Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

Nafasi ya Masomo/kusomesha Marekani


Opportunity in Swahili at The University of Mississippi

The Department of Modern Languages has funding to support someone to do a 2-year master's degree in Modern Languages with a specialization in Teaching English as a Second Language (TESL), Spanish, French or German while teaching two basic Swahili courses each semester for two years. We can offer a stipend of $5,250 per semester ($10,500 per year), which will be split between the Departments of Modern Languages and African-American Studies. This assistantship will waive both resident and non-resident tuition and will be offered for four semesters with successful academic progression toward the master’s degree. We anticipate courses with about ten students in them per semester in both Swahili 1 and 2.
This is a great opportunity to do a master's degree at UM and to get additional teaching experience in Swahili, while being completely funded to do so. For more information, please contact Dr. Donald L. Dyer, Chair, Department of Modern Languages, The University of Mississippi, University, MS 38677 [mldyer@olemiss.edu].
Dr. Donald L. Dyer
Chair of Modern Languages
Professor of Russian and Linguistics
Co-Director of the UM Chinese Language Flagship Program
The University of Mississippi
University, MS 38677
Editor of Balkanistica
Editor of Romance Monographs
[ Read More ]

Mahafali ya nane ya Chuo Kikuu Cha Taifa Cha Zanzibar.



 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(wa tatu kulia) pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA),pamoja na Viongozi wengine wa Chuo hicho wakiwa katika maandamano wakati mahfali ya nane yaliyofanyika leo katika
kampasi ya Tunguu
 Baadhi ya Viongozi wakuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar walioalikwa katika sherehe za Mahafali ya nane ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) zilizofanyika leo katika kamapasi
ya Tunguu,Mkoa wa Kusini Unguja
 Baadhi ya Viongozi wakuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar walioalikwa katika sherehe za Mahafali ya nane ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) zilizofanyika leo katika kamapasi
ya Tunguu,Mkoa wa Kusini Unguja
 \Baadhi ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) ,akitoa hutuba yake baada ya kuwatunuku Shahada,katika sherehe za Mahafali ya nane ya chuo zilizofanyika
huko katika kampasi ya Tunguu leo.
 Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) wa fani mbali mbali wakiwa katika maandamano ya sherehe za mahafali ya nane ya chuo hicho zilizofanyika leo katika kampasi ya
Tunguu,Mkoa wa Kusini Unguja
 Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) ngazi ya Stashahada ya Lugha na Elimu, wakati walipokuwa wakitunukiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(kulia) pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA), katika sherehe za mahafali ya nane ya Chuo hicho yaliyofanyika leo katika kampasi ya Tunguu

 Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) wakivaa kofia zao baada ya kutunukiwa shahada na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) , wakati wa mahfali ya nane ya chuo hicho yaliyofanyika leo huko kamapasi ya Tunguu Mkoa wa Kusini
Unguja .

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) ,akitoa zawadi kwa mwanafunzi bora katika fani ya
Cheti cha ukutubu kwa Nyezuma Hassan Juma,katika sherehe za Mahafali ya nane ya Suza,huko katika kampasi ya Tunguu leo
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) ,akitoa zawadi kwa mwanafunzi bora katika fani ya
Shahada ya Sanaa na Elimu, kwa Sabrina Saidi Rashid,katika sherehe za Mahafali ya nane ya Suza,huko katika kampasi ya Tunguu leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) ,akitoa zawadi kwa mwanafunzi bora katika fani ya Cheti cha Teknolojia ya Habari,(IT) kwa Lukuman Mohamed Bachu,katika sherehe za Mahafali ya nane ya Suza,huko katika kampasi ya Tunguu leo
    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) ,akitoa zawadi kwa mwanafunzi bora katika masomo ya
Elimu Ngazi ya Shahada Stephen Syepwa,katika sherehe za Mahafali ya nane ya Suza,huko katika kampasi ya Tunguu leo
 \Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) ,akitoa hutuba yake baada ya kuwatunuku Vyeti,Shahada na Stashahada,wa fani mbali mbali wahitimi wa Chuo Kikuu cha SUZA,katika
sherehe za Mahafali ya nane ya chuo hicho ,zilizofanyika huko katika kampasi ya Tunguu leo

