Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

ATAPELI MILIONI 5/- AKIDAI ANAWEZA KUMFUFUA MTOTO

-
Rehema Mwinyi.

MGANGA wa Kienyeji, Jongo Salum, maarufu kwa jina la Dk. Manyaunyau, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam kwa tuhuma za kujipatia sh milioni 5 kwa njia ya udanganyifu, kwamba angeweza kumfufua mtoto aliyefariki dunia.

Mwendesha Mashitaka Mkuu wa mahakama hiyo, Naima Mwingi, alidai kuwa Dk. Manyaunyau (29), alijipatia kiasi hicho cha pesa kutoka kwa Zufa Abubakari, ili amfufue mtoto wake aliyedai amefariki dunia katika mazingira ya kishirikina.

Naima, alidai mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Samwel Maweda, kwamba Dk. Manyaunyau, mkazi wa Tabata Mawenzi, alitenda kosa hilo kati ya Agosti 2, 2007 na Machi 3 mwaka jana, maeneo ya Tabata Mawenzi katika Wilaya ya Ilala.

Hata hivyo, mtuhumiwa alikana kosa hilo na kuachiwa huru kwa dhamana hadi Julai 21, kesi yake itakapotajwa tena, na upepelezi bado haujakamilika.

Wakati huohuo, mfanyabiashara Henry Hadson Mwasongwe (42) mkazi wa Tabata, amepandishwa katika mahakama hiyo kwa tuhuma za kujipatia milioni 14/- kwa njia ya udanganyifu.

Mwendesha Mashtaka, Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga, alidai mbele ya Hakimu Mfawidhi, Joyce Minde kwamba, mtuhumiwa alitenda kosa hilo kati ya Desemba 11 na Machi 3, mwaka huu katika eneo la Ukonga, jijini Dar es Salaam.

Mtuhumiwa alikana kosa hilo na kurudishwa rumande baada ya kukosa dhamana hadi Juni 15 kesi hiyo itakapotajwa tena.

Leave a Reply