kifo chake. 
...baadhi ya staff wa Dar Live wakiwasha mshumaa kwenye nyota ya Kanumba
...Nyota ya Kanumba ilivyo ndani ya Dar Live katika sehemu ya Tanzania Walk of Fame.
 
picha na abdallah mrisho.
[ Read More ]

Ndege ya shirika la ndege la Tanzania (ATC) yaanguka .




Ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATC) imeanguka katika uwanja wa ndege wa Kigoma ikiwa katika matayarisho ya kupaa.Habari  zinasema kwamba abiria wote pamoja na wafanyakazi wa ndege hiyo wamenusurika.
[ Read More ]

MAMA KANUMBA KAFIKA DAR NA RATIBA YA MAZISHI RASMI



WAKATI MAOMBOLEZO YA MSIBA YAKIENDELEA VIONGOZI MBALIMBALI WAKIFIKA KUTOA MKONO WAPOLE  AMBAPO LEO MHESHIMIWA PREZIDAR J.K ALIFIKA NYUMBANI KWA KANUMBA KUTOA MKONO WA POLE, NA KESHO ASUBUHU WAZIRI MKUU MHESHIMIWA PINDA ANATARAJIWA KUFIKA  KUTOA MKONO WA POLE KABLA YA KUELEKEA MKOANI DODOMA KWA AJILI YA BUNGE LINALOANZA JUMANNE

 
 RATIBA YA MAZISHI IMETOLEWA RASMI AMBAPO MAZISHI YAMEPANGWA KUFANYIKA SIKU YA JUMANNE KAMA ILIVYOKUWA IMEPANGWA, MAREHEMU ATAAGWA KATIKA VIWANJA VYA LEADERS CLUB AMBAPO KUANZIA SAA 4 SHUGHULI ZA MISA NA KUAGA MWILI ZITAANZA NA KISHA MAREHEMU ATAZIKWA KATIKA MAKABURI YA KINONDONI JIJINI.
R.I.P KANUMBA

 

 
 MAMA MZAZI WA MAREHEMU AMESHAFIKA JIJINI  NA AMETOA BARAKA ZOTE ZA MAZISHI YAFANYIKE HAPAHAPA JIJINI
 MSALABA MWEKUNDU WAPO NA KAZI YAO INAONEKANA KWANI WATU WANAZIMIA MARA KWA MARA NAO WANAONEKANA KUFANYA KAZI YAO KWA USTADI


                                  sisi tulimpenda bali mungu kampenda zaidi
              MISA ZINAENDELEA HAPO HAPO NYUMBANI KWA MAREHEMU,HILI NI KUNDI LA WANAKWAYA WA KANISA ALILOKUWA ANASALI KANUMBA
KAMA KAWAIDA MASHABIKI WA KANUMBA WAKO NJE WAKIFUATILIA MSIBA WA KIPENZI CHAO

source 8020..
[ Read More ]

News alert:



Habari za muda huu zinaeleza kuwa Jeshi la Polisi limeanza kumhoji 'mtoto' anayeshukiwa kuwa chanzo cha Steven Kanumba (The Great), Elizabeth Michael, maarufu kwa jina la kisanii, Lulu, amekanusha kumsukuma msanii huyo nguli hadi kufa.
 Amesema kamwe hakufanya hivyo, pamoja na kwamba walikuwa wamekwaruzana kwa muda mfupi na akaenda kuoga, akiwa anatoka bafuni alianguka (aliteleza) na kugonga kichwa kabla ya kukutwa na umauti.
 Binti huyo ameiambia Polisi kwamba Kanumba (ambaye wamekuwa na uhusiano naye wa mapenzi kwa muda sasa) alikuwa 'amebugia' ujazo mkubwa wa pombe kali aina ya Jackie Daniels (JD).
 TAJOA itaendelea kuujuza umma juu ya kila kinachoendelea juu ya mkasa huu unaoonekana kuvuta hisia za Watanzania wengi na hata wale walio nje ya nchi.

chanzo TAJOA.
[ Read More ]

HABARI NA ITV:Mazishi ya marehemu Steven Kanumba

[ Read More ]

Niliyokumbana nayo fb..kifo hakitaki utani jamani.

[ Read More ]

RAIS KIKWETE AKIWA NYUMBANI KWA MAREHEMU STEVEN KANUMBA KUTOA POLE KWA WAFIWA...!!!

 

 Rais Kikwete akiweka saini katika kitbu cha maombolezo leo alipofika nyumbani kwa Marehemu Steven Kanumba maeneo ya Sinza 'Vatican' kutoa pole na rambirambi. Rais ameto ubani wa shilingi milioni 10 kwa kifo hicho ambacho kimetingisha tasnia ya filamu ndani n nje ya nchi Rais Kikwete akiongea na wanakamati wa kamati ya msiba wa Steve Kanumba 
 Rais Kikwete akiwa nyumbani kwa marehemu mapema leo alipo enda kuhani msiba
  Rais Kikwete akitoa pole kwa dada wa marehemu Steve Kanumba na chini akiwafariji
   Rais Kikwete akiongea na wafiwa
  Rais Kikwete akimpa pole mdogo wake marehemu Steven Kanumba
Rais Kikwete akisalimiana na Dokta Sheni huku Millen Magesse na wasanii wengine wakiangalia
 Rais Kikwete akiwapa mkono wa pole wasanii wa tasnia ya filamu Tanzania

Picha kwa hisani ya Michuzi Blog
[ Read More ]

HABARI ZILIZOTANDA LEO MAGAZETINI JUMAPILI APR 8 NA Millard ayo.

 



 









[ Read More ]

Kanumba (kauli yake ya mwisho) HD

[ Read More ]