 Makamo Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) Profisa Idriss Ahmada Rai,akiteta jambo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA),wakati wa Maandamano ya sherehe za mahfali ya nane ya chuo hicho zilizofanyika katika kampasi
ya Tunguu leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati)pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA),pamoja na Viongozi wengine wa Chuo hicho wakiwa katika picha ya pamoja na wanataaluma waliohitimu fani mbali mbali,baada ya
kutunukiwa Vyeti,Shahada na Stashahada,katika mahfali ya nane yaliyofanyika leo katika kampasi ya Tunguu.
[ Read More ]

Muuaji wa Marekani ‘alikuwa’ kichaa

Polisi ya Marekani inasema inawezekeana muuaji Adam Laza mwenye umri wa miaka 20 alimuuwa mama yake kwanza Nancy Lanza kwa kumpiga risasi nyumbani kwao kabla ya kufanya mauaji ya watu 26, kati yao watoto 20 wenye umri usipindukia miaka 10, kwenye skuli ya ya Newton, Connecticut, alikuwa na matatizo ya akili. Hadi sasa serikali haijazungumza hadharani juu ya kile kinachowezekana kuwa dhamira ya mauaji hayo na polisi hawakugundua taarifa yoyote ile iliyowachwa na muuaji huyo ambaye alikuwa hana rekodi ya uhalifu. Endelea…
[ Read More ]

SUZA TO CELEBRATE ITS EIGHTH GRADUATION CEREMONY


 
The State University of Zanzibar (SUZA) will celebrate its eighth graduationceremony on Saturday 22 nd
December, 2012.
 
The event will take place in its newCampus premises at Tunguu, Central District, Zanzibar South around 08.30 a.m. HisExcellency, Dr. Ali Mohamed Shein, the President of Zanzibar and the Chairman of the Revolutionary Council who is also the Chancellor of the State University of Zanzibar is expected to confer and present degrees, diplomas and certificates to the2011/2012 University graduands.
 
In this year’s graduation ceremony a total 494 graduands out of which 262(53.03%) being females and 232 (46.96%) male graduands will graduate in nine (9)different academic disciplines of Certificate in Computer Science, Certificate of Information Technology, Certificate in Librarianship and Information Technology,
Graduation     Diploma in Computer Science and Diploma in Languages with Education.
 
 
 Others areDiploma in Science with Education, Bachelor of Arts with Education, Bachelor of Science with Education and Bachelor of Science in Computer Science. SUZA iscurrently running thirteen (13) academic programmes in addition to PhD in Kiswahili,Diploma in Educational Leadership and Management, Diploma in Social Work andUniversity Qualifications Framework (Level 6) Certificate from the above mentionedprogrammes.The State University of Zanzibar has this academic year increased its numberof students who have finalized their studies compared to the last academic year asduring the previous graduation ceremony a total of 320 (155 – 48.43% females and165 – 51.56% males) graduated in six (6) different academic disciplines
 
BACKGROUND INFORMATION
 
The State University of Zanzibar (SUZA) was established by Act No. 8 of 1999 of theHouse of Representatives of Zanzibar and became operational on 26
th
September,2001.
 
The University has recently undergone a massive restructuring process movingfrom having the School of Education, Arts and Sciences (SEAS) and two (2) Institutesof Kiswahili and Foreign Languages (IKFL) along with the Institute of Continuing Education (ICE) which existed for a decade to four (4) recently introduced Schools of Kiswahili and Foreign Languages, Natural and Social Sciences, Education and that of    Continuing and Professional Education.
 
