wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wamefunga barabara na kuharibu gari katika eneo la Mabibo baada ya kukasirishwa na wenzao wawili kugongwa na pikipiki na kuwajeruhi juzi usiku. Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema hayo jana Dar es Salaam na kuwataja wanafunzi waliogongwa ni Ibrahimu Mkama (25) na Sayelo Daniel (30), ambao walitibiwa chuoni hapo baada ya kupewa na polisi fomu maalumu ya matibabu.
Walipata majeraha madogo. Alisema baada ya kutokea kwa tukio hilo, wanafunzi hao walizingira eneo hilo na kufanya fujo kwa magari yanayopita katika barabara hiyo na kuliharibu gari aina ya Toyota DCM ambalo walivunja vioo vya gari hiyo vya pembeni na kuongeza kuwa hakuna abiria aliyejeruhiwa kutokana na tukio hilo.
Alibainisha kuwa kutokana na fujo hizo, hakuna mwanafunzi ye yote anayeshikiliwa kutokana na tukio hilo na kuwa upelelezi kuhusu tukio hilo unaendelea ambapo Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kinondoni na Polisi inafanya mazungumzo na uongozi wa Serikali ya Wanafunzi wa chuo hicho (DARUSO) ili kubaini madai ya wanafunzi hao na chanzo cha tukio hilo. Katika tukio jingine, raia wenye asili ya Kiasia, wenye uraia wa nchi mbili tofauti wamekutwa wamekufa katika Hoteli ya Harbour View Suit iliyopo katika Mtaa wa Samora Dar es Salaam.
Kamanda Kova alisema vifo hivyo viligundulika saa 8:00 mchana juzi na kuwataja waliokufa kuwa ni Salman Zuberi (41) na Yusuph Sader (33), waliokutwa vyumbani mwao wakiwa wamekufa. Alisema raia hao walikutwa na pasipoti za kusafiria za nchi zao ambapo Zuberi alikutwa na pasipoti yenye namba JX 276017 ya Canada na Sader pasipoti yake ni namba 459639277 ya Afrika Kusini ambapo katika vyumba walivyofia kulikuwa na mazingira tofauti, yakiwamo ya maiti kukutwa na mate na dalili za matapishi. Polisi inachunguza vifo hivyo.
Categories: