Hata hivyo mlinzi wa mwanasiasa huyo amesema Bwana Dabo alikuwa amelala na mke wake nyumbani kwake wakati watu waliokuwa na sare za kijeshi walipomfumania na kumuua.
Waziri wa zamani wa Ulinzi Helder Procea na walinzi wake wawili pia waliuawa kwenye operesheni hiyo.
Wizara ya Mambo ya Ndani imemtaja Bwana Proenca kama kiongozi wa njama ya kuipindua serikali.
Bwana Dabo alikuwa waziri wa Serikali na mwandani wa karibu wa Rais Joao Bernado Viera ambaye aliuawa na wanajeshi mwezi Machi.
Mauaji hayo yametekelezwa wiki tatu kabla ya uchaguzi wa urais kufanywa, hali inayozua wasi wasi kuwa huenda jeshi likaendelea kuingilia siasa nchini hiyo.
Guinea Bissau imetajwa kama moja ya maeneo muhimu ya ulanguzi wa mihadarati na hasa, Cocaine. Wadadisi wanahofia kuwa taifa hilo sasa liko katika hatari ya kudhibitiwa na mababe wa biashara hiyo haramu