Apart from these Schools, there is oneDirectorate of Library Services and several academic departments and centres So many  other    envisaged  programmes are to be  introduced    in  the  near  future.
[ Read More ]

RAMADAN KAREEM



[ Read More ]

Harakati katika Soko la Mwanakwerekwe katika Ramadhani leo.




Harakati katika soko la Mwanakwerekwe zikiwa kama kawaida ikiwa leo ni mwezi misi rRamadhani hali sokoni hapo ikiwa y kawaidi bidhaa za futari bei ikiwa ya wastani fungu la majimbi, muhogo, viazi vikuu na maboga bei ya mwazo ni shilishi 1000 mna 2000. na Nazi zilikuwa zikiuzwa kati ya shilingi 500/= hadi 700/=.

Bei ya Ndizi mbichi chana moja huuzwa shilingi 2500/= na mkono wa Tembo ndizi moja huuzwa 1200/= na 3000/
[ Read More ]

Waziri Masoud:Sioni sababu yakujiuzulu. Asema dhoruba iliizamisha Mv. Skagit .Balozi Seif asema tukio limeitia doa serikali. Waafrika Kusini, Waisrael wazamia kuifuata



WAZIRI wa Miundombinu na Mawasiliano, Hamad Masoud Hamad, amesema haoni sababu ya kujiuzulu nafasi yake, kufuatia janga la kuzama kwa meli ya MV.Skagit iliyopoteza maisha ya zaidi ya watu 60.

Waziri huyo alieleza hayo wakati akizungumza na vyombo vya habari alipokuwa akielezea kadhia ya ajali hiyo, ambapo katika mkutano huo waziri wa Uchukuzi wa Tanzania bara Harrison Mwakyembe na Naibu wake Lazaro Nyalandu nao walihudhuria.

Waziri Masoud alisema meli hiyo ilizama kutokana na janga la kimaumbile, kufuatia upepo mkali uliosababisha mawimbi na hatimaye kuzama kwa boti hiyo.

Alisema haoni sababu ya msingi ya kujiuzulu kufuatia ajali ya kuzama kwa meli hiyo licha ya kutokea ndani ya kipindi cha mwaka mmoja tangu kuzama kwa meli ya MV. Spice Islander.

Alikiri kuwepo kwa maoni ya watu kumtaka ajiuzulu na kuwaeleza watu wa aina hiyo kuwa hakuna mtu anayeweza kuzuia majanga ya kimaumbile kama upepo yasitokezee.
"Kumekuwa na watu wanaotoa maoni juu ya suala la kujiuzulu, lakini bado hakuna mtu anayeweza kuzuiya upepo usitokee kwani hauko katika mamlaka yake",alisema waziri huyo.

"Kuna wengine wanasema tumemkosa kule sasa watanipatia kwa hili, nimeshapata taarifa kuwa kuna ‘private member’ watapeleka hoja katika Baraza la Wawakilishi ya kujiuzulu, nimeshasikia na wimbo huu unaimbwa tena na natumiwa meseji kuulizwa nitajiuzulu wakifa wangapi kwani mimi napenda kuua", alisema.

Waziri Masoud alisema kutokana na ajali hiyo haitakuwa busara kuona kwa wakati huu kuanza kuzungumzia suala hilo na badala yake waendelee kushirikiana na serikali yao kuona wanaiunga mkono katika kusaaidia maafa hayo.

Akizungumzia juu ya watalii waliopatwa katika ajali hiyo alisema ni 15, ambao wanatoka nchini Ubelgiji, Israel, Uingereza na Marekani ambapo hali zao zipo vizuri baada ya serikali kuwapatia misaada mbali mbali na inatarajia kufanya utaratibu wa kuwarejesha nyumbani kwao.

KAULI YA BALOZI SEIF
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd amesema kuwa serikali ya Mapinduzi Zanzibar imesikitishwa na tukio la pili la kuzama kwa meli ndani ya kipindi cha mwaka mmoja.

