Banner 468

1234453_10201664080105694_1716282793_n
Facebook

Watoto wanne Dar watiwa mbaroni

-
Rehema Mwinyi.

Jeshi la Polisi Jijini limewatia nguvuni watoto wanne wakituhumiwa kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya.

Kukamatwa kwa watoto hao ni muendelezo wa msako unaendelea kwa ajili ya kukabiliana na watu wanaofanya vitendo vya kihalifu katika maeneo mbalimbali ya Jiji.

Akiongea na gazeti hili, Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Faustine Shilogile amesema watoto hao ni mingoni mwa watu 12 waliokamatwa katika msako uliofanywa kwenye maeneo tofauti ndani ya wilaya ya Ilala.

Amesema katika tukio la kwanza, mtoto Omar Ramadhani, 16, alikamatwa akiwa na wenzake saba wakiwa na bangi kete 24, misokoto 400 pamoja na pombe ya gongo lita 11.

Amesema watu hao walikamatwa jana majira ya saa 3:00 asubuhi baada ya raia wema kutoa taarifa zao.

Amewataja watuhumiwa wengine kuwa ni Khamis Maulidi, 20, Issah Athumani, 21, Joseph Nakati, 23 na wenzao wanne.

Kamanda Shilogile amesema katika tukio la pili, watu wanne walikamatwa huko eneo la Gerezani wakiwemo watoto watatu wakiwa na bangi puli moja na misokoto 211.

Amesema watu hao walikuwa katika harakati ya kutafuta wateja.
Amewataja watu hao kuwa ni Yahaya Ali, 16, Pascal Haruna, 26, Aidina Mgaika, 15 na Abdul Khalfani, 14, wote wakazi wa eneo hilo.

Kamanda Shilogile amesema jeshi hilo linaangalia namna nzuri ya kuwafungulia kesi watoto hao huku watuhumiwa wengine wakitarajia kufikishwa mahakamani wakati wowote.

Leave a Reply