Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

Majambazi waua askari 2 Zanzibar

-
Rehema Mwinyi.

Askari wawili wa Kikosi cha Valantia kinachomilikiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), wameuawa na majambazi wakati wakilinda kituo cha mafuta cha Mwanakwerekwe mkoa wa Mjini Magharibi kisiwani Unguja. Askari waliouawa ni Taibani Mikidadi Ali (23) na Juma Mcha Ali (25) ambao walijeruhiwa na majambazi hao kwa risasi kichwani na kifuani.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Bakari Khatib Shaaban, alikiri jana kutokea kwa tukio hilo saa mbili usiku juzi, baada ya majambazi kuvamia kituo hicho kwa lengo la kupora fedha. Katika purukushani hizo, majambazi hao walifyatua risasi na kuwaua walinzi wawili wa Valantia waliokuwa wakilinda kituo kinachomilikiwa na kampuni ya Zanzibar Petroleum. Katika tukio hilo, majambazi hao walipora silaha aliyokuwa nayo mmoja wa walinzi hao, ikiwa na risasi 10. Jeshi la Polisi linamshikilia Gideon Simponda kwa uchunguzi baada ya kukiri kumiliki gari namba ZNZ 634 ambalo lilitumika katika tukio la ujambazi.

“Kwa sasa, Jeshi la Polisi linamshikilia Gideon Leonard Simponda kwa uchunguzi zaidi...yeye alijitokeza na kusema anamiliki gari ambalo liliporwa na baadaye kutelekezwa,” alisema Kamanda Shaaban. Aidha, polisi waliipata silaha iliyoporwa na majambazi hao aina ya Rifle yenye risasi 10. Kamanda alisema hata hivyo majambazi hao hawakuondoka na fedha ila walimjeruhi Bilali Omar ambaye alikuwa mpita njia eneo hilo, na amelazwa katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja kwa matibabu. Askari wa vikosi vya SMZ hutumiwa kulinda vituo mbalimbali vya mafuta na taasisi nyingine za watu binafsi zikiwamo benki.

Leave a Reply