Balozi Seif alisema tukio la kuzama Mv.Skagit limeiweka serikali ya Mapinduzi ya Zanzibra yenye mfumo wa Umoja wa Kitaifa kwenye wakati mgumu kwani baada ya kuzama MV. Spice Islander I, ilijipanga kuhakikisha tukio lile halijirejei.

Alisema ni jambo la kushangaza sana, kujitokeza tukio la kuzama kwa meli likifanana na kama lile la mwaka jana, ambapo mikakati ya kuhakikisha halijitokezi iliwekwa.

Balozi Seif alisema kujitokeza tena kwa tukio hilo ndani ya kipindi cha mwaka mmoja kunaifanya serikali kuonekana haiko makini katika kusimamia mambo yake.

Balozi alisema hivi sasa serikali inafanya juhudi za kuhakikisha inafanikiwa kukamilisha uokozi ambapo kwa mujibu ya idadi ya waliokuwemo katika meli hiyo walikuwemo watu 290 ambapo watu 146 waliokolewa wakiwa hai pamoja na maiti 67, huku 77 ikiwa bado hawajapatikana.
 
WABUNGE
Wabunge wa Bunge la Tanzania walifanya ziara maalum kuwatembelea majeruhi wa ajali ya Mv.Skagit katika hospitali kuu ya Mnazi Mmoja pamoja na eneo la Maisara ambapo miili inayoopolewa hufikishwa katika eneo hilo kwa kutambuliwa na jamaa zake.

Katika hospitali ya mnazi mmoja Wabunge hao wakiongozwa na Mbunge wa jimbo la Chambani, Salum Hemed, waliwafariji wajeruhiwa waliokua wamelazwa katika wodi maalum iliyotengwa kwa ajili yao huku wakipatiwa matibabu.
 
WAZAMIAJI WAANZA KAZI
Mamlaka ya Usafiri wa Bahari (ZMA), imesema kuwa wataalamu sita wa uzamiaji kutoka mataifa ya Afrika Kusini na Israel wameanza kuisaka meli ya Mv. Skagit iliyozama Jumatano iliyopita karibu na kisiwa cha Chumbe.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Abdullah Kombo, alilithibitishia Zanzibar Leo kuwa wataalamu hao jaa wameanza kazi ya kuzamia chini ya kina cha baharini kuisaka meli.

Alifahamisha kuwa kwa mujibu wa taarifa za awali zilizotolewa na wataalamu hao zinaeleza kuwa Mv. Skagit ipo chini ya bahari umbali wa mita 28.

"Wazamiaji wamefika katika eneo meli ilipo zama na wamebaini meli hiyo ipo chini umbali wa mita 28, muelekeao wa digirii 06`26.23 kusini na digirii 039` 10.40. mashariki",alisema Kaimu huyo.

Alifahamisha kuwa watalaamu hao wa uzamiaji baharini ambao wamepiga kambi Nungwi mkoa wa Kaskazini Unguja, wameamua kufanyakazi ya ujasiri kama njia ya msaada na kwamba wamekuwa wakishirikina na vikosi vya Tanzania katika kazi hiyo.

Miongoni mwa vikosi wanavyoshirikiana nanyo ni pamoja na Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo (KMKM), Kikosi cha Majini cha Jeshi (NAVY) na wazamiaji wengine wa kienyeji.
 
CHANZO CHA AJALI
Kaimu huyo alisema chanzo cha kuzama kwa MV. Skagit kimetokana na hali mbaya ya hewa wakati kikianza safari yake kutoka jijini Dar es Salaam kuelekea bandari ya Malindi iliyopo Zanzibar.

Alisema wakati chombo hicho kikikaribia kisiwa cha Chumbe, kulikumbana na mawimbi makali yaliyotokana na dhoruba iliyotoka upande wa kusini.

Kombo aliwataka wananchi kutofautisha mazingira yaliyosababisha kuzama kwa MV. Spice Islander na tukio la kuzama kwa MV. Skagit ambapo tukio la juzi lilisababishwa na hali mbaya ya hewa iliyotokana na kuchafuka kwa bahari.

Kaimu huyo alisema kwa mara ya mwisho MV.Skagit ilifanyiwa ukaguzi (survey), mwishoni mwaka uliopita na kwamba kiliridhisha na kupewa idhini ya kusafirisha abiria na mizigo.

Akizungumzia juu ya tuhuma za marekebisho ya uundwaji wa meli hiyo, alisema hawezi kueleza jambo lolote kwani harakati zote za usajili wa meli hiyo zilikuwazimeshafanyika awali kabla ya kukaimu nafasi hiyo.

"Mimi naingia taratibu hizo zimeshafanyika hivyo siwezi kuthibitisha hilo", alisema Kombo.

MISAADA YAANZA KUTOLEWA
Kufuatia kuzama kwa mei hiyo misaada ya pole imeanza kutolewa ambapo jana Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), kila mfuko uliwasilisha shilingi milioni 10 kama ubani kwa wafiwa na majeruhi.

Misaada hiyo alikabidhiwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi katika ofisi yake ndogo iliyopo katika jengo la Baraza la Wawakilishi liliopo Mbweni nje kidogo ya mji wa Zanzibar.

Balozi aliishukuru mifuko hiyo kwa misaada yao hiyo waliyoitoa na kuwaonea huruma wale waliofikwa na janga hilo.
[ Read More ]

MAHAKAMA YATUPILIA MBALI OMBI LA LULU


Lulu (katikati) akiingia mahakamani na askari magereza wa kike.
Kamera zikimfuata kwa shauku.
Hapa ni karibu na mlango wa kuingia katika chumba cha mahakama.
Msanii wa filamu za maigizo nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’, leo amepandishwa tena kizimbani mara ya tatu katika kesi ya mauaji ya Kanumba inayomkabili ambapo mawakili wanaomtetea wakiongozwa na Kennedy Fungamtama waliwasilisha ombi la kurekebisha umri wa mshitakiwa huyo kuwa miaka 17 na si 18 kama ilivyowasilishwa mahakamani hapo.
Fungamtama na jopo lake walisema mteja wao ni mtoto mdogo hivyo kesi hiyo ipelekwe mahakama ya watoto na kuwasilisha cheti kinachoonesha ana umri wa miaka 17. Upande wa mashitaka umetupilia mbali ombi hilo na kudai cheti kilichowasilishwa kina mapungufu kadhaa likiwemo jina la Dyana ambalo halijawahi kusikika likitu iwa na mshitakiwa huyo.
[ Read More ]

MKAPA KIZIMBANI MAHAKAMA YA KISUTU


Mkapa akiingia Mahakama ya Kisutu kutoa ushahidi.
Akisindikizwa kuelekea kizimbani.
Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, leo amepanda kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam na kuhojiwa na mawakili wa serikali na wanaomtetea aliyekuwa balozi wa Tanzania nchini Italy, Costa Mahalu, kwenye kesi ya ufujaji fedha katika ununuzi wa jengo la ubalozi inayomkabili balozi huyo.
Jengo hilo lilinunuliwa kwa shilingi, bilioni 2.9.
PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS / GPL
[ Read More ]

TUMSAIDIE WASTARA NA SAJUKI KWENYE HILI















Mimi na wewe tuungane Tumsaidieni ndugu yetu msanii wa filamu SAJUKI anaumwa na


anahitaji kwenda kutibiwa INDIA mapema iwezekanavyo!! Waweza kumchangia kupitia 


AKIBA BANK Account number 050000003047 Jina la mwenye account ni mkewe 


WASTARA JUMA au M PESA Number 0762189592
[ Read More ]